Mapinduzi Niger: Makao makuu ya chama tawala yashambuliwa baada ya Rais Bazoum kuondolewa madarakani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
Niger

CHANZO CHA PICHA,EPA
28 Julai 2023
Wafuasi wa mapinduzi ama watu wanaounga mkono mapinduzi nchini Niger wameyashambulia makao makuu ya chama cha rais aliyepinduliwa na kuyachoma moto, kurusha mawe na kuchoma magari yaliyokuwa nje.
Kikundi kidogo cha wachomaji moto kilikuwa kimejitenga na kundi kubwa la waandamanaji wakionyesho kuunga mkono viongozi wa mapinduzi nje ya bunge, ambapo bendera za Urusi zilikuwa zikipepea.
Jeshi la nchi hiyo limeunga mkono wanajeshi waliomteka Rais Mohamed Bazoum siku ya Jumatano.
Urusi iliungana na nchi nyingine na Umoja wa Mataifa katika kutoa wito wa kuachiliwa kwa Bw Bazoum.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 64, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Niger miaka miwili iliyopita, ni mshirika mkuu wa Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu katika eneo la Afrika Magharibi.
Marekani na Ufaransa, taifa lenye nguvu ya kikoloni, zote zina kambi za kijeshi katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini ya uranium - na zimelaani mapinduzi hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alimpigia simu Bw Bazoum akiahidi "uungwaji mkono usioyumba" wa Washington.
Umoja wa Mataifa (UN) umesema umesitisha shughuli zake za kibinadamu nchini Niger. Haijabainika iwapo mapinduzi hayo ndiyo yalisababisha kusitishwa huko.
Umoja wa Mataifa umesema hapo awali zaidi ya watu milioni nne nchini Niger wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Niger

CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Mapinduzi hayo yalitangazwa na msemaji, Kanali Maj Amadou Abdramane,
Siku ya Alhamisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitaka kuachiliwa kwa Bw Bazoum "mara moja na bila masharti".
Bw Bazoum alituma taarifa kwenye mtandao wa twitter siku ya Alhamisi asubuhi ukisema: "Mafanikio yaliyopatikana kwa bidii yatalindwa. Wananchi wote wa Niger wanaopenda demokrasia na uhuru wataona hilo."
Waziri wake wa mambo ya nje pia amekuwa akijaribu kuunga mkono na kuhimiza mazungumzo, lakini mkuu wa majeshi alisema anaunga mkono mapinduzi hayo ili kuepusha mapigano ndani ya vikosi vya jeshi.
Bado haijafahamika ni nani hasa anaiongoza Niger kwani serikali ya kijeshi haijatangaza kiongozi wake.
Televisheni ya Taifa imekuwa ikirudia tangazo la mapinduzi ya usiku lililochanganyikana na muziki wa kizalendo na aya za Qur'ani - na taarifa yake ya kawaida ya wakati wa chakula cha mchana haikuonyeshwa.
Lakini katika mji mkuu, Niamey, maduka na masoko yalifunguliwa kwa biashara na baada ya kuchelewa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mapema asubuhi, wafuasi wa mapinduzi waliingia mitaani.
Mamia waliokusanyika nje ya Bunge walikuwa na bendera za Urusi, huku wengine wakiinua mabango yaliyoandikwa kwa mkono yakisema: "Ondoka na Ufaransa" na "Kambi za majeshi ya kigeni ziondoke".
niger

CHANZO CHA PICHA,AFP
Polisi baadaye walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya waliokuwa wamekusanyika katika makao makuu ya chama tawala, ambapo wanaharakati wa chama hicho walikimbia walipowaona waandamanaji wakija.
Baadhi ya watu walijeruhiwa katika tukio hilo huku magari yaliyoteketezwa kwa moto yakionekana kuzingira jengo la chama cha PNDS Tarraya.
Wafuasi wa mapinduzi wanakishutumu chama hicho kwa ufisadi na kutofanya vya kutosha kuboresha hali ya usalama na kumaliza uasi wa muda mrefu wa wanajihadi.
Nchi mbili jirani, Mali na Burkina Faso, zimekumbwa na mapinduzi yaliyochochewa na maasi ya Kiislamu katika miaka ya hivi karibuni.
Katika nchi zote mbili viongozi wapya wa kijeshi wamesogea karibu na Urusi baada ya kutofautiana na Ufaransa.
"Natumai wataweka usalama mzuri katika jiji na kutusaidia kufikia hali bora, kwa sababu tuna rasilimali nzuri. Sijali kama wanataka tu kufuata nyayo za Burkina Faso au Mali," Djibo, mfuasi wa mapinduzi hayo aliambia BBC.
Wachambuzi kadhaa maarufu wanaoiunga mkono Kremlin kwenye Telegram - mojawapo ya majukwaa machache makubwa ya mitandao ya kijamii ambayo hayajapigwa marufuku nchini Urusi - wamekuwa wakituma maoni kuunga mkono mapinduzi hayo, wakisema ni fursa kwa Urusi na Wagner kuingia Niger.
Kwa sasa, hakuna ushahidi wa kuhusika kwa Urusi katika mapenduzi haya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema utaratibu wa kikatiba nchini Niger unapaswa kurejeshwa, Reuters inasema, ikilinukuu shirika la habari la serikali la Urusi la Tass.
Baadhi ya mashirika ya kiraia nchini Niger yamekuwa yakitoa wito wa kuchana na Ufaransa na Urusi katika wiki za hivi karibuni.
Jeshi limeikemea Ufaransa kwa kukiuka kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo baada ya ndege ya kijeshi kutua katika kambi ya jeshi la anga siku ya Alhamisi asubuhi.

