Nifanyeje ili niondokane na maumivu haya?

Lee Cho in

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
941
693
Habari wana jamvi,
Mimi ni kijana wa miaka ishirini na mbili pia ni mwanachuo. Nimeleta uzi huu jamvini kwa lengo la kupata msaada utakao nisaidia kuondokana na maumivu haya.

Kuna binti mmoja nipo naye kwenye mahusiano ninampenda sana naweza kusema nampenda kuliko mtu yeyote chini ya jua hili na hata yeye unalitambua hilo, shida iliyopo ni kuwa si msikivu na ananichukulia poa sana licha ya kuwa unafanya mengi kwa ajili yake lakini mwenzangu haoneshi kujali hata kidogo anajiamulia mambo yake mwenyewe bila hata kunishirikisha kama mme wake mtarijiwa.

Kutokana na hali hiyo wakati mwingne nashindwa hata kusoma, kula na kufanya vitu vngine pia.

Ninachokifikiria ni kwenda kwa mganga kumtafutia dawa kwa sababu siwezi kumuacha na sitaki kumuacha.

Ila naomba mawazo yenu pia ili nijue ni kipi napaswa kufanya.

Natanguliza shukrani
 
Ukishindwa kusoma utafeli
ukifeli maisha yatakuendea kombo kwa namna moja au nyingine

hivyo basi binti atabebwa na wenye nazo

Ukienda kwa mganga dawa zitakapoisha kazi atakukimbia

Hawa wanawake hawatakiwi wapendwe sana au usimwoneshe kama unampenda wanabweteka

Cha kufanya endelea kusoma tatizo watoto wa chuo mkipata demu mzuri kisha akakuzingua utaona huwezi kupata mzuri kama huyo hilo sio kweli
 
Asante kaka asante sana
 
Unalipiwa ada na loans board au na wazazi wako? Au chuo cha utalii ndo unasoma
 
Huyo atakuwa demu wako wa kwanza, ukiachana na huyo ukapata mwingine naye mkaachana utawazoea.

Huyo demu anakudharau kwa sababu anajua kipato chako, ikibidi hata uwezo wako kichwani anaudharau na ukute anaambiwa na watu kibao kwamba ni mzuri, anapata kiburi ndo maana anakuzingua.

Uwe unampa muda na punguza kumwaza zaidi, waza kufanikiwa kimasomo na kimaisha, hii itakujengea heshima kwake na kwa wengine utakao wakuta kitaa.

Mtaani/makazini kuna wanawake wazuri sana, huyo asikuzuzue.
 
Hongera saaaana, ni chuo cha utalii au secretarial.
But mi nakushauri tu uende kwa mganga mwambie amfanye ndondocha kabisa ili asikuache.
Asante binadamu kama wewe wanatakiwa kuwepo pia ili yaliyotabiliwa yatimie
 
Hahahahahah ibra87 njoo nioe tafadhali.....
 
Last edited by a moderator:
Kijana pole kwa hayo unayoyapitia,ila tatizo ninaloliona haliko kwa binti tatizo unalo wewe unaiminisha akiri yako kuwa huwezi kumuacha ndivyo itakavyokuwa na binti nae anajua unampenda atakufanyia kila aina ya ujinga kadri awezavyo kwa sababu anajua hupindua kwake.

Ushauri hakikisha unatumia akiri ktk kufikiri na sio hisia kama ufanyavyo sasa,by the way uamuzi unao wewe kuamua kufikiri na kuwa na mtazamo tofauti kuhusu mapenz au kuendelea kuwa mtumwa wa hisia
 
Katika vitu vigumu kulazimishwa humu duniani ni mapenzi, mtu kama hakupendi ni hupendwi tu hata ufanyeje it won't change, sana sana unajisogezea tu maumivu mbele, bora uutoe mwiba uliokuchoma sasa hivi kuliko kuendelea kusikilizia maumivu utoe kesho
 
Huyo atakuwa demu wako wa kwanza, ukiachana na huyo ukapata mwingine naye mkaachana utawazoea.

Huyo demu anakudharau kwa sababu anajua kipato chako, ikibidi hata uwezo wako kichwani anaudharau na ukute anaambiwa na watu kibao kwamba ni mzuri, anapata kiburi ndo maana anakuzingua.

Uwe unampa muda na punguza kumwaza zaidi, waza kufanikiwa kimasomo na kimaisha, hii itakujengea heshima kwake na kwa wengine utakao wakuta kitaa.

Mtaani/makazini kuna wanawake wazuri sana, huyo asikuzuzue.

Asante mkuu darasan nipo vizur ila kutokana na hii hali najikuta nashindwa kusonga mbele na pia kuhusu kipato bado nawategemea wazaz wangu ambao wapo vzur japo sio saana na yote hayo anayafahamu na pia ni dem wangu wa pili na ninataman aje kuwa mke wangu.
 
Back
Top Bottom