Nifanyaje juu ya hili jambo?

Nifanyaje juu ya hili jambo?

Mzazi ni mzazi tu,mshawishi mama naimani atakubali thn msaidie baba ako,wa kuhukumu ni mungu pekee,binadamu uwezo huo hatuna,fanya vile nafsi inavyokutuma!all the best mpnz!
 
hayo mateso Mugu keshampa hapa hapa duniani tayari na meshajuta, we msidie tu sbb ni mzazi wako..mzazi halipiziwi kisasi my dear..we msaidie tu na utashangaa Mungu atakavyokubariki maisha yako hapo baadae...funga macho beba mzigo japo mzito

Hiki (kwa red) ndo nilichotaka kuongezea kumtia moyo Nyamayao, thanks umekisema tayari, play your part Nyamayao, huyo ndo baba yako hakuna mwingine
 
Last edited by a moderator:
Wema si kitu rahisi hasa kumtendea wema asiyestahili.
Huyo ni mwanadamu aliyekosea, wewe na mimi tunaweza kukosea vilevile.
Mara nyingine tumewasamehe hata tusiokuwa na vinasaba hata kidogo kwa nini ushindwe hapa.
Pamoja na kwamba pengine ikawa ni wakati wake wakujuta, huu ni wakati wenu wakutenda msije juta kama yeye baadaye.
Huyo ni zaidi ya omba omba unaye mdondoshea shilingi ukipita.
Kama muamini, utakubaliana Mungu amekuletea mengi ya kukupima umeyashinda. Hili nalo jifunge kibwebwe ushinde.
Namjua mama aliyewahi kumsamehe na kuishi naye muuaji wa familia yake.
Nakuombea Mungu akupe ujasiri, unapokubali kupokea baraka hizi. Unaweza usipate laana usipomhudumia ila ukweli utakosa baraka ukimwacha ateseke peke yake. Binadamu wote hata wenye roho mbaya, wakati wa shida zetu tunatamani awepo wa kutujali, Jitolee kwa ajili ya baba yako.
 
kinyongo hakifai.. sio kitu kizuri, usilipize mabaya kwa mabaya... hata ukifanya nini wont change the fact that ni baba yako. mlee vile uwezavyo,samehe n let God be the judge not u! kwani wewe umetenda mema through out ur life? hujawahi kosea? why judging him that much? give him the love from deep inside n God will reward u handsomely ukashangaa! ur grown up usianze kuuliza fulani mbona hafanyi n why me not that one?? do your part asiyefanya ni yeye ameamua kutofanya!
nimeshawahi kupatwa na the same situation although sii exactly lakinu sijawahi juta kutoa msaada maana nabarikiwa kila iitwapo leo... DO IT WITH ALL YOUR HEART
 
Sijui nisemeje ndugu,mie bado nina kinyongo nae, bado sijaachia moyo kivilee.

Ikitokea huyo mzee akafariki atakuacha na kinyongo chako, ambapo hutakitoa maisha yako yote, biblia inasema usiache jua lichwee likuache na hasira moyoni, ningekuwa mimi ningemchukua huyo mzee na kumpeleka kwa mama na kumtibisha na kumhudumia lkn ningemwambia kile kilichoujaza moyo wangu ili niwe huru, naamini hata yeye anatamani kusema nanyi ili mumsamehe
 
Naweza ku"feel the real sincerity" iliyopo kwenye uzi huu. Kwanza nitangulize pole zangu na kumtakia afya njema baba yako.
Usahauri wangu ni kuwa usilipe ubaya kwa ubaya hasa katika hali aliyonayo baba yako. Ingawaje aliwatesa sana alipokuwa na nguvu na kukubali kutekwa na dunia na kuwatelekeza ninyi na mama yenu kipindi mlipokuwa mnamuhijati sana lakini hili haliwezi kuwafanya msimsamehe. Msiweke kinyongo kisichoisha, ni dhambi mtavuna kama mnamwamini Mungu (hata kama mnasema si laana lakini dhambi ya kumwekea baba yenu kinyongo itawanyima raha pindi atakapoaga kama hamtamsaidia). Kwa sasa nguvu zimemwishia, dunia imemtenga, hana pa kuegemea. Matumaini yake yote yapo kwenu ninyi watoto, japo najua anaogopa kuwaomba msaada kwa kuwa anajua hastahili kutokana na kuwatelekeza hapo awali. Ndiyo, alikosea kama binadamau na ni vizuri mkamsamehe na kumsadia wakati huu amabpo anaumwa.

