Nikiitupa hii nguo nitapata dhambi?

Nikiitupa hii nguo nitapata dhambi?

Walinzi walikuonea wivu tu,mbona suruali za kitambaa maofisini zinavaliwa tu

Mtandio utunze tu,kuutupa ni kama kutothamini hivi nguo ya mtu
 
kuna jambo linanitesa sana jamani .
mwaka jana mwanzoni nilienda ofisi moja ya umma kikazi.nilikuwa nimevaa suruali ya kitambaa ya kawaida tu ya ofsini. nilipofika getini pale nikazuiwa eti hawaruhusu mavazi hayo . nikashangaa maana sikuwa nimevaa jeans wala kipedo .ni suruali ya kitambaa ya kawaida tu ofsini wala haikuwa imenibana kiivo basi tu labda vile mimi mnene maana niliona wanawake wengine wamevaa wanaingia tu fresh.
wakati wale walinzi pale wananigomea kuna mama akaja akanipa mtandio wa dera umechooka mchafu mchafu ila sikuwa na jinsi maana niliiitaji kitu muhimu sana. nilivoingia ndani nikamkuta mdada mwingine akanipa kitenge kizuri na ule mtandio mchafu nikauweka kwenye pochi maana yule mama aliniambia nirudishe.
nilikaa huko ndani kwa muda .nilipotoka sikumkuta yule mama pale ,nikamtafuta sana sikumuona.nikawaomba wale walinzi niwaachie wakagoma. ikabidi niondoke nao
toka jan mwaka jana ninao . naogopa kuutupa .haufai kabisa umepauka ,nilishaufua ni msafi ila sijui niufanyeje . nikitaka kuutupa naogopa roho inauma najiona kama sina shukrani .
Yaani sasa hivi nikikutana na wewe nakusalimia nimeshaunganisha vipande vya image yako vimekamilika. Facial expression nimeipata kwenye comments zako.
 
usiutupe....endelea kuhifadhi tuu as long as haukudhuru.......no one knows tomorrow
 
mi naona bora uitupe tu mkuu maana kwanza inaonyesha jinsi gani inakukera kwa kupauka kwake,huwenda mwenzio ndio alikuwa anawafunikia watoto wake usiku wakilala,aliamua akupe kukusitiri
 
Sijapenda unavyo ikashifu nguo iliyokusaidia! Kwani wenye nguo mpya safi hawakupita hapo getini? Kama unaweza isema vibaya bila kuona huna shukrani unaogopeje kuitupa?
nimeeleza uhalisia mkuu ili unielewe sina dharau na hii nguo
 
Ulipewa it's okay, ulipewa kwa sababu ulikuwa na shida basi na wewe uwafanyie wengine vile vile kama ulivyotendewa(WEMA) wewe, sometimes kunamatukio huja na huwa ni funzo maishani!!!
 
Ulipewa it's okay, ulipewa kwa sababu ulikuwa na shida basi na wewe uwafanyie wengine vile vile kama ulivyotendewa(WEMA) wewe, sometimes kunamatukio huja na huwa ni funzo maishani!!!
sawa nkuu ,asante kwa ushauri
 
Yaani sasa hivi nikikutana na wewe nakusalimia nimeshaunganisha vipande vya image yako vimekamilika. Facial expression nimeipata kwenye comments zako.
mimi sio mnene wala
 
mimi sio mnene wala
Ndio maana uliweza kufunika mkia vizuri. Usiwe na wasiwasi Mimi nikimprofile mtu sikosei. Nitakusalimia Kwa heshima tu, to make exception itakuwa Kwa mkono wa kushoto ili unitambue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom