Nifanyaje juu ya hili jambo?

Nyamayao

JF-Expert Member
Jan 22, 2009
6,966
2,352
Habari zenu nyote, naomba niwashirikishe kwa hili linalonisumbua kwasasa,

Nilishawahi kusema humu kuhusu Baba yangu, Sasa huyu mzee kwasasa tunaambiwa ni mgonjwa sana, anahitaji watu wa karibu wa kumuangalia na misaada mingine ya matibabu, kwasasa hatupigii sisi simu bali anamtumia dada yake (Shangazi) aongee na Mama kwahiyo habari zote tunazipata kwa mama.

Anatakiwa mtu aende Dar ama mgonjwa aende mji wowote kwa maangalizi ya karibu, nikisema mji wowote namaanisha kwamba huyu Baba ana wanawake/watoto miji tofauti tofauti, labda Arusha, Musoma kuna Mtoto wake wa kwanza mkubwa tu ambae nilishawahi kumuona, Dar hiyo ana watoto/wake , Mwanza pia, tatizo langu ni kwamba hakuna anaetaka jukumu hili, hata wale watoto wake aliowalea vizuri wakakua wakaanza maisha yao na miji yao nao wapo kimya, Wanawake aliozaa nao tunaambiwa wanaenda tu hapo nyumbani kumpikia na kuondoka, hana mtu wa karibu wa kumpa uwangalizi mzuri.

Hili limegeuka shida kwetu, kwamba sasa mimi na dada yangu ndio tuchukue hili jukumu, dada yangu hataki hata kusikia hii habari, mie walimwengu wananiambia nibebe hili jukumu mana kuna "laana" Mzee asije kufariki tukapata "laana" kwamba nisichukulie maamuzi ya dada yangu bali niwe na maamuzi yangu kukwepa "laana" Najiuliza hivi "laana" zinaachwaje jamani, kwamba sisi kunung'unika koteee kipindi hiko baadhi ya walimwengu wananiambia ndio laana imemfika, kwamba maisha yake yamekuwa jinsi yalivyo kwasasa, siamini hili mana na sisi tuliyaacha hayo na kusonga na maisha yetu.

Sasa basi kama dada yangu mzazi hataki hili jukumu kwamba alikuwa wapi wakati tukitaabika na mama yetu yeye akila raha zake sasa hivi aje atusumbue? wanawake aliozaa/kula nao raha wako wapi, watoto wake rundo wengine wapo wapi, kwanini sisi?

Dada ameshajitoa, hapa ni mie niamua kufanya maamuzi ya kubeba huu mzigo, ni kwamba nimlete huku nilipo ana nilimpekele Njoro kwa mama, huku mimi sitaweza, sina mtu wa kunisaidia katika hili jukumu, mana kama naambiwa anaumwa sana basi sitaweza kumfanyia yote, Msukuma wangu ni mtu wa masafari sana hataweza, bali kaniambia yupo nyuma ya maamuzi yangu yoyote kwa msaada wowote, kilichopo ni kumpeleka kwa mama, MMh hapo kwa mama sasa, ni kwamba ni mashamba/maeneo ya urithi, Babu alivyoona mama anateseka wakati huo huyu Mzee alivyomtelekeza akamkatia mama Kiamba aanze maisha,alianza mdogo mdogo mpaka tumekuwa tumepatengeneza ipasavyo ndio mji wa mama akiwa amezungukwa na ndugu zake, Huyu mzee anaendaje kuanza maisha ya pale? Mama anasema hawezi kwenda Dar kukaa kwa "watu" akimaanisha hiyo nyumba ya Mzee ina wenyewe (wanawake aliozaa nao). Kaka yake na mama (mjomba) anasema haya ni maisha yanaweza kutokea kwa kila mtu kama ninaweza kumleta kwa mama nifanye hivyo, hapa dada yangu ananilalamikia kwanini nataka kumsumbua/kumtesa mama kwa mambo ambayo hayamuhusu tena? kwanini nakazania mambo na kujifanya nina huruma sana wakati Mzee hakuwa na huruma yoyote kwetu? "nina kiherehere sana"