Kutokana na ulivyoeleza, nakushauri nenda mshawishi mama yako akubali kumsamehe mumewe, na akubali kumtunza hapo nyumbani ambapo mama anapenda kuishi. Mshirikishe pia baba, akikubali kamlete baba hapo nyumbani na saidianeni na mama katika kumtunza siku hizi za uzee na ugonjwa wake. Mtabarikiwa. Hata kama Mungu atamchukua mtabaki na amani maishani na mwenu. Ukishamleta endelea kumshawishi dada yako na ndugu wengine pia washiriki/wachangie kumtunza, naamini nafsi zao zitawasuta na watasaidia kumtunza baada ya kuona jitihada zako. Nawatakia kila la kheri katika kumuuguza.
 
Wakati mwingine inafaa kuwapenda SANA waliotuumiza SANA!
Tukiwapenda wanaotutenda mazuri twafanya sadaka gani?
-msamaha ni kwa ajili yetu wala si kwa ajili ya waliotukosea,!
Sweetheart ,baba ameshaumia vya kutosha!anayoyabeba sasa plus maumivu ya kuumwa yanatosha.hakuna kitu kibaya kama kukataliwa na familia!
Kutamani kuuguzwa na kutafuta suluhisho nanyi I tayari ni kujikana kwa kiasi kikibwa sana!msizidi kumsonta huyo babu wa watu!
Ikiwa kumpa amani ya kuungana na familia aliyoitelekeza ndilo pekee analoomba kwa Muumba wake kabla hajarudi mavumbini,hakika msimnyime fadhili hiyo.
Narudia tena
Tukiwapenda watupendao twafanya sadaka gani?
 
Pagumu hapa Nyamayao, lakini msikilize sana dada yako na mama yako wote mfanye uamuzi wa pamoja, usithubutu kufanya uamuzi wa pekee yako bila kuwashirikisha. Kwa maoni yangu hapa hakuna laana, kutakuwaje na laana wakati yeye hakuwajali akawakimbia katika kipindi ambacho mlihitaji sana uwepo wake kama Baba/Mume!?

Kinachonistaajabisha ni kuona watoto aliowalea na kuwatunza vizuri nao wamemtelekeza. Ungekuwa na nafasi ya kumchukua kwako basi ningekushauri ufanye hivyo. Pole sana naona hili linakutafuna sana lakini huna kosa lolote lile na wala usijiumize kwa mawazo.

King'asti, Kaunga, MwanajamiiOne,Preta,nyumba kubwa, Kongosho,The Boss, BAK, Asprin, Mbu, na wengineo hebu niambieni mwenzio nisipate "laana" mjue
 
Last edited by a moderator:
kusamehe ni ubinadamu pamoja na yote hayo huyo ni baba yako do what is best for him hata km alikukosea ni yeye, baya hulipizwa na jema maana likilpzwa baya kwa baya bac chuk,visasi,hasira havitaisha kamwe, kumbuka ur party of him
 
msaidie kama roho yako inataka ivo ila usimsaidie kwasababu ya kuogopa laana.
Acha kusikiliza ya watu, your papa need you now.
 
Pagumu hapa Nyamayao, lakini msikilize sana dada yako na mama yako wote mfanye uamuzi wa pamoja, usithubutu kufanya uamuzi wa pekee yako bila kuwashirikisha. Kwa maoni yangu hapa hakuna laana, kutakuwaje na laana wakati yeye hakuwajali akawakimbia katika kipindi ambacho mlihitaji sana uwepo wake kama Baba/Mume!?

Kinachonistaajabisha ni kuona watoto aliowalea na kuwatunza vizuri nao wamemtelekeza. Ungekuwa na nafasi ya kumchukua kwako basi ningekushauri ufanye hivyo. Pole sana naona hili linakutafuna sana lakini huna kosa lolote lile na wala usijiumize kwa mawazo.

