Nikiweka fixed deposit 10M naweza kulipwa kiasi gani na bank kila mwezi?

Lipo mkuu ongea na watu vizurii ila hizi bhangiiii..eti mil 10 ajenge hostel..

Ujue hadi nmeogopa nikasema hivi me ndio sioni hizi fursa yani nimeenda kutafuta kiwanja cha million 8 huko pori kumbe karibu na vyuo vikuu kuna maeneo ya million 3 tu kwahiyo ningeongeza million 2 tu ningejenga na hostels niwe navuta mpunga tu saa hizi

JF DAH.
 

Ujue hadi nmeogopa nikasema hivi me ndio sioni hizi fursa yani nimeenda kutafuta kiwanja cha million 8 huko pori kumbe karibu na vyuo vikuu kuna maeneo ya million 3 tu kwahiyo ningeongeza million 2 tu ningejenga na hostels niwe navuta mpunga tu saa hizi

JF DAH.
Kijanaa hajuii hata thamani ya kiwanjaa huyooo akisikia mil 10 anahisii ni helaa flanii ya kufanya maajabuu.
 
Millioni kumi. Tafuta chuo kikuu haps dsm chenye demand kubwa ya wanachuo , angalia eneo zuri ununue ujenge vyuumba vya kupsngisha wanachuo tena kama ukipata eneo la million 3 , ukajenga vyumba 15 (au ndan yake 6 ni self) ukaongezea pindi ikipelea ,,aseewe hiyo investment itazalisha hela Vitukuuu na vining'ina....
Motivation speaker naona uko kazini.
 
10M bodaboda 4 hapo.
Bodaboda 1 kwa siku 10,000. X 4= 40,000 kwa siku.
40,000 x 30 = 1,2000,000 kwa mwezi.

Hio 1,2000,000 unaweka vijana wa kuuza chipsi kuku kwa siku wakupe 20,000. Kwahio 20,000x30= 600,000.
Bodaboda 1,2000,000 + chipsi kuku 600,000 = 1,8000,000 kwa mwezi.

Unafungua mkahawa
Unafungua wakala wa vinywaji
Unafungua wakala wa mpesa
Unafungua
Unafungua
Unafungua

Usiweke hela bank wakupe faida ndogo tumia akili yako ndogo uweke hela kubwa. Usifanye kazi kwa kupata hela, Bali tumia hela ilete hela.
Hizo ni hesabu tu ila ingiza ela uone zinavyo kataa
 
Watu wengine hua mnafurahisha sana. Jiulize hiyo Milioni 10 anayotaka kuiweka benki ili awe anapata gawio bila kufanya kazi ameitoa wapi? Yani 10 Milioni ameitoa wapi? Ameiokota? Ujue sometimes muwe mnfkr pande zote. Lengo la jamaa kuweka huko itakua Kuna mchongo anausoma. Mm nimeweka UTT lengo ni kusoma game maana biashara niliyokua naifanya ikanipa hiyo 10m kwa sasa haisomeki so nimeamua niweke UTT ili niwe napata hela nikisubiri mambo yakae sawa. Je hili ni kosa? Tufikiri kwa mapana na marefu kabla ya kutoa maoni
Pesa za wizi au savings au madili tuu ila ingekuwa ya jasho Wala asingeuliza Cha kuifanyia
 
Mkuu biashara ya boda boda anae pata faida ni dereva. Twende taratibu utanielewa. Tufanye umenunua piki piki hadi inaingia barabarani umetumia 2.5m ,hesabu kwa siku elfu 10 kwa mwezi laki tatu kwa mwaka hadi mkataba unaisha utakua umeingiza 3.6m .sasa toa gharama uliyo nunulia hiyo piki piki una baki na 1.1m , Gawanya hiyo pesa kwa miez 12 uone kwa mwezi unapata kiasi gani na ukipata kwa mwezi gawa kwa siku 30 uone kwa siku moja unapata kiasi gani. Hapo utajua wewe uliye wekeza 2.5m na dada anae saidia mama ntilie na kulipwa buku 3 mpo sawa

sipingi mkuu,nshafanyaga hiyo hesabu nmejionea
 
Ukicheki calculator yao riba inasoma 9.5 ila ukienda kuweka unaletewa risiti inasoma 5 au 6 percent… ukilalamika wanakupa semina ooh hii imekosewa mara hii sio riba ya fixed kuna sijui uwekezaji wa maisha , kimsingi maelezo yao hayaeleweki
Hii ni ukweli mkuu na mimi nilideposit 1M nikijua rate ni 9.5% ila nikapewa karatasi et rate ni 3.5% duuh nilichoka. Sikua na matumizi nayo muda ule basi nikaondoka. Nadhani hii issue ya fixed ni biashara ya benki kujipatia pesa za kurun activities na wateja hawaelewi.
 
Back
Top Bottom