Na mie kwa upande wangu najiuliza kwanini mie? kwanini nibebe hili jukumu la Mzee ambae hakujali maisha yetu kabisaaa, hii laana ninayoambiwa isinipate mbona haitendi haki jamani? kama ndio hivyo kwahiyo hii laana naikwepa mie mwenyewe tu lakini kwa watoto/wanawake/aliekuwa mke wake zitawafikia? na kama zitawafikia mbona hawana hofu wala hawaonekani kujali? Kwanini mie baadhi ya ndugu/jamaa/marafiki wananiambia nijiepushe na hii laana?

Kwa aliewahi kuuguza anajua mambo yanavyokuwa, na hali ikiwa ndivyo sivyo inabidi mie ndio niwe mchezaji mzima wa hilo game. kwanini nijitie kitanzini jamani?

Naomba muwe wapole, hatuhukumiani hapa bali nataka kusikia tu na wenzangu mngekuwa kwenye situation kama yangu mngeitatuaje?

Asanteni sana.
 
ninavyoona mimi hapo suala la laana hapo halipo.....mzee hakutekeleza majukumu yake kama mzazi na ndo maana watoto wake wanaishia kumkimbia...upendo na huruma vimekosekana kwake kwa kuwa yeye hakuvionyesha kwa wake na watoto zake. isipokuwa wanasema Mzazi ni mzazi hata iweje............iwapo nafsi yako inaridhika na kumtunza baba yako bila kinyongo, kwanini usifanye hivyo.....amini usiamini hapo alipo baba nafsi inamsuta kwa aliyotenda, anajua alichokifanya si sahihi.
Dada yako ana hasira na ni haki kufeel kile anachokifeel, inauma sana....lkn ndo yashatokea haina jinsi. ongea na mama yako iwapo yuko radhi kubeba hilo jukumu, basi na iwe hvyo.....kumwacha mzazi wako anateseka na kudhalilika kwa makosa aliyotenda haimsaidii mtu yoyote zaidi ya yeye kuchekwa na walimwengu. usiangalie nani anasema nini au anafanya nini.....sema na moyo wako, tenda lile unaloona ni sahihi kwako.
 
Sijui nisemeje ndugu,mie bado nina kinyongo nae, bado sijaachia moyo kivilee.
 
King'asti, Kaunga, MwanajamiiOne,Preta,nyumba kubwa, Kongosho,The Boss, BAK, Asprin, Mbu, na wengineo hebu niambieni mwenzio nisipate "laana" mjue
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mdogo wangu,,, funga macho,,,,,yote alifanya but ni babako,,,msaidie kwa sehemu ya maisha yake iliyobaki....laana hapo haipo,,,,ila usitumie kigezo cha kutokuwepo laana ukaacha akaadhirika......na wala usimsaidie coz unaogopa laana...lah hasha inua moyo.....msaidie mzazi wako....
 
Kama una kinyongo unataka kufanya hayo kwa faida ya nani....Achilia hicho kinyongo na umsaidie mzazi wako.
Naomba nikuulize swali...hv kama anafariki mtaenda au mtasusia msiba??

Leo, nimeulizwa hili swali na dada yake Mzee, nimeshindwa kulijibu!
 
Sijui nisemeje ndugu,mie bado nina kinyongo nae, bado sijaachia moyo kivilee.

ndivyo inavyokuwa, ila kadri muda unavyozidi kwenda, utamuonea huruma na kumsamehe...mimi nakuelewa unachofeel, isipokuwa mara nyingi iwapo amri ya mungu itapita na akaondoka, nafsi yako itajilaumu sana, tena sana kwanini sikumsamehe na kumtendea wema...usiache ikafika huko. Na ninaamini mzazi wako iko siku atakuomba msamaha na kinyongo ulichonacho kitaondoka.
 
