Nilesh: Pesa nilizompa Heche hazikuhusiana na CHADEMA

Nilesh: Pesa nilizompa Heche hazikuhusiana na CHADEMA

Nilesh kashajichanganya sana hadi hapa. Ikumbukwe huyu Gabachori ndo alimjengea hekalu manzi fulani slayqueen wa town. Kwamba Heche ni mfanyabiashara wa mafuta ni utetezi wa kipumbavu sana. Mara zote Heche amekuwa akijinadi kuwa ni mfugaji na mkulima. Kimsingi inaonekana baadhi ya walioichangia CCM ndo wanaichangia CHADEMA pia.
 
Erythrocyte Retired zitto junior mnaona nililosema, kunatatizo hapa!
Tatizo liko wapi? Sasa pesa za biashara binafsi zinahusiana nini na ufisadi kwenye chama? Ingekua za chama tungesema ni wizi ila binafsi hazihusiani hata lissu nakumbuka aliwahi kuchangiwa pesa binafsi za gari mpaka CCM na unafki wao kupitia makala wakachangia hela hadharani na ilibaki ni personal issue wala haikua ya chama.
 
Nilesh kashajichanganya sana hadi hapa. Ikumbukwe huyu Gabachori ndo alimjengea hekalu manzi fulani slayqueen wa town. Kwamba Heche ni mfanyabiashara wa mafuta ni utetezi wa kipumbavu sana. Mara zote Heche amekuwa akijinadi kuwa ni mfugaji na mkulima. Kimsingi inaonekana baadhi ya walioichangia CCM ndo wanaichangia CHADEMA pia.
Unaongea kama mama hipoppotumus.
 
Mdosi ajiandae kusakamwa na TRA, Polisi, TAKUKURU etc
Hata heche ajiandae. Kesho heche chadema ikishika madaraka, biashara za huyo mdosi zinaweza kuguswa ikigundulika kuna mafyongo?

We have to be smart than this. Matatizo tunayokumbana nayo chanzo ni kutelekeza azimio la Arusha.

Bila marekebisho, ccm itatoka madarakani lakini kina abdul mtaendelea kuwa nao kwa majina mengine.
 
hivyo, Nilesh amesisitiza kuwa katika tukio husika, hakukuwa na uhusiano wowote kati ya fedha hizo na chama cha CHADEMA
Hata uliweke kwa namna gani swala kama hili; haya ni matope yaliyochanganywa na kinyesi yanayopakwa kwa Heche.
Ukishahusishwa na mapapa ya uovu kama haya kwa namna yoyote ile, unajiweka katika hali ngumu sana ya kuaminiwa na jamii. Unaua imani yako kwa wananchi wanaokutegemea kwenye uongozi.

This is terrible news fo Heche.
 
Mfanyabiashara Nilesh amefafanua kuwa fedha alizompatia mwanasiasa John Heche hazikuwa na uhusiano wowote na shughuli za kisiasa au chama cha CHADEMA, bali zilikuwa sehemu ya mahusiano yao ya kawaida ya kibiashara na kirafiki.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Nilesh alisema Heche ni mfanyabiashara mwenzake katika sekta ya mafuta nchini Kenya, na kwamba mara kadhaa wamekuwa wakisaidiana kifedha kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu.

"Ninachotaka kuweka wazi ni kwamba fedha nilizompa Heche si za CHADEMA wala hazikuhusiana na shughuli zozote za kisiasa. Heche ni mfanyabiashara mwenzangu upande wa mafuta nchini Kenya, hivyo kumpatia fedha kwa ajili ya shughuli zake binafsi ni jambo la kawaida kwetu na si mara ya kwanza kufanya hivyo," alisema Nilesh.

Alisisitiza kuwa uhusiano wao umejengwa katika biashara na kuaminiana kwa muda mrefu, hivyo hakuna sababu ya kuhusisha msaada huo na masuala ya kisiasa.

Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na mijadala mbalimbali kuhusu chanzo na matumizi ya fedha zinazohusishwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa. Hata hivyo, Nilesh amesisitiza kuwa katika tukio husika, hakukuwa na uhusiano wowote kati ya fedha hizo na chama cha CHADEMA.

Aidha, ametoa wito kwa umma kuepuka kueneza taarifa zisizothibitishwa ambazo zinaweza kupotosha ukweli na kuharibu sifa za watu bila ushahidi.
View attachment 3633374bila ushahidi.
Sauti ya video au hata audio tu iko wapi ya huyu anayezungumza haya...?

Hii ni pure script iliyotengenezwa tu na walewale wanaotafuta mlango wa kuingilia ili kumpa kashfa John Heche...

Mimi sioni wakifanikiwa....

