Nifanyeje na hawa wenzangu? Ninajibu sana maswali naonekana nina kiherehere

Nasoma lakini katika kusoma kwangu nimezoea kujibu jibu maswali hadi inafika muda mwalimu ananiambia nipumzike lakini sio kusema kwamba wengine hawajui sijui kwao ni hofu kujibu au hawajisikii lakini sio kusema kwamba hawaelewi wanaelewa ila hawataki kuparticipate.

Sasa naona kama wananiona nina kiherehere kujiona naelewa sana, nina mpango wa kukauka class yaani nisiwe na jibu na mimi. Maana unajibu sana mtihani wanakupita kama so flani hivi hahaha.
Hakuna zuri duniani. Kama hukurupuki bali unajibu baada ya kulifikiria swali na kufanyi tafakuri-basi usiwe na wasiwasi, hiyo inakusaidia na walimu wengi pamoja na maprof hupenda vijana wenye tabia kama hiyo.
Sasa tunapishana wengine hawata jibu hadi mwalimu awaulie moja kwa moja au wanasubiri mitihani. Kwa mwalimu hawezi kufagilia tabia hiyo hata kama wewe ni kipanga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom