Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 77,155
- 111,066
Yaani nataka kufunga dish langu kwa mfano la azam au statimes au zuku ila naweka ile l.n.d bila lile li sahani lake je nikiunganisha hivyo nikaenda kuwasha tv yangu itaonyesha picha?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inaitwa LNB na sio LND...
Dish na ungo ni kitu kimoja...kazi yake ni kukusanya mawimbi yanayotoka kwenye satelaiti za anga za mbali, na kuyaelekeza ilipo LNB...
LNB inayakusanya hayo mawimbi toka pande tofauti tofauti za ungo baada ya kuwa reflected (akisiwa) na kuyashusha kwenye kisimbusi/king'amuzi/decoder
Huwezi kufunga LNB pekee ukapata mawimbi lazima kuwe na dish/ungo...