Mdogo wangu,,, funga macho,,,,,yote alifanya but ni babako,,,msaidie kwa sehemu ya maisha yake iliyobaki....laana hapo haipo,,,,ila usitumie kigezo cha kutokuwepo laana ukaacha akaadhirika......na wala usimsaidie coz unaogopa laana...lah hasha inua moyo.....msaidie mzazi wako....

Kuuguza kuna mengi, nafikiria pia mambo yakienda ndivyo sivyo nafanyaje? na hili swali ujue haliuliziki kwasasa kabisa.
 
ndivyo inavyokuwa, ila kadri muda unavyozidi kwenda, utamuonea huruma na kumsamehe...mimi nakuelewa unachofeel, isipokuwa mara nyingi iwapo amri ya mungu itapita na akaondoka, nafsi yako itajilaumu sana, tena sana kwanini sikumsamehe na kumtendea wema...usiache ikafika huko. Na ninaamini mzazi wako iko siku atakuomba msamaha na kinyongo ulichonacho kitaondoka.

Alishajaribu hili kwa namna fulani, lakini nikashindwa kumwelewa, akajaribu nimpelekee wajukuu akawaone sikumuelewa pia.
 
Nimesoma tu nusu, nakomenti kabla ya kumalizia. Kama nilivyokuambia awali, una connection na baba yako, nahisi unamjali ila maumivu hayajakwisha. Ni kama unatamani utoe ya moyoni kabla hujasonga mbele.

Kwa kuwa wewe ndie unayejali na kuumia, fanya kitu si kwa ajili ya baba yako, fanya kitu kwa ajili yako ili upate amani. Jambo hili litakuwa linakurudia kila mara hadi lini?

Sio kila mara unasamehe sababu umeombwa msamaha, sometimes unasamehe sababu chuki si sehemu ya maisha yako, afterall ni baba yako.

I feel you, hadi machozi ujue.
 
Nyamayao kama umeamua na unaona unaweza kumsaidia mzee katika kipindi hiki ambacho ni mgonjwa fanya lile ambalo moyo wako unakubaliana nalo na una support kutoka kwa msukuma wako pia
Kama ni kujuta mzee ashajuta sana na hapo alipo huenda anajilaumu kwa matendo aliyoyafanya ni vile tuu kurudi na kuwaaambia nisameheni inakuwa ngumu kwake (mfumo dume)
Kama umeamua msaidie na usijiulize maswali mengi sana maana litakapotokea la kutokea hautakuwa peke yako kwenye maamuzi bali mtakuwa wote kwenye kuamua ni wapi mtafanya hilo la kufanya
Na utakapoenda kumchukua naamini utawajulisha pia wale wanaokaa nae kuwa ni kwa ajili ya matibabu tuu mambo mengine mtajadiliana kama familia
Ondoa kinyongo na sio suala kuwa unaogopa laana ila kwa kuwa una damu yake inayotembea ndani ya mishipa yako na regardless ya mengi mabaya aliyokutendea na kuwatendea bado ni mzazi wako tuu
 
Last edited by a moderator:
Kuuguza kuna mengi, nafikiria pia mambo yakienda ndivyo sivyo nafanyaje? na hili swali ujue haliuliziki kwasasa kabisa.

wengi wetu tushauguza wazazi wetu,,,,hilo lisikuumize,,, hivi akirest in pis mtasusa? fanya kama wewe,,, usiangalie ndugu waliokuzunguka......inuka ukatende wema kwa babako.....
 
Pole sana mpenzi.
Mimi nakushauri, mtunze kama uwezo unaruhusu mchukue kwako na mtafute mama mtu mzima wa kumuhudumia umlipe. Hii unaifanya si kwa kuogopa laana, bali ni for God's sake. Maana maandiko yanatuambia tuwaheshimu baba na mama ili tupate miaka yenye heri duniani. Kumbuka Mfano wa Yesu juu ya kumpenda jirani (msamaria mwema); so fanya hivyo just for salvation of your soul na utakuja simulia jinsi Mungu atakavyokulipia.

