Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 28,051
- 52,594
kuna jambo linanitesa sana jamani .
mwaka jana mwanzoni nilienda ofisi moja ya umma kikazi.nilikuwa nimevaa suruali ya kitambaa ya kawaida tu ya ofsini. nilipofika getini pale nikazuiwa eti hawaruhusu mavazi hayo . nikashangaa maana sikuwa nimevaa jeans wala kipedo .ni suruali ya kitambaa ya kawaida tu ofsini wala haikuwa imenibana kiivo basi tu labda vile mimi mnene maana niliona wanawake wengine wamevaa wanaingia tu fresh.
wakati wale walinzi pale wananigomea kuna mama akaja akanipa mtandio wa dera umechooka mchafu mchafu ila sikuwa na jinsi maana niliiitaji kitu muhimu sana. nilivoingia ndani nikamkuta mdada mwingine akanipa kitenge kizuri na ule mtandio mchafu nikauweka kwenye pochi maana yule mama aliniambia nirudishe.
nilikaa huko ndani kwa muda .nilipotoka sikumkuta yule mama pale ,nikamtafuta sana sikumuona.nikawaomba wale walinzi niwaachie wakagoma. ikabidi niondoke nao
toka jan mwaka jana ninao . naogopa kuutupa .haufai kabisa umepauka ,nilishaufua ni msafi ila sijui niufanyeje . nikitaka kuutupa naogopa roho inauma najiona kama sina shukrani .