Niijuavyo Freemasonry

Niijuavyo Freemasonry

Eiyer,

Uko vizuri Mkuu, asante sana kwa Elimu hii. Nimrod wanasema alisimika misingi ya kimason duniani. Ndie aliigawanya siku ktk masaa 24, mwezi ktj siku 28, 29, 30 na 31. Japo huwa najiuliza kabla walihesabu vipi siku?

Katika kitabu cha mwanzo, hii ni kabla ya yooote kutokea, muandishi anahesabu siku saba, hapa ni kwa kutumia masaa yapu? Haya alobadilisha Nimrod? Ama yapi? Kama unajibu naomba unisaidie tafadhali...
 
Uko vizuri Mkuu, asante sana kwa Elimu hii. Nimrod wanasema alisimika misingi ya kimason duniani. Ndie aliigawanya siku ktk masaa 24, mwezi ktj siku 28, 29, 30 na 31. Japo huwa najiuliza kabla walihesabu vipi siku? Katika kitabu cha mwanzo, hii ni kabla ya yooote kutokea, muandishi anahesabu siku saba, hapa ni kwa kutumia masaa yapu? Haya alobadilisha Nimrod? Ama yapi? Kama unajibu naomba unisaidie tafadhali...

Masaa 24 ya siku, ni commandment ya Mungu, sio Nimrodi.

Siku za Kalenda hii tunayotumia kama leo tarehe 15 July 2014 ni kazi ya Roma na Kanisa.
 
Hivi unategemea nipate opportunity ya kumdeclare Mungu wa Kweli alafu niache sababu ntakuwa natoka nje ya Mada, wakati najua kabisa hata hii mada inapata nguvu kwa binaadamu kwa sababu ya kutomuabudu Mungu wa Kweli?

Lakini kumbuka sio tu kwakuwa unahubiri injili ya kweli basi unaweza kwenda kuhubiri baa kwa walevi

Mungu amekupa ubingo wakufikiri mahali palipo salama pa kupeleka neno lake lakini pia ubongo huo amekupa ili uone ni wakati gani ni sahihi kufanya jambo au laa

Hili ambalo unataka kulileta hapa halistahili hapa hata kama unadhani ni la ukweli,labda uneomba ruhusa kutoka kwa mwenye mada!
 
Uko vizuri Mkuu, asante sana kwa Elimu hii. Nimrod wanasema alisimika misingi ya kimason duniani. Ndie aliigawanya siku ktk masaa 24, mwezi ktj siku 28, 29, 30 na 31. Japo huwa najiuliza kabla walihesabu vipi siku? Katika kitabu cha mwanzo, hii ni kabla ya yooote kutokea, muandishi anahesabu siku saba, hapa ni kwa kutumia masaa yapu? Haya alobadilisha Nimrod? Ama yapi? Kama unajibu naomba unisaidie tafadhali...

Siku kuwa na masaa 24 sio Nimrod bali ni Mungu kwakuwa mzunguko unaosababisha masaa 24 ni matokeo ya uumbaji na sio kitu kingine

Kuhusiana na tarehe au idadi ya siku katika mwezi pia sio Nimrod bali kuna historia ambayo inaelezea idadi ya siku kwenye mwaka,kalenda tunayotumia ni kalenda ya mfalme Gregory na ndio maana inaitwa Gregorian calender,huyu alikuwa ni mfalme wa Rumi ya kale,kuna historia ndefu sana kumhusu

Mungu alikuwa anahesabu siku ya kwanza,yapili,ya tatu na kuendelea na hakuweka majina ya siku,mwaka kwenye kalenda ya mwanza ulikuwa na siku 360 na sio 365/6 kama ilivyo sasa!
 
Lakini kumbuka sio tu kwakuwa unahubiri injili ya kweli basi unaweza kwenda kuhubiri baa kwa walevi

Mungu amekupa ubingo wakufikiri mahali palipo salama pa kupeleka neno lake lakini pia ubongo huo amekupa ili uone ni wakati gani ni sahihi kufanya jambo au laa

Hili ambalo unataka kulileta hapa halistahili hapa hata kama unadhani ni la ukweli,labda uneomba ruhusa kutoka kwa mwenye mada!

Nimekuelewa.
 
According to us Catholics......hawa wajenzi huru tunawachukulia kama maadui wa Injili.....huu ni mtizamo wa Kanisa Katoliki juu ya hawa wajenzi huru.....chanzo cha habari hii ikiwa Catholic Answers....

Freemasonry is incompatible with the Catholic faith. Freemasonry teaches a naturalistic religion that espouses indifferentism, the position that a person can be equally pleasing to God while remaining in any religion.

Masonry is a parallel religion to Christianity. The New Catholic Encyclopedia states, "Freemasonry displays all the elements of religion, and as such it becomes a rival to the religion of the Gospel. It includes temples and altars, prayers, a moral code, worship, vestments, feast days, the promise of reward or punishment in the afterlife, a hierarchy, and initiation and burial rites."

Masonry is also a secret society. Its initiates subscribe to secret blood oaths that are contrary to Christian morals. The prospective Mason swears that if he ever reveals the secrets of Masonry - secrets which are trivial and already well-known - he wills to be subject to self-mutilation or to gruesome execution. (Most Masons, admittedly, never would dream of carrying out these punishments on themselves or on an errant member).

