Nifanye nini kumudu maumivu ya kushuhudia siku za mwisho za uhai wa mke wangu?

Habari zenu wakuu,!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii,ijapokua halii hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu. Ahsanteni
Pole sana Mkuu
Mkabidhi mkeo mikononi mwa Mungu,
Omba mapenzi ya Mungu yatimizwe..,Ni yapi!?sijui!.
Ndilo pekee lililobaki.

Mungu anajua yote.
 
Hakika usipopitia hivyo vipindi ni ngumu,kupata mguso wa ndani…ila kubwa Hakikisha mkeo,Amepata Neema ya kumjua Yesu kristo…Na ikitokea Yesu atamwita kwake…Atakuwa amempa uponyaji wa mwisho…Pole sana kaka
Nasi tunawaombea Neema Yake MUNGU iwashike katika hichi kipindi
 
Pole Sana mkuu. Sina uhakika hapo kwetu ila ulaya huwa kuna specialists wa Kutoa palliative care support check na hospitali kama tushajiongeza labda wanaweza kuwepo ukapata professional support .pia just be careful unapoleta sensitive issues humu maana kwenye Uzi wako wa Kwanza nahsi kuna mtu nilipambana nae maana humu wengi wanajitoa oblongata badara ya kukusupport unaweza ugulia maumivu juu ya maumivu
 
Habari zenu wakuu,!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii,ijapokua halii hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu. Ahsanteni
Mkuu nilikupa dawa umepuuzia, narudia teba hizi dawa nina uhakika nazo kwa asilimia 100, kuna mtu alishapona na dawa zangu akiwa kwenye stagge aliyopo mkeo. Jaribu kumpa, ale stafeli hata 5 kwa siku na majani yake yawe ndo maji ya kunywa lita 2 au zaidi kwa siku. Utaokoa maisha ya mkeo
 
Cha msingi ni kumwamini Yesu mkuu! Huyo ndiye faraja yako ambayo itakupa amani, na hata kama unaamini kuwa saratani haiponi ni mawazo yako tu yanakutuma hivyo, ila kwa Yesu hakuna kinachoshindikana, lakini uzuri ni kwamba akimwamini Yesu hata kama utampoteza ni wewe utahuzunika na familia yako lakini yeye atakuwa kwenye raha ambayo haielezeki, atakuwa na uzima ajapo ondoka dunia hii!! Kikubwa fuata huu ushauri
Acha ujinga
 
Habari zenu wakuu,!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii,ijapokua halii hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu. Ahsanteni
Pole sana mkuu, naijua vzr cancer ya matiti ilivyomteketeza dada yangu aise ni huzuni sana unashuhudia inavyomla Hadi dk ya mwisho kabisa. Mi nashauri kama wazazi wako wapo mpeleke huko kwanza ili machungu yapungue kwako wewe na kwa watoto
 
Pole sana kaka,

Endelea kumpa faraja mkeo, jitahidi uwe karibu nae muda mwingi.
Mkumbushe vitu, mambo mbali mbali, na nyakati za furaha mlizo share pamoja.
Hakika itawapa faraja kwamba kuna nyakati Mwenyezi Mungu aliwapa furaha pia.

Hali ya mgonjwa inakuwa na masononeko iwapo nawewe muuguzaji utapomuonyesha unakata tamaa. Jitahidi, hali inapokuwa ngumu, sali nae, omba nae dua, jipeni tumaini kwamba kwenye kila hali kuna kheri zake Mwenyezi Mungu.

Pole sana, na Mwenyezi Mungu azidi kukupa ujasiri.
 
Back
Top Bottom