Nilaumu macho yangu Au moyo, niambieni?

Nilaumu macho yangu Au moyo, niambieni?

Wewe ndo umeniambia leo dear, ila mie nakupendaga toka meingia humu!

Mie namtukuza Mungu kwa hilo, kama naonekana wa heshima! Pongezii ziende kwa mamangu mimi jamani!!!
Ukipitia pm yako ambayo umechati na mimi utaona.
Uwiiii kumbe unanipendaga, acha niaenze kutembea kifua mbele.
 
Moyo umesalitika na sababu macho yangu
Na ninadhirika nimekiri wenzangu
Mwisho nitafedheheka kupenda kitu si changu
Ni laumu macho yangu au moyo nambieni?

Umeuliza swali jawabu nakuletea
Uwamuzi wa halali hukumu isiyo hatia
Itakuwa ni muhali kimoja kukionea
Laumu vyote viwili usilaumu kimoja

Macho yangu yamenena lawama hizi si zangu
Mie kweli nimeona hazifumba mboni zangu
Moyo subira hauna niutendeje wenzangu?
Nilaumu macho yangu au moyo nambieni?

dah huu wimbo original version aliimba marehemu maulid machaprala.
mungu amlaze pema peponi.

mimi nitalaumu viungo vyote viwili
 
Back
Top Bottom