MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,114
- 3,769
Ukisema kwamba Quran hairuhusu kuua mtu asiye na hatia unamaanisha nini?sijawahi ona andiko lolote ndani ya Quran linaloluhusu kuua watu wasio na hatia
kama wewe una andiko hilo liweke hapa watu waelimike mkuu
navyofahamu mimi msingi wa mfumo mzima wa dini ya kiislamu ni amani
na yatakiwa umpende muislamu mwenzio kwa mapenzi makubwa
na yule ambae si muislamu ufanye juhudi kwa kumuita katika dini kwa elimu na upole na sasa unapomuona mtu anaua binadamu mwinzie bila sababu huyo ana dhambi kubwa mbele ya Mungu
Amani ya Mungu iwe nawe
Je,mwenye hatia Ni halali Kuuawa kwa mjibu Quran?
Je,huyo mhusika Nani anasema anahusika kabla ya adhabu hiyo ya kifo?
Unajua uislamu Ni dini Nzuri Sana,Mimi Ni Mkristo lakini nimeishi na Waislamu Mkoani Tanga kwa Miaka 5. Hawa jamaa hawana shida kabisa.
Nadiliki kusema,uislamu ungelikuwa ndio dini iliyojikamilisha kuliko dini zote endapo kipengele Cha Jihad kisingelikuwepo. Kipengele hiki kinawapa Go ahaed hata Wenye dhambi Kama Taliban eti kutoa hukumu ya Kifo kwa Mtu aliyetenda uharifu.
Harafu,unaposema kuua mwenye hatia Ni sawa,je huyo mwenye hatia unamjuaje? Make hao wanajilipua na kuua wanawake na watoto huenda wao wanawaona wanahatia ilihali wewe unawaona hawana hatia. Tafsiri ya mwenye hatia na asiye na hatia ndio inaleta Mkanganyiko. Ni sawa na Kesi ya Uchochezi hapa kwetu,Hiyo kesi ya Uchochezi inafit popote pale wakiamua kukupa hiyo kesi,kwahiyo inategemeana na lengo la Mtoa hukumu tu.