Historically, one of Masonry's primary objectives has been the destruction of the Catholic Church; this is especially true of Freemasonry as it has existed in certain European countries. In the United States, Freemasonry is often little more than a social club, but it still espouses a naturalistic religion that contradicts orthodox Christianity. (Those interested in joining a men's club should consider the Knights of Columbus instead.)

The Church has imposed the penalty of excommunication on Catholics who become Freemasons. The penalty of excommunication for joining the Masonic Lodge was explicit in the 1917 code of canon law (canon 2335), and it is implicit in the 1983 code (canon 1374).

Because the revised code of canon law is not explicit on this point, some drew the mistaken conclusion that the Church's prohibition of Freemasonry had been dropped. As a result of this confusion, shortly before the 1983 code was promulgated, the Sacred Congregation for the Doctrine of the Faith issued a statement indicating that the penalty was still in force. This statement was dated November 26, 1983 and may be found in Origins 13/27 (Nov. 15, 1983), 450.


 
Eiyer,

Mkuu,

Asante, kuna hadithi kuwa hapo mwanzo siku ilikuwa na masaa 12. Hivyo mchana na Usiku zilikuwa ni siku mbili tafauti' Mpaka Nimrod alipobadilisha.

Ni kitabu gani ama source gani inaelezea habar za Nimrod kwa ufasaha zaidi?

Semiramis kwann wanasema alikuwa Mama yake Nimrod? Wakat nikisoma naona walikutana kwenye danguro la Semiramis?
 
Mkuu,

Asante, kuna hadithi kuwa hapo mwanzo siku ilikuwa na masaa 12. Hivyo mchana na Usiku zilikuwa ni siku mbili tafauti' Mpaka Nimrod alipobadilisha.
Suala la siku kuwa ni masaa mangapi au ni baada ya muda gani hilo ni suala la Mungu zaidi kwakuwa kwenye Mwanzo Mungu alisema "ikawa jioni ikawa aubuhi siku ya kwanza",kuanzia hapo tunaweza kuona kuwa siku moja ni pamoja na usiku na mchana na sio kinyume chake

Na kwakuwa ni hivyo basi siku ni masaa 24 na sio chini au zaidi ya hapo,Nimrod hakufanya hili bali lilianzia kwa Mungu mwenyewe
Ni kitabu gani ama source gani inaelezea habar za Nimrod kwa ufasaha zaidi?
Hakuna kitabu kimoja ambacho ni authentic kinachomzungumzia huyu jamaa,ili uweze kujua angalau kwa uwezo wako kuhusiana na Nimrod ni kutafiti kutoka zaidi ya chanzo kimoja na utaweza kufikia tamati kutokana na uwezo wako wa kutafakari mambo kuwa Nimrod alifanya hiki au kile

Nimrod hajaelezwa sana kwenye biblia kuwa lifanya nini bali kwakuwa yeye ndie founder wa Babel na babel inajulikana kwa imani yake basi kuanzia hapo anajulikana kuwa ni mwanzilishi wa imani hiyo ya kipagani

Kwenye biblia anaelezwa Tamuz ambae alikuja kujulikana ni mtoto wa Nimrod

Semiramis ametajwa kwenye Biblia kama Diana
Semiramis kwann wanasema alikuwa Mama yake Nimrod? Wakat nikisoma naona walikutana kwenye danguro la Semiramis?
Habari za Semiramis ziko tofauti kulingana na chanzo unachokisoma,kwa mujibu wa vyanzo nilivyovisoma mimi vinaniambia kuwa huyu alikuwa ni mama yake na baadae alikuja kuwa mkewe,hilo sina uhakika nalo kama vile ambavyo sina uhakika na mengine ambayo yanamhusu huyu mwanamke

Kufuatilia sana kutakuja kukufikisha mahali utaujua ukweli,endelea tu usichoke!
 
Kutokana na vyanzo mbali mbali vya habari inasemekana kuwa Semiramis alikuwa mama yake Nimrod na baadae walikuja kuishi kama mke na mume

Nimrod alikuwa ni mfalme wa Babeli na ufalme wake ulikuwa na utamnaduni tofauti na falme zingine,yeye ndie aliyeamua kujenga mnara mrefu sana ambao ulikuwa na malengo mawili

1;Kuzuia watu wa ufalme wake kufa na mafuriko au gharika kama itakuja kutokea tena
2;Kwenda kumfuata Mungu na kumhoji sababu ya kuleta gharika na kuuwa watu

Nimrodi alianzisha imani ya kuabudu sayari na nyota,umani hiyo ilikuwa sana wakati huo na ikafikia hadi kuwa kama imani ya ulimwengu kwa wakati huo

Babu yake Nimrod ambae ni mtoto wa Nuhu aliyeitwa Shem alikuja kumkamata na kumuua Nimrod na kuukatakata mwili wake vipande vipande na kuvisambaza maeneo yote ambayo kulikuwa na imani aliyoianzisha Nimrod na Shem aliagiza kuwa kama kutakuwa na mtu mwingine aliyekuwa anaifuata imani hiyo nae atafanywa kama Nimrod

