Nifanyaje juu ya hili jambo?

Nifanyaje juu ya hili jambo?

Although he has never been a good father to you lkn he is still your dad. Isingekua yy hata jamii forums tusingekuona humu. Please take the responsibility.
Be strong n do th needful.
 
Japo umechagua washauri naomba usome hapa kutoka 20:13-15
Mpe tiba mzazi wako nalo ni fundisho kubwa kwake
Mtibu kwa upendo bila kinyongo akipona mrudishe kwake.
Hutapata laana yeyote bali utapata baraka kubwa sana kwa Mungu wako.
Hesabu unampa msaada kama mtu mwingine ili usipate uchungu ule uliopata mamayako akiteswa kipindi hicho
 
Kwanza pole kwa kuuguliwa na pole kwa mkanganyiko unaoendelea ktk familia yako. Hata mimi nikiwa sekondari niliwahi kujiambia kuwa nikshafanikiwa katika maisha kamwe baba asinitafute na sitokua tayari kumsaidia kwa hali yeyote. Lakini nadhani angekuepo leo ningemsaidia kwa kuwa nilijifunza kusamehe japokua Mungu alishampenda kwa sasa.
Ninakushauri kama mama yako yuko tayari kumhudumia na mumeo ameridhia basi jaribu kukaa na mama mumsihi dada pia asahau yaliyopita na mumsaidie huyo mzee. Nasema hivi kwa kuwa huezi jua ni kwa nini haya yanatokea na moyo wako kwa kiasi flani unakusukuma umsaidie, alafu huyo ndiye baba yako hata iweje ukweli utabaki hivyo tu.
Alafu unasema hujamuachilia kabisa kwa aliyotenda. Akifariki hukumsaidia huoni unaweza kuwa guilty zaidi utaishi maisha gani dhamira inakusuta? Yeye alichagua kutokuwasaidia tena ikiwa ni wajibu wake na Mungu amewapigania mmefanikiwa mwache akajibu sehemu yake ila we fanya yako . Achana na style ya maisha aliyoyachagua zamani ambayo utakapomsaidia dhamira yake kumsuta ni adhabu tosha kwa kuwa anajua alichowafanyia. So please msimuadhibu kwa mara nyingine imetosha. Jiulize kama Mungu akihesabu makosa utakua wapi then fuata moyo wako. Ila nakusihi usimuache kaeni nyie watatu msaidiane.
 
Huyo ni mama yako pia, na kama mama yuko radhi kumlea mume wake sioni kama kuna suala la kumsikiliza dada yako ambaye kimsingi naona ni mtu ambaye hana huruma. Hata kama aliwatenda atabaki kuwa ni baba yako na siku asipokuwepo katika dunia hii utasema umeondokewa na baba. Moyo wako unakuambia utende hicho unachotakiwa kukitenda na hii nadhani ni roho ya Mungu ndiyo inayokusukuma na ni tegemeo langu kamba lipo lililojema nyuma ya jambo hili. Ni vipi akutake umpelekee watoto wako wakamuone na si watoto wa ndugu zako wengine. Huwezi hata kufikiria juu ya hilo? Nenda kamchukue baba yako umuhudumie katika wakati huu mgumu alionao na lipo la baraka ambalo utalipata kutoka kwake. Sikiliza kiu ya moyo wako ya kumsaidia baba yako. KUpona na ama kutokupona kwake ni la mungu na si lako. MSAIDIE BABA YAKO KWA HILO NAWE UTABARIKIAWA SANA.
 
Back
Top Bottom