Sijui nisemeje ndugu,mie bado nina kinyongo nae, bado sijaachia moyo kivilee.
Nyama yao nimeelewa situation muliyonayo!
Ngoja nitiririke hivi:
Baba yenu si mtu mzuri! Alichokifanya yastahili yamkute yanayomkuta sasa!
Nadhani ile principle ya karma inafanya kazi yake!
Ule msemo "fainali uzeeni" ndio unafanya kazi!
Ningependa utoe wasi wasi kwamba kitendo cha kumuabonden huyo mzee hakuna laana itakayokukuta!
Walatin walisema 'Volenti non fit injuria!' waswahili wakatafsiri 'kusudi haiambiwi pole!'
Laana anatoa Mungu ikiwa nawe unaamini nguvu na uwepo wake (Mungu) Laana hutolewa kwa kulipa mabaya pale ulipokopeshwa mema!
Hiyo ni wazi kwamba hakuna laana itakayokukuta kwa kutompokea baba yako!
Huo ni upande mmoja! Na ufuatao ni upande wa pili:
Waswahili walisema "mama ni mama hata kama ni rikwama/mkokoteni" Ikimaanisha, hata awe chizi, muhuni, malaya, katili nk, bado atabaki kuwa mama kwa wewe aliekuzaa! Hiyo inamaana ya kwamba WAJIBU WAKO KWA MAMA UTABAKI PALE PALE!
Ningependa usikariri! Neno mama hapo halijawa limited kumuexclude baba! kwa lugha nyepesi neno 'mama' lina maana ya 'mzazi'
Kwa mantiki hiyo, wajibu wako kwa mzazi (baba yako) bado uko pale pale!
Ukiamua kutomsaidia baba yako mzazi
ni sawa kutokana na aliyoyafanya! Kuna mtaalamu alisema wajibu huendana na haki, haki yako ikivunjwa wajibu huna!
But itakuwa
sawa zaidi pale utakapoamua kumsaidia baba yako! Ukumbuke! Ile principle ya karma haitaishia kwa baba yako tu!
Siku zote ishi wewe kama wewe! Kitendo cha dada yako kukataa kumsaidia mzee isiwe sababu ya wewe kufata uamuzi wake!
imeandikwa kila mtu atabeba mzigo wake!
Kitendo cha wewe kumsaidia baba yako licha ya mabaya aliyokufanyia (aliyowafanyia) ni kupata baraka za Mungu (kama unamuamini) na ni njia moja wapo ya kukuza nguvu zako za asili (psychic power) alizokujalia Muumba wako! For sure psychic power hufunguka kwa upendo na huruma! Embu zingatia hilo! Au haujui faida za psychic power?
Vile vile ukimsaidia baba yako licha ya mambo aliyowafanyia, hufanyi hivyo bure! Kuna malipo mazuri kwa Muumba wako!
Laiti ungetambua psychological disorder anayosuffer baba yako kwa sasa, hata usingeanzisha huu uzi instead ungemruhusu mzee wako kuja ktk himaya yako!
...
Ni vipi utamsaidia mzee wakati mmeo ni mtu wa kusafiri na wewe ni mtu wa mihangaiko?
Kwanza mshukuru Mungu kwa kukupatia mme bora na mwenye upendo! Kitendo cha mmeo kukuahidi atakuwa nawe bega kwa bega kutokana na janga linalokukabili, unapaswa uitumie vyema hiyo chance kwa kumuhudumia baba yako as if hakuna ubaya wowote aliyokutendea!
Jaribu hata kuajiri mtu ili akusaidie kumhandle mzee!
Usiache neema ya kumuhudumia mzee ikupotee hivi hivi! Yule ni baba yako!
...
I hope umenielewa na nakutakia kila la heri na Mungu akusaidie!