Muda ulipita na Shem alikuja kufariki Dunia,baada ya kufariki Dunia mke wa Nimrod au mama yake kwa upande mwingine alikusanya mabaki ya mwili wa mumewe au mwanae ili akayazike upya,alifanikiwa kupata mwili wake wote lakini alishindwa kupata mabaki ya kiungo cha uzazi cha mumewe au mwanae

Baada ya kukikosa aliwaambia wafuasi wa imani hiyo kuwa Nimrod alkuwa amekwenda kwenye jua na ndiko alikokuwa anaishi na amekwenda na kiungo chake cha uzazi na alikuwa ametoa maagizo kuwa kuanzia wakati huo hicho kiungo kitakuwa ni alama ya imani yao,haikufahamika hasa mawazo hayo aliyatoa wapi lakini ndivyo alivyowaambia wafuasi wa Nimrod na kuanzia wakati huo kiungo hicho kikawa ni alama kubwa sana ya imani hiyo

Baadae walikuja kui design alama hiyo na kuwa na muonekano tofauti ili unsiweze kuonekana kiurahisi na kugunduliwa na watu

Leo kiungo au alama hiyo inaitwa Obelisk,unaweza kuona picha yake hapa chini

WashingtonDC_Obelisk.jpg


Hiyo ni obelisk iliyoko Washington

Baadae mabaki ya mwili wa Nimrod ulizikwa kwa taratibu zote za kiimani na baada ya muda kupita uliota mti kwenye kaburi la Nimrod na mama yake au mkewe alisema kuwa hiyo ilikuwa ni ishara ya Nimrod kuzaliwa upya na mama yake au mkewe aliagiza kuanzia siku hiyo mti huo utakuwa ni alama ya kuzaliwa upya Nimrod

Lakini pia mkewe aliagiza kuwa Nimrod amekuwa mungu na kuanzia wakati huo alitakiwa aabudiwe na ndivyo ilivyokuwa na alipewa jina na Baal,hivyo mti huo ambao umekuja kujulikana kama "christmass tree" leo hii ndio inasemekana uliota kwenye kaburi la Nimrod na ni ishara ya kuzaliwa upya

Decorating-Christmas-Trees-1.jpg


Mti wa Christmass

Semiramis alipotoa hayo maagizo alipotea kwa muda na kurudi akiwa mjamzito,alipoulizwa alikokuwa alisema kuwa alikuwa amemfuata mwanae au mumewe na ujauzito aliokuwa nao alikuwa amepewa na mumewe na alikuwa anakuja kumzaa mtoto ambae atakuwa mwokozi wa kizazi kile kutoka kwa watu waliokuwa wanawanyanyasa lakini zaidi atakuja kuwaokoa na wanyama wakali waliokuwa wanatishia uhai wa jamii ile ya Babeli

Kweli baada ya muda Semiramis alijifungua mtoto aliyepewa jina Tamuz na alipokua alikuja kuwa na tabia kama ya "baba" yake kwa kuwa muwindaji bora

Mtoto huyu alikuja kupata ajali mbaya iliyokuja kuyaondoa maisha yake pale alipokuja kujeruhiwa vibaya na nguruwe pori na kusababishiwa majeraha ambayo hakupona na alikuja kufariki,ile siku ambayo aliuwawa na nguruwe pori iliamriwa kutokuliwa nyama na ilisemwa kuwa nyama ya nguruwe pori na nguruwe yoyote yule kuwa haifai baada ya mnyama huyo kumuua aliyetarajiwa kuja kuwa kiongozi wa watu wa Babeli

Muda ulipita na Semiramis alikuja kuwaambia kuwa mwanae hakuwa amekufa bali alikuwa amemfuata baba yake huko alikokuwa na akawaambia wafuasi wake kuwa tangu siku hiyo atahesabika kuwa ni mtoto wa mungu wao na atakuwa akiabudiwa,aliagiza ia kuwa alama itakayokuwa inamuwakilisha mungu wao ambao ni Nimrod itakuwa ni jua

Baadae aliwaagiza kuwa alikuwa ameagizwa kumfuata mumewe siku sio nyingi na aliagiza kuwa atakapomfuata alama yake itakuwa ni mwezi,ulipita muda na alikuja kufariki na kuanzia hapo alikuwa akiabudiwa

Na hapo dipo ilipopatikana imani ya kopagani yenye utatu wa Nimrod,Semiramis na Tamuz,utatu huu ulikuwa una majina tofauti tofauti kila imani hiyo ilipokuwa inakwenda na kuota mizizi,mfano Misri walikuwa wanafahamika kama Isis,Horus na Osiris

Hiyo ndio historia fupi ya Nimrod na imani yake pamoja na Babeli

Historia hiyo ndio inaaminika kuwa ya kweli japokuwa kumekuwepo na historia zingine tfauti na hiyo,ili uweze kupata ukweli ni bora ukatafiti mwenyewe ili uujue ukweli

CC: juve2002 Mkuu wa chuo Ntuzu Sangarara charminglady Kaunga Ablessed Kongosho King'ast Mtambuzi Ishmael MTAZAMO RGforever .......

Mkuu, Asante sana,

Japo napata shida, sina hakika hadithi hii ni tafauti na niijuayo mm, ama ni sawa.

