Chris wood
JF-Expert Member
- Dec 21, 2020
- 1,667
- 5,010
Msaada wa haraka unahitajika wakuu, Nifanyaje kuzuia hii hali. Hapa nilipopanga kuna Mwanamke nilimkuta anaishi.
First time nilijua labda ni mwanafunzi maana umri wake unachezea 18~19 , Ila baada ya muda nilikuja gundua anamtoto umri unachezea kama mwaka na miezi 8.
Shida ilipoanzia kuna siku nilikuwa nje nafua yeye alikuwa amekaa na yule mtoto wake, siunajua tabia za watoto kakaropoka huku kanatembea kuja kwangu baba baba baba.
Yaani toka siku hiyo imekuwa ndio wimbo baba baba. Nikiwa naondoka anamwambia mwambie baba akulete zawadi, nikirudi jioni anamwambia kampokee baba kanakuja kugonga mlango baba baba yaani.
Fedhea kubwa inapokuja kuna wapangaji wengine wapo sasa ile nikiwa narudi kile kitoto kinakuja baba baba yaani nashindwa hata nijibu nini naishia tu kujichekesha kinafiki.
Hapa nilikuwa nawaza nimwambie amkataze yule mtoto naona haiwezekani, Au nijiegeshe tu kuwa baba hewa. Nahitaji ushauri wandugu natanguliza shukrani.