Mapinduzi haya ni habari mbaya kwa Magharibi​

Mapinduzi haya ni habari mbaya zaidi kwa juhudi za Ufaransa na Magharibi kurejesha utulivu katika eneo la Afrika Magharibi linalojulikana kama Sahel. Wakati nchi jirani ya Mali ilipochagua kushirikiana na Kundi la Wagner la Urusi badala ya Wafaransa, Paris ilihamisha shughuli zake kuu kutoka eneo hilo hadi Niger.
Mapinduzi haya, hata kama yatatokea kuwa ya muda mfupi, yameonyesha kwamba hata Niger haiwezi kutegemewa kuwa msingi salama wa kudumu. Ushawishi wa Magharibi katika eneo hilo unapungua kama bwawa la maji wakati wa kiangazi.
Serikali za Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Mali zote zimeamua kwamba zingependelea kufanya kazi na mamluki wa Wagner kuliko jeshi lolote la Magharibi. Maslahi ya msingi ya Wagner barani Afrika yameonekana kuwa zaidi ya kujitajirisha na kupanua ushawishi wa Kremlin kuliko kufuata malengo ya Magharibi ya kujaribu kukuza utawala bora.
Kwa makundi mawili makubwa ya waasi katika kanda, yale yanayohusishwa na kile kinachoitwa Islamic State na al-Qaeda, hii ni habari njema. Wanastawi kwa kukosekana kwa utulivu, utawala mbovu na chuki za serikali za mitaa. Kwa hivyo mapinduzi nchini Niger huenda yakatatiza zaidi juhudi za kuyadhibiti.
Niger

Matukio haya yamewagawa watu wa Niger - na wengine wameshtuka na kufadhaika.
Wakati ikiendelea siku ya Jumatano, mamia ya wafuasi wa rais walikaidi wanajeshi hao na kuandamana kuwataka wanajeshi kurejea kambini.
Walitawanyika baada ya risasi za onyo kufyatuliwa - ikiwa ni milio ya risasi pekee iliyosikika katika mapinduzi haya ya madaraka yaliyofanyika bila kumwaga damu.
"Mapinduzi yanasikitisha sana. Inanihuzunisha kwa sababu naitakia mema nchi yetu. Niger itarejea sasa," Mustapha, mkazi wa Niamey alijificha nyumbani na mkewe na mtoto wa kiume wa miaka mitatu, aliambia BBC.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger Hassoumi Massoudou ametoa wito kwa wakazi kupinga mapinduzi hayo.
Katika mahojiano na idhaa ya France24, alisema kuwa hali hiyo bado inaweza kutatuliwa kupitia mazungumzo na kusema wajumbe waliotumwa kutoka nchi jirani ya Nigeria walikuwa wakizungumza na wanajeshi.
Rais wa Benin Patrice Talon ambaye alipanga kuwa na ujumbe wa upatanishi kwa niaba ya jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas, amelazimika kuachana na safari yake ya kwenda Niger kwa sababu ya kufungwa kwa mpaka.
Nchi hiyo kubwa kame kwenye ukingo wa jangwa la Sahara - moja ya mataifa maskini zaidi duniani - imekumbwa na mapinduzi manne tangu uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, pamoja na majaribio mengi ya mapinduzi. chanzo.BBC
 
Democracy in Africa is like child's attempt to walk, it will take a myriad of generations for this impoverished continent to come to terms with democracy.
 
Back
Top Bottom