Kwanini hatuna Wizara ya mafuta na gesi kama mataifa mengine yenye gesi na mafuta

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,316
8,227

Kwanini hatuna Wizara ya mafuta na gesi kama mataifa mengine yenye gesi na mafuta.​

Maoni yangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wizara ya Nishati

Mimi nashauri tungeanzisha wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas). Wizara ya nishati igawanywe mara mbili kuwa wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas) na wizara ya nishati (Ministry of Energy).

Wizara ya nishati (Ministry of Energy) ishughurikie usambazaji na uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo mbalimbali mfano maji, gesi, joto ardhi, upepo, jua, mawimbi ya bahari n.k. TANESCO iwe chini ya Wizara ya nishati. Ateuliwe waziri wa nishati muda wote awaze umeme tu ili kuharakisha na kuboresha uzalishaji na usambazaji wa umeme Tanzania.

Wizara ya mafuta na gesi ishughurikie mambo ya utafutaji wa mafuta na gesi (exploration), uzalishaji wa mafuta na gesi (production), usafishaji wa mafuta na gesi (refining), usambazaji wa mafuta na gesi (distribution), uuzaji wa mafuta na gesi (marketing), uingizaji mafuta kutoka nje ya nchi (import), na uuzaji wa gesi nje ya nchi (export), pamoja na conservation of petroleum, natural gas, petroleum products, and liquefied natural gas Tanzania. TPDC, PURA na EWURA ziwe chini ya wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gesi). Ateuliwe waziri wa mafuta na gesi aharakishe na kuiboresha sekta ya mafuta na gesi nchini. Waziri huyo akiwa ofisini kwake awaze mambo ya gesi na mafuta tu, hakika tutapata matokeo kama ya Qatar.

Maeneo muhimu ambayo ningependa hii wizara ihusike nayo ni haya yafuatayo.

1. Utafutaji (Exploration) wa rasilimali za mafuta na gesi asilia (methane na helium)

2. Uzalishaji, usambazaji, na uuzaji wa rasilimali za mafuta na gesi aina zote.

3. Viwanda vya kusafisha mafuta, vilainishi vya mashine, na viwanda vya kuchakata gesi asilia, gesi za vimiminika (LNG na LPG).

4. Matumizi ya gesi asilia kama malighafi ili kupata bidhaa zenye thamani kama mbolea, kemikali, plastics, mafuta n.k; Matumizi ya gesi asilia majumbani, viwandani, kwenye magari nk.

5. Mipango, uendelezaji na udhibiti na usaidizi kwa sekta zote zinazoshughulikiwa na Wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas).

6. Mipango, maendeleo na udhibiti wa huduma za mafuta na gesi.

7. Usimamizi wa Sheria mbalimbali zinazohusu Petroli na Gesi Asilia

Ninahisi ikiwa hivi tutaipunguzia wizara ya nishati mzigo, na tutaongeza ufanisi na ukuaji katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.

Bright and Genius Editors
Ni waandishi na wahariri wa documents mbalimbali
Tovuti: www.bgeditors.com
Barua pepe: contact@bgeditors.com
Namba ya simu/Whatsapp: +255687746471/+255612607426
 
Sisi tuna wizara ya nishati inayoshughulikia hayo mambo. Unataka wizara ya nishati ibaki na Tanesco tu? Kuongeza units za huduma na za kiutawala ni demand driven. Lazima kuwepo na mahitaji ya lazima. Ni gharama kuendesha wizara.
 
Kwanini hatuna Wizara ya mafuta na gesi kama mataifa mengine yenye gesi na mafuta.​

Maoni yangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wizara ya Nishati

Mimi nashauri tungeanzisha wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas). Wizara ya nishati igawanywe mara mbili kuwa wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas) na wizara ya nishati (Ministry of Energy).

Wizara ya nishati (Ministry of Energy) ishughurikie usambazaji na uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo mbalimbali mfano maji, gesi, joto ardhi, upepo, jua, mawimbi ya bahari n.k. TANESCO iwe chini ya Wizara ya nishati. Ateuliwe waziri wa nishati muda wote awaze umeme tu ili kuharakisha na kuboresha uzalishaji na usambazaji wa umeme Tanzania.

Wizara ya mafuta na gesi ishughurikie mambo ya utafutaji wa mafuta na gesi (exploration), uzalishaji wa mafuta na gesi (production), usafishaji wa mafuta na gesi (refining), usambazaji wa mafuta na gesi (distribution), uuzaji wa mafuta na gesi (marketing), uingizaji mafuta kutoka nje ya nchi (import), na uuzaji wa gesi nje ya nchi (export), pamoja na conservation of petroleum, natural gas, petroleum products, and liquefied natural gas Tanzania. TPDC, PURA na EWURA ziwe chini ya wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gesi). Ateuliwe waziri wa mafuta na gesi aharakishe na kuiboresha sekta ya mafuta na gesi nchini. Waziri huyo akiwa ofisini kwake awaze mambo ya gesi na mafuta tu, hakika tutapata matokeo kama ya Qatar.

Maeneo muhimu ambayo ningependa hii wizara ihusike nayo ni haya yafuatayo.

1. Utafutaji (Exploration) wa rasilimali za mafuta na gesi asilia (methane na helium)

2. Uzalishaji, usambazaji, na uuzaji wa rasilimali za mafuta na gesi aina zote.

3. Viwanda vya kusafisha mafuta, vilainishi vya mashine, na viwanda vya kuchakata gesi asilia, gesi za vimiminika (LNG na LPG).

4. Matumizi ya gesi asilia kama malighafi ili kupata bidhaa zenye thamani kama mbolea, kemikali, plastics, mafuta n.k; Matumizi ya gesi asilia majumbani, viwandani, kwenye magari nk.

5. Mipango, uendelezaji na udhibiti na usaidizi kwa sekta zote zinazoshughulikiwa na Wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas).

6. Mipango, maendeleo na udhibiti wa huduma za mafuta na gesi.

7. Usimamizi wa Sheria mbalimbali zinazohusu Petroli na Gesi Asilia

Ninahisi ikiwa hivi tutaipunguzia wizara ya nishati mzigo, na tutaongeza ufanisi na ukuaji katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.

Meneja wa Makampuni siku zote wewe huwa una mawazo mazuri sanaa
Hongera kwa hilo!
vipi Kuhusu Mabadiliko yaliofanyika Hivi Karibuni kwenye Mambo ya Gesi?
 
Mimi sidhani tunahitaji wizara. Maeneo yote uliyotaja hapo juu yanashughulikiwa na TPDC au PURA. Zinatosha kwa maoni yangu. Tunachohitaji ni kuwapeleka wataalum nje ya nchi wapate work experience kutoka nchi rafiki zenye uzoefu kwenye mafuta na gesi. Mimi nina experience kwenye sekta, nimefanya kazi kwenye multinationals za hapa ulaya. Ukipita na ukiongea na watalaam wa TPDC/PURA unaona uzoefu hawana wa kutosha, taasisi husika zinatakiwa ziongezee bidii kwenye hili. Tutaibiwa mchana kweupe.

Jingine ni kwanini waziri Makamba hajaiweka ile Host Government Agreement (HGA) wazi nchi nzima tuisome? Hizi agreements huwa zinawapa makampuni tax breaks and concessions, ni muhimu kujua what are getting ourselves into. Mh Makamba afungue hii mikataba, iwe wazi. Mfano wa HGA between BP and Azerbaijan huu hapa
 
Back
Top Bottom