Inauma na ni ngumu lkn najua kwa msaada wa Mungu utaweza. Who knows, huenda baba angewaspoil leo hii ungekuaje. Huenda usingekuwa na mafanikio yoyote, Mungu anaruhusu mambo magumu yatupate sometimes ili kutuandaa na responsibity kubwa baadaye, au kutuweka karibu naye au kutuepushia mabaya zaidi mbeleni.

Msamehe maana nawe wahitaji msamaha, na kumbuka sala ya bwana. Ili tusamehewe twahitaji kusamehe kwanza. Msamehe makubwa aliyoyafanya ili baba wa mbinguni naye akusamehe makubwa uliyo/utakayoyafanya.

Mungu akutie nguvu na hekima. Amina
 
Kama ungekuwa bado umemkasirikia kihivyo, wala usingekuwa unajali.

Kila mtu kaumbwa ki vyake, kama watoto wake wengine hawamtaki, inaelekea wewe unamtaka. Labda ndio chance ya ninyi kufahamiana, labda ndio chance ya ninyi kusameheana, labda Mungu anajua tamanio lako ameamua akupe fursa ya kuweka mambo sawa?

Kama bado yuko hai unahangaika hivi, una nafasi ya kupatana naye unahangaika hivi, imagine hayupo na huwezi patana naye, naona utateseka zaidi.

Piga moyo konde ukamtunze, kwa ajili yako na amani yako.

Alishajaribu hili kwa namna fulani, lakini nikashindwa kumwelewa, akajaribu nimpelekee wajukuu akawaone sikumuelewa pia.
 
Nimesoma tu nusu, nakomenti kabla ya kumalizia. Kama nilivyokuambia awali, una connection na baba yako, nahisi unamjali ila maumivu hayajakwisha. Ni kama unatamani utoe ya moyoni kabla hujasonga mbele.

Kwa kuwa wewe ndie unayejali na kuumia, fanya kitu si kwa ajili ya baba yako, fanya kitu kwa ajili yako ili upate amani. Jambo hili litakuwa linakurudia kila mara hadi lini?

Sio kila mara unasamehe sababu umeombwa msamaha, sometimes unasamehe sababu chuki si sehemu ya maisha yako, afterall ni baba yako.

I feel you, hadi machozi ujue.

Kongosho, kwa hili limeniumiza kuliko mengine niliyowaza juu ya huyu Mzee, kwamba ni kama "nimesusiwa" ila natamani kusaidia, ingekuwa ni msaada wakifedha tu nisingekuwa na shida, hapa hana mtu wa kumuangalia kwa karibu,huku kwangu atateseka tu, kwa mama, dada ndio ananiambia namsumbulia/mtesa mama yake kwa mambo yaliyopitaga na kujifanya nina huruma sana.
 
Nimesoma tu nusu, nakomenti kabla ya kumalizia. Kama nilivyokuambia awali, una connection na baba yako, nahisi unamjali ila maumivu hayajakwisha. Ni kama unatamani utoe ya moyoni kabla hujasonga mbele.

Kwa kuwa wewe ndie unayejali na kuumia, fanya kitu si kwa ajili ya baba yako, fanya kitu kwa ajili yako ili upate amani. Jambo hili litakuwa linakurudia kila mara hadi lini?

Sio kila mara unasamehe sababu umeombwa msamaha, sometimes unasamehe sababu chuki si sehemu ya maisha yako, afterall ni baba yako.

I feel you, hadi machozi ujue.
Well said, nami nimenote roho ya huruma aliyonayo ingawa anatamani angekuwa na moyo mgumu kama wale waliokataa.

She should take care of her dad for God's sake. Itamsaidia sana.
 
Back
Top Bottom