Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,129
18,743
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
 
Kama kasema ukifilisika ni shauri yako hatakudai.... kwanini akulazimishe uache kazi? Kama kaamua kukupa mtaji si akuache upange unavyoona inafaa???

Nina mashaka na huo msaada
 
Anasema eti nikiendelea kufanya kazi sintakuwa committed na jambo nitakaloanzisha, kwa kuwa always ninakuwa najua hata nikivurunda bado nina kazi yangu. Anasema lazima nitambue factor ya risk - kwamba nikizifuja sina cha kusimamia, na sina kazi tena, ndio maana anasema nikifilisika ni shauri yangu
 
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Chukua hiyo hela alafu weka kwamza fixed deposit huku ukiwaza nini chakufanya
 
Kwa ufupi,nduguyo anataka akupe kiinua mgongo na mtaji kidogo kwa hiyo 200 milioni.Tulia.Piga hesabu.Tafakari biashara endelevu ya kufanya.Hiyari yashinda utumwa.
 
Omba likizo ya mwezi mmoja. Muambie ndugu yako kuwa umeacha kazi.

Tumia mwezi huo kujihakikishia kama ndugu yako atakutumia hiyo fedha lakini pia kufanya research ya biashara gani ya kufanya.

Kama kweli atakuingizia kitita kizima, basi fanya kazi ulichokiona kitakupa matokeo.

Ila ukipata kiasi chote, tumia walau 50M. Hiyo 150 iache kwanza uone matokeo ya uwekezaji wa kwanza.
 
Anasema eti nikiendelea kufanya kazi sintakuwa committed na jambo nitakaloanzisha, kwa kuwa always ninakuwa najua hata nikivurunda bado nina kazi yangu. Anasema lazima nitambue factor ya risk - kwamba nikizifuja sina cha kusimamia, na sina kazi tena, ndio maana anasema nikifilisika ni shauri yangu
Na hizo hela anakutumia baada ya kuacha kazi au kabla hujaacha kazi?
 
Sikushauri kuacha kazi, kama mtu unaamua kumpa mtu mtaji na huna mpango wa kumdai kwanini uweke sharti la kuacha kazi? Ukaanzishe biashara huna hata idea nayo unafanya pata potea. Akupe mtaji na kazi usiache.. anzisha biashara kwa kiasi kadhaa then uone biashara inakwendaje ukiwa stable na kuimudu ndo ufikirie kama uache kazi au laa
 
Hiyo milioni 200 Nunua bitcoins halafu endelea kupiga kazi mwisho wa mwaka unaweza ukawa na bilioni 1 au milioni 200🐒
Okay. Ila ufahamu wa Bitcoins ndio sina kabisa. Ngoja nifanyie research nijieleweshe zaidi. Tanzania inaruhusu?
 
Bujibuji acha mzaha, this is serious, nategemea hekima zako!😄

By the way, wife anapinga kabisa suala la kuacha kazi!
Biashara NAYO ni kazi. 200 ml ni mtaji wa maana kabisa unaoweza kubadilisha maisha ya familia yako completely.

Kaa chini na mkeo, mwelimishe faida za kujiajiri .
Ukipata wazo LA biashara mshirikishe na umfanye kuwa partner in business, atakuamini na kuithamini biashara yenu
 
Back
Top Bottom