Nimrod alikuwa ni mpiganaji, aliekuwa na ambition za kuipanua empire yake, yy alikuwa ni mu ethiopia, katika harakat zake za kivita, ndipo alikutana na semiramis, mwanamke huyu alikuwa ni mwenyeji wa Urech, ambayo sasa inaitwa Uru wa kaldayo, Mwanamke huyu alikuwa ni malaya aliekuwa anamiliki danguro, na alikuwa anafanya kazi ya kuwapoza wanaume walokuja kujipumzisha hapo ktk huo mji.

Hapa ndipo semiramis alikutana na Nimrod, na moja ya masharti aliompa Nimrod ni kuwa ilikuwa ni lazima amuoe' na kwa kipindi kile ilikuwa haikubaliki kutawaliwa na Malaya.

Hapo ndipo uongo ukatungwa, kuwa semiramis alikuwa ni bikra, alietokea baharini, kuja kukutana na Nimrod ambaye ni Mungu jua. Hapo ndipo ikaibuka imani ya Unajimu na utabiri wa Nyota.

Imani hii ilijikita katika madai kuwa Shetani ndie mtawala wa haki, na muumba wa dunia, na Mungu alikuwa amemchakachua nafasi yake. Na ikatabiriwa kuwa atazaliwa mtoto ambae atakuja kuurudisha Utawala wa shetani kwa kumnyang'anya Mungu madaraka yote.

Hadithi hii ni ndefu kila napojaribu kuisamarise naacha mambo Muhimu.

Lakini nakumbuka, semiramis alikuja kuuliwa na mwanae kwa Upanga, tena ukatungwa uongo kwamba amepaa kwenda kwa Mume wake kumsaidia kutawala.

Habari hata google kuipata ni shida, kuna mambo mengi hapa yananichanganya, anaeifahamu hadithi hii vyema atukumbushe.

Nimrod ndie anaesemekana alisimika rasmi imani ya ki freemason duniani.

Mkuu hapo kwa RED unamaanisha Utatu Mtakatifu wa Yesu, Maria na Mungu Baba? Hebu finyanga upya hoja hapo ili urudi kwenye tunachoamini yaani Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.......

Kuna vitu ni kweli Kanisa lilikubali kuvifanya ambavyo sioni tatizo lake ambavyo vilikuwa vya kipagani lakini Kanisa likavigeuza ili kwa mfano ile siku ya jua iliyokuwa sikukuu kubwa sana kwa wapagani baada ya wao kuong'oka huwezi kuifuta tu siku iliyosheherekewa karne nyingi zaidi ya Kanisa kuifanya siku hiyo iwe siku ya kuzaliwa Yesu badala ya siku ya jua............

Siku hizi tunaita utamadunisho yaani kutumia utamaduni ule ule waliozoea watu wa jamii fulani kabla ya kumjiua Yesu na kuvifanya vitu vile vile (vinavyokubalika na Kanisa) katika ibada za Kanisa kwa mfano kupokea sadaka za mifugo au mazao badala ya fedha tu kama ilivyozoeleka..............

Haya mambo tumeishayaongea sana hapa.
Nadhani kuna tatizo kubwa la kuchukulia kila issue independently, ni ngumu sana kuzungumzia kila kitu upya kila wakati kinapo resurface.

Ukiristo uliopelekwa Roma ulikuwa unazunguzia Mungu in duality, Converts wakawa wengi kiasi cha kutishia Ufalme kupinduka sababu ya kukosa fedha, ndio haraka sana habari za Maria na Yesu zikawa Spinned, BOOM, mungu akatengenezwa haraka haraka akawa ni yule yule wao ufalme ukaendelea.

Ntakuwapo jioni kwa mjadala zaidi, wakati huo niletee fungu linaloelezea utatu mtakatifu kabla ya kufa kwa Yesu na Kabla Injiri haijaubiliwa Roma.
Eiyer angalia na haya maelezo
Nimrodi aliunda mfumo wa Ibada ya Udanganyifu na akawa mfalme wa kwanza Muasi. Nimrodi alioa msichana aliyeitwa Semerimus ambaye alimzaa mtoto wa kiume aliyeitwa Tamuzi. Nimrodi akamfanya mkewe kuwa kuhani mkuu. Huyo mama na mtoto wakawa ndiyo miungu ya kuabudiwa huko Babiloni. Kilichongwa kitu kama sanamu ya mwanamke aliyebeba mtoto ikawa alama ya Mungu wao. Mwanamke huyu akapewa jina Malkia wa Mbinguni.

Mtindo huu wa kumwabudu mwanamke na mtoto wake ulienea hadi Israel. Wakati wa nabii Yeremia, Waisrael walikuwa wamezama katika dimbwi la kuabudu kwa namna hii. Yeremia alipowaeleza jinsi BWANA alivyokusudia kuwaadhibu kwa sababu ya kufuata miungu mingine, Waisrael hawa walikataa.

Yeremia 44:15-17
15. Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema,

16. Neno lile ulilotuambia kwa jina la Bwana, sisi hatutakusikiliza.

17. Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.

Katika kitabu cha Ezekiel, twasoma kuwa ibada hii ya malkia wa mbinguni iliingia mpaka katika hekalu ya Yerusalem. Mungu alimuonyesha Ezekiel machukizo hayo hekaluni ambako aliwaona wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi mtoto wa Nimrodi

Ezekiel 8:14 Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.

Imani hii ya mwanamke na mtoto wake iliendelea mpaka wakati wa dola ya Rumi. Wakati makaisari wa Rumi wakitawazwa, walipewa jina PONTIFEX MAXIMUS yaani Kuhani Mkuu. Kaisari akiwa mfalme wa Rumi na Kuhani mkuu alitawala mfumo wa ibada ya mama na mtoto wake, ambayo watu walilazimika kuheshimu na kushiriki maandazi ya moto, mayai ya pasaka na mti ulioletwa wakati wa baridi tarehe aliyozaliwa Tamuzi mtoto wa Nimrodi na makafara mengine mengi.

Constantine alipotawala Rumi katika mwaka 312 AD alitangaza kuwa Dini ya Kikristo ni dini ya dola ya Rumiyote na watu wote katika dola hiyo ni wakristo

Harakati hizi za Constantine kujenga kanisa la Kikristo la Rumi ziliunganisha Ukristo na Ibada ya Wababiloni. Baadaye watu hawa wa Rumi wakaona heri wamwabudu Mariamu mama wa Mwokozi wetu Yesu Kristo kuliko kumwabudu Malkia wa Mbinguni wa Babiloni na mtoto wake Tamuzi.
 
Last edited by a moderator:
Eiyer angalia na haya maelezo
Nimrodi aliunda mfumo wa Ibada ya Udanganyifu na akawa mfalme wa kwanza Muasi. Nimrodi alioa msichana aliyeitwa Semerimus ambaye alimzaa mtoto wa kiume aliyeitwa Tamuzi. Nimrodi akamfanya mkewe kuwa kuhani mkuu. Huyo mama na mtoto wakawa ndiyo miungu ya kuabudiwa huko Babiloni. Kilichongwa kitu kama sanamu ya mwanamke aliyebeba mtoto ikawa alama ya Mungu wao. Mwanamke huyu akapewa jina Malkia wa Mbinguni.

Mtindo huu wa kumwabudu mwanamke na mtoto wake ulienea hadi Israel. Wakati wa nabii Yeremia, Waisrael walikuwa wamezama katika dimbwi la kuabudu kwa namna hii. Yeremia alipowaeleza jinsi BWANA alivyokusudia kuwaadhibu kwa sababu ya kufuata miungu mingine, Waisrael hawa walikataa.

Yeremia 44:15-17
15. Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema,

16. Neno lile ulilotuambia kwa jina la Bwana, sisi hatutakusikiliza.

17. Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.

Katika kitabu cha Ezekiel, twasoma kuwa ibada hii ya malkia wa mbinguni iliingia mpaka katika hekalu ya Yerusalem. Mungu alimuonyesha Ezekiel machukizo hayo hekaluni ambako aliwaona wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi mtoto wa Nimrodi

Ezekiel 8:14 Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.

Imani hii ya mwanamke na mtoto wake iliendelea mpaka wakati wa dola ya Rumi. Wakati makaisari wa Rumi wakitawazwa, walipewa jina PONTIFEX MAXIMUS yaani Kuhani Mkuu. Kaisari akiwa mfalme wa Rumi na Kuhani mkuu alitawala mfumo wa ibada ya mama na mtoto wake, ambayo watu walilazimika kuheshimu na kushiriki maandazi ya moto, mayai ya pasaka na mti ulioletwa wakati wa baridi tarehe aliyozaliwa Tamuzi mtoto wa Nimrodi na makafara mengine mengi.

Constantine alipotawala Rumi katika mwaka 312 AD alitangaza kuwa Dini ya Kikristo ni dini ya dola ya Rumiyote na watu wote katika dola hiyo ni wakristo
Haya maelezo yana ukweli mwingi
Harakati hizi za Constantine kujenga kanisa la Kikristo la Rumi ziliunganisha Ukristo na Ibada ya Wababiloni. Baadaye watu hawa wa Rumi wakaona heri wamwabudu Mariamu mama wa Mwokozi wetu Yesu Kristo kuliko kumwabudu Malkia wa Mbinguni wa Babiloni na mtoto wake Tamuzi.

Hapa naweza kusema ibada ya mwanamke ni ileile kwakuwa hata alama ya mwanamke aliyebeba mtoto au sanamu hiyo ni ile ile na hata desturi za kuvaa kofia wa makuhani pamoja na taratibu za ibada zinafanana!
 
Mkuu wa chuo,

Mkuu,

Huu mti ndio mti chritsmass? Kuna namna inafanya niwaze huende tar 25 ndio tarehe alozaliwa TAMUZ, maana nashindwa elewa ilipatikana vipi hii tar? Ama ilipangwa na Roma?

Vipi boxing day?

Kuna mambo mengi ya kipagani yameingizwa ktk imani ya Ukristo.

Hebu nisaidie hayo machache kwanza tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Eiyer angalia na haya maelezo


Harakati hizi za Constantine kujenga kanisa la Kikristo la Rumi ziliunganisha Ukristo na Ibada ya Wababiloni. Baadaye watu hawa wa Rumi wakaona heri wamwabudu Mariamu mama wa Mwokozi wetu Yesu Kristo kulikokumwabudu Malkia wa Mbinguni wa Babiloni na mtoto wake Tamuzi.

Upo sahihi sana mkuu ingawa hapo kwa RED kwa wakristo wa sasa wakikusoma wanaweza kuendelea na conclusion ile ile wanayoimbiwa kila siku ya Wakatoliki kumuabudu Mariamu........

Lakini pia soma hii kitu uone pia ili uone pia wakati gani Kanisa lilipomtambulisha kama Malkia wa Mbingu in relation to Babiloni concept...............

The beginning of the concept that Mary is a Queen is found in the annunciation narrative. For the angel tells her that her Son will be King over the house of Jacob forever. So she, His Mother, would be a Queen.

The Fathers of the Church soon picked up these implications. A text probably coming from Origen (died c. 254: cf. Marian Studies 4, 1953, 87) gives her the title domina, the feminine form of Latin dominus, Lord. That same title also appears in many other early writers, e.g. , St. Ephrem, St. Jerome, St. Peter Chrysologus (cf. Marian Studies 4. 87-91). The word "Queen" appears abut the sixth century, and is common thereafter (Marian Studies, 4, 91-94).

The titles "king" and "queen" are often used loosely, for those beings that excel in some way. Thus we call the lion the king of beasts, the rose the queen of flowers. Surely Our Lady deserves the title richly for such reasons. But there is much more.

Some inadequate reasons have been suggested: She is the daughter of David. But not every child of a king becomes a king or queen. Others have pointed out that she was free from original sin. Then, since Adam and Eve had a dominion over all things (Genesis 1. 26) she should have similar dominion. But the problem is that the royalty of Adam and Eve was largely metaphorical.

The solidly theological reasons for her title of Queen are expressed splendidly by Pius XII, in his Radiomessage to Fatima, Bendito seja (AAS 38. 266): "He, the Son of God, reflects on His heavenly Mother the glory, the majesty and the dominion of His kingship, for, having been associated to the King of Martyrs in the unspeakable work of human Redemption as Mother and cooperator, she remains forever associated to Him, with a practically unlimited power, in the distribution of the graces which flow from the Redemption.

Jesus is King throughout all eternity by nature and by right of conquest: through Him, with Him, and subordinate to Him, Mary is Queen by grace, by divine relationship, by right of conquest, and by singular choice [of the Father]. And her kingdom is as vast as that of her Son and God, since nothing is excluded from her dominion."

We notice that there are two titles for the kingship of Christ: divine nature, and "right of conquest", i.e., the Redemption. She is Queen "through Him, with Him, and subordinate to Him." The qualifications are obvious, and need no explanation. Her Queenship is basically a sharing in the royalty of her Son. We do not think of two powers, one infinite, the other finite. No, she and her Son are inseparable, and operate as a unit.

Of the four titles Pius XII gave for her Queenship, we notice that two are closely parallel to those of Jesus:
(1) He is king by nature, as God; she is Queen by "divine relationship" that is, by being the Mother of God. In fact her relation to her Son is greater than that of ordinary Mothers of Kings. For she is the Mother of Him who is King by very nature, from all eternity, and the relationship is exclusive, for He had no human father. Still further, the ordinary queen-mother gives birth to a child who later will become king. The son of Mary is, as we said, eternally king, by His very nature.

(2) He is king by right of conquest. She too is Queen by right of conquest. We already saw that this title for Him means that He redeemed us from the captivity of satan. She shared in the struggle and victory. Since the Pope expressed her dependence on Him in a threefold way--something we would have known anyway--then it is clear that he did not have in mind any other restriction which he did not express. So, maintaining this subordination, "by right of conquest" means the same for her as it does for Him.

The other two titles

(3) She is Queen by grace. She is full of grace, the highest in the category of grace besides her Son.

(4) She is Queen by singular choice of the Father. A mere human can become King or Queen by choice of the people. How much greater a title is the choice of the Father Himself!

Pius XII added that "nothing is excluded from her dominion." As Mediatrix of all graces, who shared in earning all graces, she is, as Benedict XV said, "Suppliant omnipotence": she, united with her Son, can obtain by her intercession anything that the all-powerful God can do by His own inherent power.
In the Old Testament, under some Davidic kings, the gebirah, the "Great Lady", usually the Mother of the King, held great power as advocate with the king. Cf. 1 Kings 2:20, where Solomon said to his Mother Bathsheba, seated on a throne at his right: "Make your request, Mother, for I will not refuse you." Here is a sort of type of Our Lady.
 
Mkuu,

Huu mti ndio mti chritsmass?
Kutokana na maelezo ya Eiyer uki compare na hayo ya kwangu, inavyoonekana ndio wenyewe...
Kuna namna inafanya niwaze huende tar 25 ndio tarehe alozaliwa TAMUZ, maana nashindwa elewa ilipatikana vipi hii tar?
Hayo maelezo yako yanawezekana pia yakawa na ukweli maana vyanzo vingi vinasema hivyo...
Ama ilipangwa na Roma?
Yeah, ilikuja pia kutumika na Roma na mfalme Constantine mfalme wa kwanza wa Kirumi aliyekuwa Mkristo na inasemekana kusherekewa kwa mara ya kwanza ilikuwa Desemba 25, mwaka 336 AD, Ambapo baada ya miaka michache Papa Julius I akaiweka ndio wanasema officialy ikawa siku ya kusherekea kuzaliwa kwa Yesu

Vipi boxing day?
Boxing day ni siku inayofuatia baada ya Christmas, ni siku ya kufungua zawadi kama jina lisemavyo... Lakini ngojea tuje tuchimbe zaidi kuijua kwa undani

Kuna mambo mengi ya kipagani yameingizwa ktk imani ya Ukristo.
Hebu nisaidie hayo machache kwanza tafadhali.
Inawezekana kwa hilo pia kukawa na ukweli...
 
