Niger: Wanamgambo wavamia Msikiti, raia kumi wauawa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wenye msimamo mkali wamewauwa wanakijiji 10 katika shambulizi la msikitini mapema wiki hii magharibi mwa Niger.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Tillaberi kwa mujibu wa taarifa za wakazi wa eneo za Jumatano.

Shambulizi la Jumatatu lilifanyika katika Kijiji cha Abankor katika eneo la mpaka unaokutanisha mataifa matatu ya Niger, Mali na Burkina Faso.

Afisa wa mji wa Banibangou ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba washambuliaji hao waliwasili wakiwa katika pikipiki wakati wa sala ya jioni, na walio uwawa walikuwa ndani ha msikiti.

Mkazi wa mji wa karibu wa Tondiwindi alithibitisha kutokea kwa shambulizi hilo na idadi ya vifo.

Moja ya kituo cha redio katika meneo hayo kimetangaza zaidi ya watu 10 waliouwawa na kuongeza kwamba shambulizi lilitokea mapema jioni.
 
Huwa napata shida sana kuelewa imani ya uisilamu. Kuna mafundisho fulani nahisi huwa ni halali lakini huenda hayawekwi hadharani kwa kuwa kijamii ni haramu
Hakuna jambo lolote la siri katika uislamu, vilevile hakuna mazingira (katika uislamu) yoyote yale inaruhusiwa kuuwa watu aidha wawe msikitini,kanisani au mahala pengine. Hao wanaouwa watu na kuitwa eti ni waislamu wenye itikadi au misimamo mikali they are criminals like other criminals.
 
Kwanini kile kitabu hakitafsiriwi kwa lugha mbalimbali ili kila mtu aweze kusoma na kuelewa yaliyomo?
 
Wakati dini za kigeni hazijaletwa Afrika tulikuwa na raha sana, ujinga kama huu usingetokea au hata kama wangejaribu wangejuta kuzaliwa.
 
Kwdli chuki na roho mbaya haimwachi mutu salama,
Yaani watu wakiua kanisani ni waislamu, wakiua baa ni waislamu, wakiua sijui mall ni waislamu sasa wameua msikitini pia ni waislamu?!
Hembu shtukeni wandugu tafuteni ukweli
Angalau mujadili kiuadilifu
 
Alafu et turuhusu hawa wapuuzi watawale dunia kwa taratibu zao izi za kipumbavu?

Hiki ni mojawapo ya kizazi ambacho kinapaswa kifutiliwe mbali kulinda amani ya dunia.
Na wenzako pia wanasema hatuwezi kuruhusu dini inayokubali kuowana wanaume kwa wanaume itawale dunia
Kaazii kweli kweli
 
Hao ni mawakala wa shetani tu hawana tofauti na wale Taleban, hata kama una msimamo kiasi gani unawezaje kuua mtu asiye na hatia tena yupo nyumba ya ibada
Ni kweli na wakala anaweza kuwa dini yeyote, sio lazima awe muislamu inawezekana pia wakawa ni wale wa dini pendwa ya wadhungu
Mashetani na mawakala wakuu wa gujonkwa kisingizio cha elimu ya juu
 
Kwdli chuki na roho mbaya haimwachi mutu salama,
Yaani watu wakiua kanisani ni waislamu, wakiua baa ni waislamu, wakiua sijui mall ni waislamu sasa wameua msikitini pia ni waislamu?!
Hembu shtukeni wandugu tafuteni ukweli
Angalau mujadili kiuadilifu

ni jukumu lenu waislam kukemea hao watu wasitumie kivuli cha dini yenu ila kukaa kwenu kimya kunehalalisha ubaya WAP uwe ndo ubaya wa uislamu. , mtu akimwanyooshea kidole msilalame
 
Back
Top Bottom