Nikisafiri kwenda sehemu sipendi kufikia kwa Mtu

Haya mambo ni kawaida, na commonsense
Ukiwa na pesa utafikia hoteli za hadhi, ukiwa mnyonge ndio itapidi ukajibane kwa jamaa japo wao na wewe unajua ni shida tupu kwenu wote
 
Mwenyewe automatically nimejikuta hivyo.
Hasa mjini labda nikienda village.

Sababu ni ratiba. Sipendi kibadili ratiba zangu kisa mtu mwingine. Muda wa kuongea na watu wangu wa karibu, napenda kusoma sana na sipendi kelele. Siangalii TV, aina ya vyakula ninavyotaka vitawapa shida, napenda kuandika, Napenda maombi ya Muda mrefu, napenda kusikiliza Hymnals.
Yote hayo mara nyingi kila ninapoenda naonekana wa ajabu

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Nikafikia kwa ndugu yangu, picha linaanza siku ya kwanza nyumba nzima wamefunga(fasting)namimi wanataka nifunge nikawakubalia kishingo upande.

Alfajiri ya saa kumi na moja naamshwa kwenye maombi, hamna kitu sipendi kama kuamshwa alfajiri, kulivopambazuka nikafua kashati kangu, mida ya tea tukagonga tea, ikaja kusoma bibilia tulivomaliza kusoma nikoga nikavaa shati langu nikabeba rasket yangu huyooo nikayeya.

Nilipanga kukaa siku tatu lakini ilinilazimu kuondoka, yaani nishindwe kuvuta embassy kisa ulokole wenu.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi kwenda mkoa fulani nikamtaarifu ndugu yangu kuwa nitakuwa huo.....akanisihi sana nifikie kwake....nikaona haina shida......aisee nilijuta ule uamuzi........

Nilikuwa najiweza hata kukaa hotel lakini nikasema nisimkwaze ndugu yangu.....

Nafika pale mapema kidogo tunapiga Stori za hapa na pale muda wa kulala napelekwa chumba cha watoto na humo kuna watoto kama wanne na wawili natakiwa kulala nao......

Vyakula sasa ndio adhabu......nilikuwa kila asubuhi nikienda kwenye mambo yangu namuachia jamaa kiasi cha pesa ili aongezee kwenye bajeti yao ili tufurahie maisha..... lakini matokeo yake mkewe anatulisha vitu vya ajabu......

Kila siku ugomvi na mkewe mimi ndio muamuzi....muda mwingine ugomvi ukizidi hakupikwi......

Nilikaa pale kama wiki hivi niliona kama nimekaa mwezi........

Kwa sifikirii tena kufikia kwa mtu nikisafiri.......
Hahahaha,kwa hiyo walikua hawagombanii chumbani kwao?Pole.
 
Mwenyewe automatically nimejikuta hivyo.
Hasa mjini labda nikienda village.

Sababu ni ratiba. Sipendi kibadili ratiba zangu kisa mtu mwingine. Muda wa kuongea na watu wangu wa karibu, napenda kusoma sana na sipendi kelele. Siangalii TV, aina ya vyakula ninavyotaka vitawapa shida, napenda kuandika, Napenda maombi ya Muda mrefu, napenda kusikiliza Hymnals.
Yote hayo mara nyingi kila ninapoenda naonekana wa ajabu
Angalau wewe una sababu za msingi.
 
Niliwahi kwenda mkoa fulani nikamtaarifu ndugu yangu kuwa nitakuwa huo.....akanisihi sana nifikie kwake....nikaona haina shida......aisee nilijuta ule uamuzi........

Nilikuwa najiweza hata kukaa hotel lakini nikasema nisimkwaze ndugu yangu.....

Nafika pale mapema kidogo tunapiga Stori za hapa na pale muda wa kulala napelekwa chumba cha watoto na humo kuna watoto kama wanne na wawili natakiwa kulala nao......

Vyakula sasa ndio adhabu......nilikuwa kila asubuhi nikienda kwenye mambo yangu namuachia jamaa kiasi cha pesa ili aongezee kwenye bajeti yao ili tufurahie maisha..... lakini matokeo yake mkewe anatulisha vitu vya ajabu......

Kila siku ugomvi na mkewe mimi ndio muamuzi....muda mwingine ugomvi ukizidi hakupikwi......

Nilikaa pale kama wiki hivi niliona kama nimekaa mwezi........

Kwa sifikirii tena kufikia kwa mtu nikisafiri.......
Watanzania kwanini hatupendi kuficha aibu zetu au ni kutojali na kukosa busara.

Mtu unajua una matatizo nyumbani unakaribisha wageni wa nini?

Tangu enzi za Musa na Ibrahimu Mgeni anakarimiwa sio tu kwa chakula kizuri bali mazingira, maneno na maelewano ya amani.

Sasa unajua kabisa wewe na Mke wako ni Chui na paka. Nafasi ya kulala huna unamkaribisha mtu wa nini?

Mbona mimi nilikaa miaka kibao sijawahi karibisha hata ndugu( sitaki maneno maneno mara ooh anajifanya mjanja) na nikaishi kwa uhuru na raha hadi nilipojipata.

Mke pia anatakiwa kulinda heshima ya Nyumba( familia) hata kama kuna maugomvi una nyuti mbele za wageni.
 
Mimi Huwa sipendi kushikuru yaani umetoka kuoga Asante,umekula Asante,umetoka chooni Asante, sipendi
Wewe una shukuru Moyoni? Hata Mungy huwezi kumshukuru Moyoni akakubali sembuse binadamu.

Mungu lazima ukiri kwa kinywa chako hakuna kushukuru moyoni wewe huna roho ya shukrani yaani Huridhiki😂😂
 
Watanzania kwanini hatupendi kuficha aibu zetu au ni kutojali na kukosa busara.

Mtu unajua una matatizo nyumbani unakaribisha wageni wa nini?

Tangu enzi za Musa na Ibrahimu Mgeni anakarimiwa sio tu kwa chakula kizuri bali mazingira, maneno na maelewano ya amani.

Sasa unajua kabisa wewe na Mke wako ni Chui na paka. Nafasi ya kulala huna unamkaribisha mtu wa nini?

Mbona mimi nilikaa miaka kibao sijawahi karibisha hata ndugu( sitaki maneno maneno mara ooh anajifanya mjanja) na nikaishi kwa uhuru na raha hadi nilipojipata.

Mke pia anatakiwa kulinda heshima ya Nyumba( familia) hata kama kuna maugomvi una nyuti mbele za wageni.
Dah!
Yaani ndugu we Acha tu...... ilikuwa mpaka muda mwingine nachelewa kurudi ili niepuke ile aibu......
 
We kama mimi tu.hua nakua unconfortable na mazingira mapya sana.halafu napenda ya uhuru binafsi
 
Back
Top Bottom