Nifanyeje madogo wasiingie chumbani ninakolala

Nifanyeje madogo wasiingie chumbani ninakolala

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
323
Reaction score
1,128
Aisee,nipo nyumba ya kupanga nimeweka dressing table Ina kioo, wadogo zangu wanapenda kunitembelea, wakifika tu kunitembelea lazima wazame chumbani niwepo nisiwepo,hata nisipokuepo lazima utakuta mabadiliko chumbani,nikasema isiwe kesi niweke kioo full sebureni hapa nilipoweka kochi na tv lakini bado lazima waende chumbani ni wadogo zangu wa damu mama mmoja baba mmoja,wa kiume lazima azame room shida ni kwamba chumba hakina mlango kina pazia tu ni ramani ya nyumba yenyewe mlango uko mmoja tu wa sebureni.huyu wa kike utakuta mimi nimekaa hapa sebureni utakuta anapitiliza moja Kwa moja chumbani vipi wakimkuta mwanaume wangu huko ndani amelala,ndio naishi peke angu lakini uwezi jua na mimi ni binadamu siku wakimkuta mtu huko room kwangu factly nakerekwa Sana na tabia Yao hii ya kuingia room bila utaratibu.leo Hadi nimeandika hivi nimekerekwa zaidi Kuna kipimo Cha mimba nilipima jana nilikiacha tu juu kwenye dressing table sikujua kama atafika dogo Leo home.
 
Aisee,nipo nyumba ya kupanga nimeweka dressing table Ina kioo,mda wakifika tu kunitembelea lazima wazame chumbani niwepo nisiwepo,nisipokuepo means wanaombaga funguo lakini wakitoka nikija najua tu chumbani Kuna mtu aliingia ,nikasema isiwe kesi niweke kioo full barazani hapa nilipoweka kochi na tv lakini bado lazima waende chumbani ni wadogo zangu wa damu mama mmoja baba mmoja,wa kiume
Inawezekana huko kwenu na wewe zilikuwa pigo zako!,Waambie sio poa kabisa.
 
Wanakuona pia kama mdogo wao, hujakaa kikomavu kuanza kulea familia mpaka kutoa amri kipi kifanyike na kipi kifanywe ndani ya Nyumba


Nakushauri acha hela flani juu ya meza halafu waidokoe..

Ukija anzia kesi hapo piga na mkwara wa kuingia room kwako
 
Nadhani issue ni mazoea Kuna familia wamezoea kuingia room ya huyu hivyo Ila kwa mipaka.... Kikubwa isipitilize hasa chumba Chako na we ni mdada
 
Jambo dogo kama hili nalo huwezi kulitatua? Kama ni wadogo zako unashindwaje kuwaamru waache hiyo tabia?
Hawakawii kukasirika wataanza kuninanga mi katili siwajali ,na wanaweza stop kabisa kuja ni wakubwa Wana miaka ishirini na Tano kwenda juu
 
Weka picha ya chumba kwa faida ya members
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom