Nifanyeje ili niondokane na maumivu haya?

Nifanyeje ili niondokane na maumivu haya?

Habari wana jamvi,
Mimi ni kijana wa miaka ishirini na mbili pia ni mwanachuo. Nimeleta uzi huu jamvini kwa lengo la kupata msaada utakao nisaidia kuondokana na maumivu haya.

Kuna binti mmoja nipo naye kwenye mahusiano ninampenda sana naweza kusema nampenda kuliko mtu yeyote chini ya jua hili na hata yeye unalitambua hilo, shida iliyopo ni kuwa si msikivu na ananichukulia poa sana licha ya kuwa unafanya mengi kwa ajili yake lakini mwenzangu haoneshi kujali hata kidogo anajiamulia mambo yake mwenyewe bila hata kunishirikisha kama mme wake mtarijiwa.

Kutokana na hali hiyo wakati mwingne nashindwa hata kusoma, kula na kufanya vitu vngine pia.

Ninachokifikiria ni kwenda kwa mganga kumtafutia dawa kwa sababu siwezi kumuacha na sitaki kumuacha.

Ila naomba mawazo yenu pia ili nijue ni kipi napaswa kufanya.

Natanguliza shukrani
Ndicho kilicho kupeleka chuo? Miaka 22 ati mume mtarajiwa wake, hebu someni acheni upuuzi
 
hukuzaliwa nae huyo umemkuta tu
Acha uboya dogo fanya kweli kwenye masomo huyo unaempenda ana mwingine ambae yeye anampenda cha kufanya we rudisha mapenzi kwa mama mzazi aliekuleta duniani achana na huyo mbulura
Kuomba advice its good lakini ni vizuri zaid mambo yako ya ndani,
umushirikishe mtu wako wa karibu tena yule unamwamini coz sio kila utakaemwomba akushauri atakushauri vema au ataguswa na matatizo uliyonayo wengine wanafurahi kuona uko kwenye matatizoo.
Pole sana, i know how it feels as a MAN unapompenda mwanamke wako wa kwanza.

Mimi ishanikuta iyo hali, ila kwa sasa nahis a human part of me ishaondoka, nikiwa na demu anipende its fine, asinipende it also fine nipo 50%,50%. @lee Choo in
Time will heal you
Hivi hayo mnayomwambia huyu dogo anajua basi, labda mngemshauri asome mwambieni gari ina utaalam wake sio kupanda na kushuka
 
Duuu kupenda kuna kaz kweli kwa MTU asiye kupenda so lazima uyo
 
Hivi elimu yetu ndo imefika hapa msomi wa chuo kikuu kbsa anafikri kwenda kwa mganga kwa ajili ya mapenzi. Karne hii 21ya utandawazi na ushindani wa hali ya juu basi maendeleo tutakuwa tunaona kwenye tv
 
Mfundishe yeye pia kukujari kwa kufanya haya.. Ukuona mtu hana habari na wewe mpuuzie.... usijadiri mambo anayokukosea fanya yako....jipende wewe mwenyewe kuwa huru kufanya mambo yako bila kumjari itakufanya usonge mbele... jifunze kutomjari... ukiona hana habari na wewe zaidi... tafuta mwengine tu
Mwache aende zake sivyo atakutambulisha kwa mwanaume mwingine kuwa wewe x-boi friend wake jicho likutoke...watoto wazuri kila sekunde wanazaliwa boi asikusumbue .. kubari akupite pembeni fanya maisha yako mengine
 
Hutamuoa huyo usijidanganye. Komaa na kitabu tu, Kama upo nae jua kwa starehe tu. Ww mwenyewe miaka 22 demu labda 20 afu mnasoma. Ww unaanza kumbebesha majukumu makubwaaaa et Mme mtarajiwa. Soma kwanza
 
Dogo unasikitisha, kweli kabisa mtu mmoja asiekupenda wala kukujali anakupa stress kiasi cha kushindwa kufanya mambo ya muhimu kama kusoma, kula, au kuwa na furaha?
Acha kusoma, ufeli, uishi bila qualification wala kazi ya maana uje uone jinsi ulivyochezea muda wako kwa kuupoteza kwa mpuuzi mmoja tu asie na maana.
Wanawake wako wengi sana tena kuna wazuri utakaokutana nao, huyo utamuona kama kitoto cha Sokwe, kinachokusumbua sasa ni hormones tu zinazokuletea picha na maono yasiyo na uhalisia. Amka acha kuota bwana mdogo, miaka 22 ni michache sana kujiita mume mtarajiwa wa mtu.
 
Back
Top Bottom