Nifanye nini kumudu maumivu ya kushuhudia siku za mwisho za uhai wa mke wangu?

prospilla

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
1,111
1,637
Habari zenu wakuu!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii, ijapokua hali hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu.
Ahsanteni
 
Pole sana ndg, nafikiri sana itakuwa sahihi zaidi kama mtatumia muda mwingi kuwa karibu nae na kumfariji pia kuwa karibu na Mungu na kufanya ibada na sala kwa pamoja, pia muwashirikishe viongozi wa dini ili wakati atakapoondoka basi awe ameondoka kwa tumaini na amani hata wewe moyoni utakuwa na amani tele, maana atakuwa ameondoka akiwa ameyatengeneza mambo yake na Mungu,
Pole sana mkuu. Mungu akafanyike faraja kwenu
 
KITUO CHA PILI
Yesu anapokea msalaba

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.
- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Yesu anakubali kupokea msalaba kwa ajili ya wokovu wa watu. Ndivyo anavyonifundisha moyo wa sadaka, moyo wa kujitolea na kujisahau kwa ajili ya wengine.

Ee Yesu wangu mkarimu, mimi pia ninao msalaba wangu: jirani zangu, mwenzangu wa ndoa, watoto, wazazi wangu, kazi zangu, joto, baridi, njaa, kiu, vishawishi, magonjwa na matatizo mengine ya maisha, wajibu wangu kwa Mungu, kwa umma na kwa Kanisa.

Unipe ukarimu wako ee Yesu niyapokee bila kunung'unika, na kuyabeba vyema.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana utuhurumie W. Utuhurumie

Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.
 
Daahh inatia huzuni sana kiukweli ni kuwa nae karibu wakati wote angalau muombe pamoja n.k keep smile with her usilie nae akalia. Kiukweli uo ugonjwa kutoboa ukishafika stageb mbaya ni ngumu sana
 
Habari zenu wakuu,!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii,ijapokua halii hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu. Ahsanteni

0756901102 .
Pole mkuu.
Ni vigumu sana ila nakuomba ujikaze kwani wewe kama ndiye muuguzaji wake daima aspoona hofu ndani yako anakuwa na tumaini kubwa sana na hasa km mna watoto atahisi hata ikiwa huu ndio mwisho wake basi watoto wake wanabaki na mtu imara.

Najua kuficha ni ngumu lkn ukiwa karibu naye ficha hisia zako,mpe moyo na upendo ongeza sana,jaribu kujifunza kupokea hali yoyote na uhakikishe kuwa familia yenu haitayumba hasa watoto wenu.
 
Mtumainie Mungu tu, pata wakati wa kusali mara nyingi pamoja na mpendwa wako. Ni ngumu kibinadamu lakini katika Mungu utatiwa nguvu. Kuna mahali katika biblia pameandikwa kuna nyakati mbalimbali katika maisha ya mwanadamu...kuna wakati wa kulia na kuna wakati wa kucheka, kuna wakati wa uzima na wakati wa kuomboleza. Lakini katika nyakati zote anazopitia mwanadamu Mungu ni anabaki kuwa Mungu.

Mkuu umekuwa mume mwema sana maana umesimama kando ya mke wako katika nyakati zake nzuri na hata hizi ngumu. Mungu aonaye sirini akubariki.
 
Habari zenu wakuu,!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii,ijapokua halii hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu. Ahsanteni

0756901102 .
Pole sana ndugu yangu, Muombe Mungu akupe ujasiri, muonyeshe upendo wa kutosha mkeo, mtie moto, .Unajua Hali unayopitia . Hakika Cancer ni tishio sana.
 
Habari zenu wakuu,!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii,ijapokua halii hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu. Ahsanteni

0756901102 .
Pole sana kaka
 
Pole sana mkuu.Tumuombee Kwa Mungu

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Ita ndugu wa pande zote muweke kikao, kama mnasikilizana lakini; hasa wa upande wa mke ndio muhimu zaidi.
Wasiliana na vikundi vya maombi ili mfanye maombi pamoja na kuwaongezea ujasiri katika hali unayopitia.
Muondoe mgonjwa hofu na uumpe matumaini ya kupona.​
 
Back
Top Bottom