Nifanyeje nizoeane na majirani?

Jirani yangu alikuwa mchangamfu sana kabla sijahamia na vitu alinihifadhia yeye na vingine naazima vya ujenzi, tena akisisitiza 'hamia hivyohivyo jirani mbona poa tu?' Nimehamia kawa kauzu na ikitokea tumekutana kwa bahati ananiwekea ukuta kwa kila niliyeanza kuzoeana naye, mara huyu mnafiki huyu mbaya nk nk. I'm baffled.
Heeheee
 
Kuna jamaa mmoja nadhani ni mgeni kwenye eneo hili, yeye amejijengea utaratibu wa kugawa pipi kwa watoto wa mtaa mzima. Mwaka unaende kukatika sasa lakini amekuwa maarufu kwa watoto wa mtaani na hata mitaa mingine ya jirani. Kwenye begi lake anatembea na fuko la pipi akiwagawia watoto kila anapowaona.... Ukisikia Babuu!.. Babuu!... ujue tu anafanya shughuli yake ya kukusanya watoto kama mpiga filimbi wa Hamelin.
Hii pia ni mbaya mtoto akipata food poison sehemu nyingine akafa jumba bovu linamuangukia huyo
 
Huna mke na watoto?Hao ndiyo kiboko kwa kuanzisha ujirani.Kama kuna mini-bar jirani na unatupia chombo nenda utawajua majirani.😝😝😝😝😝😝😝
 
Hahahah ndio si kutafuta kuonekana jirani mwema tu ! Mie siwezi ila nawashauri wanaoweza tu wafanye hivyo maana dah! Mie naweza kukaa ndani hata siku 2 bila kutoa unyayo nje as long as huduma zote nazipata frijini, jikoni na chooni kukaa vijiweni ni very rare case labda nikakae mbali sana na home! Na ndio maana JF is my first kijiwe
Sawa tunawahitaji sana watu lkn inabidi uwe makini sana

Kuna mmoja kasema eti ukae nao baa za kitaa ulewe nao

Pombe unaijua hujaropoka mambo yako kwao, usiku hao hao wanakuingilia mapanga shaa
 
Umemmaindi sana dah,,, sema ndio hivyo mie mwenyewe nahisi kuna watu watakuwa wanahisi ninaringa ila mie sina habari! Sifa nilionayo tu kitaa wanajua mie sio kicheche na kijana mpole sana
kumbe mzee wa utelezi

Haahaahaa
 
Wewe ukija huku united states na europe utapata shida sana. Ni kitu cha kawaida mno. Hao sasa wameadapt maisha ya wazungu na ndipo tunakoelekea siku 1000 zijazo
 
Tangu nimehamia hapa mtaani ni takribani mwaka sasa umekatika. Mtaa ninaoishi ni nje kidogo ya mji ambapo watu wamejenga nyumba zao wamezungusha fensi na mageti. Pia wengi (pamoja na mimi) ni wafanyakazi ambapo mara nyingi ni watu wa kutoka asubuhi na kirudi jioni wakiwa ndani ya magari yao.

Sasa leo nimekaa nikatafakari, nikagundua kuwa zaidi ya majirani niliopakana nao upande wa kushoto na kulia, hakuna jirani mwingine ambaye walau hata namjua kwa jina. Hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati yangu na majirani zangu, hakuna tukio lolote linalotukutanisha, na hata ikitokea mtu akapata tatizo, sidhani kama kuna mtu atajitokeza kusaidia.

Mimi naona kama hii hali sio nzuri ila nashindwa kujua nifanyeje ili kujenga ujirani mwema, hasa kwa hawa majirani wa mbali kidogo nyumba ya tatu ya nne huko?
Watangazie kuna kiti moto bure.
 
Kuna jamaa mmoja nadhani ni mgeni kwenye eneo hili, yeye amejijengea utaratibu wa kugawa pipi kwa watoto wa mtaa mzima. Mwaka unaende kukatika sasa lakini amekuwa maarufu kwa watoto wa mtaani na hata mitaa mingine ya jirani. Kwenye begi lake anatembea na fuko la pipi akiwagawia watoto kila anapowaona.... Ukisikia Babuu!.. Babuu!... ujue tu anafanya shughuli yake ya kukusanya watoto kama mpiga filimbi wa Hamelin.
Atapewa kesi ya ubakaji soon
 
Huyo Mtume Muhammad unaemsema amehusia Sana watu waishi kwa wema na akazitaja had haki za jirani kwa jirani mwenzake
Kama husalimii majiran na unajitenga nao ww bado humfati Muhammad (S.A.W
Hakuna sehhemu nimesema sisalimii majirani. Hakuna sehemu nimesema najitenga na majirani.
 
Itisha kikao kwa majirani wote alfu jiteue kuwa mwenyekiti au balozi au mtafute mwennyeji wa muda muweke kikao Cha ujirani mwema hapo mtampata majiran wote.
 
Back
Top Bottom