Pamoja na kumjua John Heche vyema, yaani leo kupitia JF ndo nasoma hizi rumours kuwa kumbe huyu John Heche ni mfanyabiashara wa mafuta (haijafafanuliwa ni mafuta ya nini kula, kujipaka au petroleum)

Na cha ajabu kumbe biashara yenyewe ya mafuta, huyu John Heche anaifanyia Kenya, sio Tanganyika🤔🤔🤔

Bado tu hawa wapiga propaganda, wanashindwa ku - execute vyema hizi propaganda zao...
 
Kumekucha,
chanzo kifo cha dereva Suez Daniel Maradufu chaanza kujidhihirisha 🐒
Screenshot_20260714-183814~2.png
 
Hata uliweke kwa namna gani swala kama hili; haya ni matope yaliyochanganywa na kinyesi yanayopakwa kwa Heche.
Ukishahusishwa na mapapa ya uovu kama haya kwa namna yoyote ile, unajiweka katika hali ngumu sana ya kuaminiwa na jamii. Unaua imani yako kwa wananchi wanaokutegemea kwenye uongozi.

This is terrible news fo Heche.
Umeiamini habari hii? Imeingia kabisa kichwani mwako ndugu Kalamu kiasi cha kusema "this is terrible news for John Heche?" Really?

Kumbe, you can simply be carried away by fake news jus like that...?

SIKILIZA BHANA, HAKUNA JIPYA HAPA KWA SABABU;

Bado ni tuhuma zilezile kama zilivyoanza....

Tofauti na mwanzo, this time wamemtaja na mtu anayedaiwa kumpa John Heche fedha....

Kusema tu ni rafiki wa Heche kibiashara na huwa anampa pesa mara nyingi tu bado haithibitishi kuwa hii ni kweli na sio uongo wenye nia ovu...

Hata hivyo, kasoro kubwa ya uongo huu kiasi cha wahusika watengeneza uongo huu kubaki wanapiga marktime palepale ni;

1. Mleta taarifa hataji ni fedha kiasi gani...

2. Mleta taarifa hatuambii, huyu Nilesh alimpa John Heche hiyo fedha lini na kwa njia gani? Je, cash in hand au kupitia bank..?

3. Benki Account gani? Jina la Benki na ilikuwa lini...?

4. Hiyo Kampuni ya mafuta ya John Heche inaitwaje jina lake...?

5. KUBWA ZAIDI KULIKO YOTE NI HILI: Katika tuhuma kama hizi, ushahidi wake ulipaswa umwoneshe huyo Nilesh mwenyewe akizungumza haya. Lakini, maneno tu bila uwepo wa muhusika inabaki ni hadithi ya kutungwa tu katika corridor za Lumumba kwa msaada wa TISS lengo likiwa lile lile linalojulikana na kila mmoja wetu..

NB: Lengo la propaganda hii ni kumfanya John Heche apoteze focus kwenye kile anachokisimamia na aanze kupoteza muda wake kujibu tuhuma zisizo na kichwa wala miguu kama hizi. Na ofcoz, lengo la waandaa propaganda hii ni kuleta mgawanyiko ndani ya CHADEMA kwa baadhi ya watu waanze kupoteza imani na kiongozi wao. Kikubwa kabisa ni kuwa huu ni uongo wa mchana kweupe, but let's see how John Heche and CHADEMA by in larger will handle this without causing damage...
 
Umeiamini habari hii? Imeingia kabisa kichwani mwako ndugu @Kalamu kiasi cha kusema "this is terrible news for John Heche?" Really?
Niweke sawa mkuu ''The Palm Beach'. Mimi nimeichukulia kama ilivyo wekwa hapo; sina la zaidi ya hilo.

Labda kweli, nilikosea kutoi'qualify' kwa kuandika:: "Kama taarifa hii ni sahihi"

Sasa, kama kweli kuna chembe hata ndogo tu ya hiyo taarifa ya huyo Nilesh kuwa na ukweli; italazimu Heche atoke na kuitolea taarifa hiyo usahihi wake.
And that will be terrible!
Ile tu kuwa na uhusiano na kampani ya watu kama hawa; na hasa nyakati kama za sasa, that is a terrible miscalculation on the part of Heche.

Hawa ni aina ya watu wa kukaa nao mbali kabisa kwa wakati huu..
There's nothing good that can come out of such a relationship na watu wa aina hii.
 
Hata yule Mfanyabisara Turky aliyetoa pesa za kulipia ndege Lissu apelekwe Nairobi ilibidi ajieleze sana kwenye media maana alionekana mhaini na unfortunately alifariki miaka michache baadae.
Sad country. Wangeacha wengine pia wapate kama wapatavyo wao CCM
Acheni Kuleta taharuki Turky ilikua Natural death aliigua na akafa mwaka 2020. Lakini ukisaidia Wahuni lazima credibility yako iwe questionable
 
Back
Top Bottom