Mkuu wa chuo,


Kwa faida Zaidi ya wengi Waweza kwenda mbali Zaidi ktk maelezo yako ya hao Watu waliokua wakimwabudu TAMMUZ walikua wakiamini nini Zaidi Mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Kwa faida Zaidi ya wengi Waweza kwenda mbali Zaidi ktk maelezo yako ya hao Watu waliokua wakimwabudu TAMMUZ walikua wakiamini nini Zaidi Mkuu?
Hapo sijalipata swali lako vizuri mkuu, Ila hawa watu waliokuwa wakimuabudu Tammuz waliamini katika Miungu mitatu yaani Mungu Jua, Mungu Mwezi na Mungu Nyota ambapo Mungu jua ni Nimrod, Mungu mwezi ni Semerimus na Mungu Nyota ni Tammuz ilikuwa ni ibada ya kipagani ila ilifuata ile trend kama ya Utatu mtakatifu yaani kwa kifupi naweza kusema waliufananisha utatu mtakatifu na miungu yao

2 Wafalme 23:5 Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni.

Nimekuwekea huo mstari kuonyesha hayo mambo Waisrael walirithi kutoka Babeli
 
Nimekuwa nikijaribu kila wakati kufikiri na kufanya tafiti kwa kutumia akili binafsi bila machapisho wala vitabu rejeaa ma msaada hadithi za kusimuliwa,.moja ya mambo ambayo huwa nafikiria ni kuhusu jamii inayosemekana ni jamii ya siri(Free mason) kama wengi wanavoiita.,,

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo nimegundua ambayo pia yaweza kuwa tofauti na wengi wanavofikiri.


Nitaaanza kwanza kwa kuifafanua maana ya Free mason na misingi yake,(narudia tena please hii ni kwa mujibu wangu na nnaandika kutoka kichwan sio machapisho yoyote).

Free Mason ama wajenzi huru,ni jamiii ama kikundi ambacho kina misingi toka zaman sana enzi za mfalme solomon.kwa jinsi nnavojua mimi kilianzaa kama umoja wa wajenzi waliokuwa maarufu sana wakati ule hasa katika mambo.ya ramani na usanifu majengo,kikundi hiki kilikuwa namisingi yake mashariki yakati.wakati kinaanza hawakuwa na nia yoyote mbaya kama inavyosemekana sasa.


Walianza kama umoja wa wajenzi na baadae kutanuaka hadi ulaya,asia,america kusini na kaskazin na pia africa kaskazin na ethiopia.malengo yao makubwa yalikuwa kusaidia nak udumisha umoja wao na kuendeleza chama chao.

UHUSIANO WAO NA UTAJIRI
Baada ya kupata wafuasi(wajenzi),kikundi hiki kilitanuka na kushawishi watu waliokuwa nau wezo wa kifedha kuwekeza na kujiunga nao ili kuweza kuendelza imoja wao.matajiri mbali mbali kutoka mabara hasa ya ulaya na asia pia marekani waliwasapoti na kuinua mfuko wao wa umoja wa wajenzi.

Walikuwa wakichukua tenda za ujenzi katika sehem mbalimbali duniani na hivo kuanzisha kampuni nyingi karibu kila bara na kanda kadhaa. Na kwa sababu hiyo walijitengenezea jina na heshima na kwa kuwa walikuwa wengi matajir waliweza kushawishi mambo mengi katika siasa,sayansi,na dini.waliweza kufanya mageuzi katika serikal nyingi na kuweka watu waliowataka wao.waliweza pia kufadhili tafiti mbalimbali za lisayansi na kuwasapoti watu maarufu na kuwaaminisha watu kuwa wao(watu),kuwa ni bora na wanauwezo mkubwa kuliko........


KUHUSISHWA KWAO NA SHETANI

Baada ya jamii hii kukua na kuota mizizi ikiwa kama jamii wa wasomi,wataalam,wabunifu na watu maarufu,ilianza kujipanua na kujiingiza katika serikal kubwa duniani.na kushawishi mambo ambayo yalikuwa na manufaaa kwao na hasa katika kuendeleza umoja na mfuko ama ustawi wao.,
Kutokana na kukua kwake wajenzi hawa,wakafikia hatua ya kuanzisha imani yao binafsi,ambapo moja ya misingi yao ni kuamini katika nafsi(sisi),(we the people),rejea hotuba za rais obama za kuapishwa.kwah iyo wakaanzisha utaratibu wao wa kuabudu ambapo wamekuwa wakitoa kafara na sadaka mbali mbali kutokana na imani yao.wamekuwa na ishara zao z kutambuana n.k

Kutokana na wao kuamini katika uwezo wao,wamekuwa wakihisiwa kuwa wanapinga uwepo wa anayeitwa mungu badala yake kwamba wanamuunga shetani mkono.madai haya binafsi nayapinga kwa sababu kuu zifuatazo.

