Wanajeshi 7 wa Niger wauawa baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
1683530128421.png

Wanajeshi saba waliuawa Jumapili baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa ardhini katika eneo la Tillaberi magharibi mwa Niger, jeshi la Niger limesema.

Wanamgambo wa kiislamu hufanya mara kwa mara mashambulizi katika eneo hilo.

Gari lililokuwa limebeba bidhaa za wanajeshi lilikanyaga bomu hilo la kutegwa ardhini nyakati za asubuhi kwenye umbali wa kilomita 6 kutoka kijiji cha Samira, jeshi limesema katika taarifa.

Ni shambulio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Niger.

Nchi hiyo maskini ya eneo la Sahel inakabiliana na uasi wa wanamgambo wa kiislamu wanaohusishwa na Al-Qaeda na kundi la Islamic State.

Katika eneo la kusini magharibi, wanajeshi wa serikali wanapambana pia na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Niger inasaidiwa na nchi kadhaa za magharibi, zikiwemo Ufaransa na Marekani, ambazo zote zina kambi za kijeshi huko.
---

Landmine Kills 7 Soldiers in Niger
Seven soldiers were killed Sunday after their vehicle ran over a landmine in the Niger's western Tillaberi region, said the National Guard of Niger (GNN).

Jihadist fighters regularly launch attacks in the region.

A vehicle carrying supplies on a weekly delivery run hit the mine late in the morning 6 kilometers (4 miles) from Samira village, said the GNN in a statement.

The village, which lies not far from Niger's border with Burkina Faso in the southwest, has since 2004 hosted the country's only industrial-scale gold mine.

This assault was just the latest in a series of attacks against Niger's soldiers.

The impoverished Sahel country is grappling with an insurgency by jihadists linked to al-Qaida and the Islamic State group. In the southwest, they also have to contend with jihadist fighters from Boko Haram.

It is supported by a number of Western countries, including France and the United States, who both have military bases there.

Source: VOA
 
Waislamu Ni watu wazuri, Ila uombe usikutane waislamu wenye misimamo mikali ama itikadi kali. Muda huo reasoning inakuwa hamna kabisa.
 
Chanzo kikubwa ni umaskini.uliokithiri kwenye jamii nyingi.
Burundi ni maskini wa kutupwa, Zambia vilevile, Togo ndio usiseme na huko hakuna ugaidi kwa sababu vichocheo vya ugaidi havipo kule.
Kama ugaidi unachangiwa na umaskini basi nchi tajiri zisingekuwa nao
 
Mkuu huo ni utafiti uliofanywa mwaka huu na tv ya aljazera,kuwa ukanda wote huo wa sahel ,kutokana na mabadiriko makubwa ya tabia ya nchi,vijana wengi wanajiunga na makundi hayo ya kigaidi,ili kujipatia pesa!!ilikuwa ni documentary kabisa!!!na ndio maana hata wiki jana jeshi la burkinafaso lilivamia kjiji na kuwaua wana kijiji karibu 150!!kwa kuwatuhumu kushirikiana na makundi hayo ya kigaidi.
 
Mkuu unajua kuna nchi nyingine pia hapa Afrika ni maskini ila angalau wao wanajiunga na waasi wakilazimika, hawajiungi na magaidi wanaoua yeyote. Kuna kichocheo kikubwa kinachotafuta sababu kwenye huo umaskini ukanda huo, na kikiwa kanda nyinginezo kinatumia visingizio vingine
 
Burundi ni maskini wa kutupwa, Zambia vilevile, Togo ndio usiseme na huko hakuna ugaidi kwa sababu vichocheo vya ugaidi havipo kule.
Kama ugaidi unachangiwa na umaskini basi nchi tajiri zisingekuwa nao
Hakika
 
Hakuna kundi la kigaidi linapigania dini yote ni tumbo tu kupitia mgongo wa dini
 
Back
Top Bottom