Nikisafiri kwenda sehemu sipendi kufikia kwa Mtu

CHIBA One

JF-Expert Member
Nov 16, 2018
560
2,087
Hili jambo kwa kweli labda naweza nikaonekana nna roho mbaya au Ant-Social, ila kiuhalisia katika utu uzima wangu huu, kama ikitokea safari fulani nahitaji kwenda sehemu kwa siku mbili tatu...sipendi kufikia kwa rafiki au ndugu, lakini naweza kuwapa taarifa kwamba ntafika Mkoani kwao na tunaweza kuonana sehemu Nyingine, ama nikaensa tu chap kuwasalimia na kuondoka bila kulala, kwangu mimi huwa naona kufikia kwa mtu kuna.

Mambo yafuatayo:
1. Unafikia kwa mtu lets say ni dar, wewe unashuka stand Mbezi lakini Yeye anaishi mbagala, huoni kama huu ni usumbufu na hakuna unachosave? Imagine umeingia dar saa 6 usiku uanze tena kukimbizana kwenda mbagala, ambapo ukifika tena unaambiwa umpe simu boda, halafu kesho yake issue zako unafanyia posta au k.koo.

2. Sio kila mazingira anayoishi mtu yatakufavor na wewe, unakuta unafikia kwa mtu inabidi sasa wagawe sebule iwe chumba kushoto na kulia ni chumbani kwao ni USUMBUFU.

3. ratiba ya kulala, kula na mambo yako inakuwa chini ya maamuzi ya mwenyeji wako, plus utakula nini na utakunywa nini?

4. Uaamka asubuhi unaulizia pasi unyooshe shati lako, mwenyeji hana pasi, au unakuta kuna bonge la joto na yeye hana hata feni.

5. Kuna hali fulani inakuwa inakufanya usijiamini, mfano inakulazimu unaporudi pale ulipofikia uwaze kupitia japo ka zawadi au kitu chochote kuwapelekea na unakuwa huna maamuzi na ratiba zako.

Kimsingi nadhani inapendeza kama unasafiri utafute tu altenative utafte hotel ama lodge kama Hali yako ni mbaya Kifedha.. hayo niliyoyataja hapo juu niliwahi kuyapitia ndio maana sitamani tena kufikia kwa mtu labda niwe nimekwama sana 100%

Toa maoni yako kuhusu hili, na ilikuwaje uliposafiri na kufikia/kukaa kwa rafiki au Ndugu?
 
Mimi sijawahi fikia kwa ndugu, wala kwangu hafiki mtu wa jinsia ya kiume, na wakilazimisha fikia kwangu nawalipia guest siku ya kwanza nyingine watajua wenyewe.

Si sawa kufikia kwa mtu kienyeji, labda kijana mwenzako, ambaye ajaoa na wewe ujaoa, hakuna jipya au la ajabu ulilosema, ni kwamba unaona umefanya jambo la ajabu, la hasha, hiyo ndo kawaida.
 
Halafu ukifika eti unataka uhuru.
1710587330179.jpg
 
Hili jambo kwa kweli labda naweza nikaonekana nna roho mbaya au Ant-Social, ila kiuhalisia katika utu uzima wangu huu, kama ikitokea safari fulani nahitaji kwenda sehemu kwa siku mbili tatu...sipendi kufikia kwa rafiki au ndugu, lakini naweza kuwapa taarifa kwamba ntafika Mkoani kwao na tunaweza kuonana sehemu Nyingine, ama nikaensa tu chap kuwasalimia na kuondoka bila kulala, kwangu mimi huwa naona kufikia kwa mtu kuna Mambo yafuatayo:
1. Unafikia kwa mtu lets say ni dar, wewe unashuka stand Mbezi lakini Yeye anaishi mbagala, huoni kama huu ni usumbufu na hakuna unachosave? Imagine umeingia dar saa 6 usiku uanze tena kukimbizana kwenda mbagala, ambapo ukifika tena unaambiwa umpe simu boda, halafu kesho yake issue zako unafanyia posta au k.koo
2. Sio kila mazingira anayoishi mtu yatakufavor na wewe, unakuta unafikia kwa mtu inabidi sasa wagawe sebule iwe chumba kushoto na kulia ni chumbani kwao ni USUMBUFU.
3. ratiba ya kulala, kula na mambo yako inakuwa chini ya maamuzi ya mwenyeji wako, plus utakula nini na utakunywa nini
4. Uaamka asubuhi unaulizia pasi unyooshe shati lako, mwenyeji hana pasi, au unakuta kuna bonge la joto na yeye hana hata feni.
5. Kuna hali fulani inakuwa inakufanya usijiamini, mfano inakulazimu unaporudi pale ulipofikia uwaze kupitia japo ka zawadi au kitu chochote kuwapelekea na unakuwa huna maamuzi na ratiba zako.
Kimsingi nadhani inapendeza kama unasafiri utafute tu altenative utafte hotel ama lodge kama Hali yako ni mbaya Kifedha.. hayo niliyoyataja hapo juu niliwahi kuyapitia ndio maana sitamani tena kufikia kwa mtu labda niwe nimekwama sana 100%

Toa maoni yako kuhusu hili, na ilikuwaje uliposafiri na kufikia/kukaa kwa rafiki au Ndugu?
Kama unazo fikia Gesti ila sisi wengi wakati bado tunajitafuta Ndugu na marafiki walitusaidia sana.

Tunawashukuru.
 
Back
Top Bottom