Marekani yatoa 'msaada usio na kikomo' kwa rais aliyeondolewa madarakani Niger

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141

Rais wa Niger Mohamed Bazoum

CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Rais wa Niger Mohamed Bazoum
Maelezo kuhusu taarifa
  • Author,By Tchima Illa Issoufou & Cecilia Macaulay
  • Nafasi,BBC News, Niamey & London
  • 29 Julai 2023, 10:27 EAT
Marekani imetoa "uungaji mkono wake usio na kikomo" kwa rais aliyepinduliwa nchini Niger Mohamed Bazoum.
Bw Bazoum aliondolewa katika mapinduzi wiki hii yaliyoongozwa na Jenerali Abdourahmane Tchiani, anayejulikana pia kama Omar Tchiani, mkuu wa kitengo cha walinzi wa rais.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alionya wale wanaomzuilia Bw Bazoum kwamba "mamilioni ya dola za msaada" ziko hatarini.
Jenerali Tchiani hapo jana alijitangaza kuwa kiongozi mpya wa nchi.
Bw Bazoum ndiye kiongozi wa kwanza wa Niger kuchaguliwa kumrithi mtangulizi wake tangu uhuru mwaka 1960.
Alikuwa akichukuliwa kuwa mshirika mkuu na mataifa ya Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kijihadi katika eneo hilo. Kwa sasa anadhaniwa kuwa na afya njema, na bado anashikiliwa na walinzi wake.
Bw Blinken alimpigia simu Bw Bazoum kwa mara ya pili ndani ya siku nyingi, akisema kwamba Washington itaendelea kufanya kazi ili "kuhakikisha utaratibu wa kikatiba na utawala wa kidemokrasia nchini Niger unarejelewa".
Katika wito tofauti kwa Mahamadou Issoufou - ambaye alikuwa rais wa Niger kabla ya Bw Bazoum - Blinken alisema "anasikitika kwamba wale wanaomzuilia Bazoum walikuwa wakitishia miaka ya ushirikiano wenye mafanikio na mamilioni ya dola" katika usaidizi, msemaji wa idara hiyo Matt Miller alisema.
Niger

CHANZO CHA PICHA,AFP
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa wito wa kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa Bw Bazoum na kulaani "juhudi za kubadilisha serikali halali" ya Niger kinyume na katiba.
Ufaransa, ambayo himaya yake ya kikoloni ilijumuisha Niger, imesema haimtambui kiongozi yeyote wa mapinduzi hayo na kwamba itamtambua tu Bw Bazoum kama mkuu wa nchi.
"Tunasisitiza haja ya kurejeshwa mara moja kwa utaratibu wa kikatiba na mamlaka ya kiraia iliyochaguliwa kidemokrasia," taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilisema.
Mapinduzi hayo yameingiza eneo la Sahel katika sintofahamu zaidi baada ya hatua kama hiyo huko Burkina Faso na Mali.
Imelaaniwa vikali na mashirika ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Afrika, kambi ya kanda ya Afrika Magharibi (Ecowas), EU na Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner nchini Urusi ameripotiwa kupongeza mapinduzi hayo na kuyataja kuwa ya ushindi.
"Kilichotokea Niger si kingine bali ni mapambano ya watu wa Niger dhidi ya wakoloni wao," Yevgeny Prigozhin alinukuliwa akisema kwenye chaneli ya Telegram inayohusishwa na Wagner.
BBC haijafanikiwa kuthibitisha u wa halisia wa maoni yake yaliyoripotiwa.
Kundi la Wagner linaaminika kuwa na maelfu ya wapiganaji katika nchi zikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Mali, ambako lina maslahi ya kibiashara lakini pia linaimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi wa Urusi. Wapiganaji wa Wagner wameshutumiwa kwa kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika nchi kadhaa za Afrika.
Ramani

Jenerali Tchiani, 62, amekuwa akisimamia walinzi wa rais tangu 2011 na alipandishwa cheo na kuwa jenerali mnamo 2018 na Rais wa zamani Issoufou.
Pia alikuwa amehusishwa na jaribio la mapinduzi ya 2015 dhidi ya rais wa zamani, lakini alikanusha mahakamani madai hayo na kuondolewa msahataka.
Akizungumza katika hotuba ya televisheni, Jenerali Tchiani alisema mamlaka yake ilichukua uongozi kwa sababu ya matatizo kadhaa nchini Niger, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa usalama, matatizo ya kiuchumi na rushwa, miongoni mwa mambo mengine.
Pia alihutubia washirika wa kimataifa wa Niger, akisema jeshi litaheshimu ahadi zote za kimataifa za nchi hiyo, pamoja na haki za binadamu.
Lakini jeshi hilo limekosoa vikali wale wanaowapinga, likiwashutumu wajumbe wa serikali iliyoondolewa madarakani ambao wamekimbilia katika balozi za kigeni kwa kupanga njama dhidi yao.
Walisema jaribio lolote la aina hiyo litasababisha umwagaji damu, jambo ambalo hadi sasa limeepushwa.
Maisha katika mji mkuu Niamey kwa kiasi kikubwa yamerejea katika hali ya kawaida huku masoko na maduka yakiwa yamefunguliwa, lakini watumishi wa umma wameambiwa warudi nyumbani.
Wakati huo huo wananchi wa Niger wamekuwa na hisia tofauti kuhusu mapinduzi hayo, huku wengine wakisema ukosefu wa usalama nchini humo haukuwa mkubwa kiasi cha kuhalalisha mapinduzi. Lakini wengine wameunga mkono jeshi.
Télé Sahel

CHANZO CHA PICHA,TELE SAHEL
Maelezo ya picha,
Jenerali Tchiani
Mapinduzi ya Niger ni ya hivi punde zaidi katika wimbi la mashambulizi ya kijeshi yaliyokumba eneo la Afrika Magharibi katika miaka ya hivi karibuni, na kuziangusha serikali katika nchi zikiwemo Mali, Guinea na Burkina Faso.
Pia inakuja kama pigo kubwa kwa uongozi wa Ecowas. Wiki mbili zilizopita, mwenyekiti wa umoja huo, Rais Bola Tinubu, alionya kwamba ugaidi na mtindo unaoibuka wa mapinduzi katika eneo la Afrika Magharibi umefikia viwango vya kutisha na kutaka hatua za haraka na za pamoja kuchukuliwa kukomesha hali hiyo.
Sasa kuna wasiwasi katika kanda ya Afrika Magharibi kuhusu nchi ambazo kiongozi mpya wa Niger ataungana nazo. Sasa kuna wasiwasi katika kanda ya Afrika Magharibi kuhusu nchi ambazo kiongozi mpya ataungana nazo. Majirani wa Niger, Burkina Faso na Mali, wote wameegemea Urusi tangu mapinduzi yao wenyewe.
Haya ni mapinduzi ya tano nchini Niger tangu ilipojinyakulia uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, pamoja na majaribio mengine yaliyotibuka ya kuchukuwa mamlaka ya nchi hiyo.
Ramani

chanzo.BBC
 
Naona maslahi ya za nchi za magharibi yameguswa pakubwa sana. Afrika inaanza kuamka sasa
 
Back
Top Bottom