Hapo na mie ndio panaponishangaza, jana niliongea na dada yake mzee nikamuuliza hilo, akaniambia kila mtoto anakimbizana kumtengenezea maisha mama yake, kuna wanaomjengea mama yao mbweni huko nao wanasema hawana hela wapo kwenye ujenzi, wa mwanza huyo ndio wa kiume mkubwa ambae angeweza kupambana kwenye uuguzi ipasavyo nae kimya ni mama yake tu anaenda hapo kupika na mwanae nae anasema hana hela biashara zake hazipo vizuri kwasasa, jana hicho chakula nilichoambiwa amepikiwa nilichoka kabisaaaaa nikajuta kuuliza.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kama ni mimi ningekuwa namtumia hela ahudumiwe tu huko huko. nafikiri hata mungu angeona kama nimemsaidia mzee.
 
Kuna wakati hela si suluhisho. Hivi unakumbuka hata kwenye movie wakikasirika wanatukananaje? 'You will die alone'

Hakuna kitu kibaya kama kufa peke yako wakati familia yako haipo, mgonjwa anahitaji upendo, tane kama huyu anahitaji kujisamehe na kusamehewa. Hata kama akitangulia mbele, aende kwa amani.

Mtu baki, may be? Mzazi? Hapana kwa kweli.

Kuna wakati unaoga ugumu kumsaidia mtu sababu ya ugumu wa maisha unaokusonga. Mtu yule akifa, halafu na wewe ukawa umesha move step ahead, nafsi huwa inakosa raha kabisa ukikumbuka ulishindwa msaidia kitu kidogo kama kile. Usumbufu/gharama huwa ni vitu vya muda na hubadilika sometimes.

kama ni mimi ningekuwa namtumia hela ahudumiwe tu huko huko. nafikiri hata mungu angeona kama nimemsaidia mzee.
 
Kama mama yako hajariudhia umpeleke hapo akamuudumie wala usijaribu kumuumiza tena maana amesahumia mwanzo na asiumie tena, kama unaweza kusaidia wewe kama wewe ni vizuri zaidi ila huruma yako isiwe kikwazo kwa watu unaowapenda. Mama akikubali well and good. lakini usimlazimishe mama yako abebe mzigo asioutaka
 
Pole sana, please keep us up to date with your final decision.

Hapo na mie ndio panaponishangaza, jana niliongea na dada yake mzee nikamuuliza hilo, akaniambia kila mtoto anakimbizana kumtengenezea maisha mama yake, kuna wanaomjengea mama yao mbweni huko nao wanasema hawana hela wapo kwenye ujenzi, wa mwanza huyo ndio wa kiume mkubwa ambae angeweza kupambana kwenye uuguzi ipasavyo nae kimya ni mama yake tu anaenda hapo kupika na mwanae nae anasema hana hela biashara zake hazipo vizuri kwasasa, jana hicho chakula nilichoambiwa amepikiwa nilichoka kabisaaaaa nikajuta kuuliza.
 
Kuna wakati hela si suluhisho. Hivi unakumbuka hata kwenye movie wakikasirika wanatukananaje? 'You will die alone'

Hakuna kitu kibaya kama kufa peke yako wakati familia yako haipo, mgonjwa anahitaji upendo, tane kama huyu anahitaji kujisamehe na kusamehewa. Hata kama akitangulia mbele, aende kwa amani.

Mtu baki, may be? Mzazi? Hapana kwa kweli.

Kuna wakati unaoga ugumu kumsaidia mtu sababu ya ugumu wa maisha unaokusonga. Mtu yule akifa, halafu na wewe ukawa umesha move step ahead, nafsi huwa inakosa raha kabisa ukikumbuka ulishindwa msaidia kitu kidogo kama kile. Usumbufu/gharama huwa ni vitu vya muda na hubadilika sometimes.

naamini Nyamayao ameshamsamehe mzaz wake na ndo maana anawaza kumsaidia. kwani ukimsamehe mtu lazma uwe nae karibu? kumbuka katika hili huyo bibie atakuwa peke yake. ni bora amsaidie huyo mzee kibluetooth lakn kumpeleka kwake au kwa mama yake sioni kama ni option nzuri.
BTW, kuitwa mzazi ni kubeba majukumu yote ya malezi. watu huwa wanasema "amemlea kama mwanae wa kumzaa". hiyo ni sababu wanajua kuwa mzazi ni kutoa malezi, yaani ni zaidi ya ile sperm moja.
 
Last edited by a moderator:
Fanya kile ambacho kitafanya nafsi yako iwe huru. ambacho naamini ni kumuuguza baba yako.
 
Back
Top Bottom