1.aina ya kuabudu wanayotumia Free masoni ni ile iliyotumiwa na mnaowaita mababa wa imani,ibrahim(Abraham ),mussa na akina solomon na wengine wengi.ref.pia kabla ya kuja wakoloni africa tulikuwa tunatoa kafara hadi ya binadam kwa mizim(was that masonic worship??)

2.hakuna kitabu cha masonic rules kinachoeleza wazi kwamba hakuna mungu,ila rules zoa zinaonesha misimamo na personal charachters za mwanadam ambazo hazina uhusiano na kisichoonekana.

3.masoni hawatoi kafara ya kuua wanadam bali ni mbuz,kondoo ama wanyama ambao ni adim kuwaona.

4.chuki,uoga na udhaifu wa dini ndo chanzo cha kusingizia yote.

WANAFANYAJE KAZI
Msonic hufanya shughuli zao kwa umakini na kanuni zao ni za siri pia.wanavitabu na mafunzo ya misingi imara katika dini yao.ili kuhakikisha wanajieneza kwa kiasi kikubwa ,wao hudeal na watu maarufu ama utafiki ama bidhaa pendwa ambapo husapoti na kuendesha shughuli mbalimbali kwa ufanisi mkubwa.

NINI LENGO LAO??
1. Free masonic,hawana lengo baya kama ambavo tumekuwa tukisimuliwa kila siku katika media.,lengo lao ni kutaka kujitawanya karibu kila pembe ya dunia na hivo kupata wafuasi ama waimini wa kutosha.,

2.pia kuitawala dunia(huu ni mpango endelevu ),na kwa imani na plan zao utatimia kabla ya mwaka 2040,lengo lao ni kuona watu wote wanakuwa kitu kimoja na kuunda umoja mahal pote katika uso wa dunia.

3.kutaka kumtoa mwanadam hofu ya misemo kama,SIKU YA HUKUMU,LIFE AFTER DEATH,KIAMA,HEAVEN,HELL n.k,vitu ambavyo kwa iman yao havipo na ni vya kufikirika.

FREE MASON NI DINI??

Kwa mtazamo wangu mimi masonic sio dini kam wengi wasemavyo,..,najua hujanielewa lakini em tufafanue nn maana ya dini,kwa nijuavyo mimi Dini ni aina ya maisha(/shughuli za kimaisha) ambayo mwanadam anaishi/anafanya kila siku.shughulizi hizo ni kama kuzalisha,kutambika,na tamaduni zote.kwa hiyo nikisema dini ni utamaduni nadhn bado ntakuwa sawa.

Lakini masonic sio dini,kwa hiyo pia sio utamaduni bali masonik ni IDEA,kijerumani wanaita IDEE,masonic ni idea tu ya kufanya jambo kwa misingi na utaratibu,na hata wanapokutana pamoja na karafa zao wanazoa ripoti za utendaji kaz na kupeana mikakati ya baaadae,( kwa hiyo sio dini bali ni idea tu.),


NB,niaminivyo mimi masonic ni kama Idea zingine ama theory tu.sifa nyingine tunazitoa sisi ambazo hata wao hawana wala hawajafikiria.,samahan kwa wale nilio wakwaza kwa uzi huu,ni mawazo yangu binafsi yaweza kuwa niko wrong pia.


,kwa maelezo zaidi,tafuta kitabi changa kinaitwa Free Ideas, cha 2013 july.

Ukipata nafasi tafuta project moja ya jamaa wawili wanajiita A noreagaa & Archenahr Production, Project yao inaitwa THE ARRIVALS, ni kama series hivi ina episode 51, Nadhani itajifunye vizuri hao jamii ni nani haswaa!
 
Ukipata nafasi tafuta project moja ya jamaa wawili wanajiita A noreagaa & Archenahr Production, Project yao inaitwa THE ARRIVALS, ni kama series hivi ina episode 51, Nadhani itajifunye vizuri hao jamii ni nani haswaa!



Niko nazo hizo SERIES za hao jamaa wamegusia mambo mengi sn Yani kila kitu Lkn Bado hawajafika ktk lengo lenyewe haswa!
 
Nilitaka uelezee Zaidi tu Mkuu juu ya swala la Imani ZA BABELI Na Tammuz kwa faida Zaidi ya Watu!

Hayo machache uko sawa!

Hapo sijalipata swali lako vizuri mkuu, Ila hawa watu waliokuwa wakimuabudu Tammuz waliamini katika Miungu mitatu yaani Mungu Jua, Mungu Mwezi na Mungu Nyota ambapo Mungu jua ni Nimrod, Mungu mwezi ni Semerimus na Mungu Nyota ni Tammuz ilikuwa ni ibada ya kipagani ila ilifuata ile trend kama ya Utatu mtakatifu yaani kwa kifupi naweza kusema waliufananisha utatu mtakatifu na miungu yao

2 Wafalme 23:5 Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni.

Nimekuwekea huo mstari kuonyesha hayo mambo Waisrael walirithi kutoka Babeli
 
Back
Top Bottom