1.
- Mkuu ni wajibu wangu kujibu au kutokujibu anything, wazazi wangu hawahusiki na wewe kutawaliwa na CCM for the last 47 years, na the fact kwamba uko about kutawaliwa tena for the next 5 years na CCm ile ile.
- Siwezi kuwatukana wazazi wako kwa sababu kwanza siwajui na hawajulikani kwamba wamewahi kulifanyia lolote taifa, kwamba eti utanitisha nisitoe maoni yangu kwa kukimbilia wazazi wangu, unapoteza muda wako bure nitanedlea kama kawaida kutoa maoni yangu tena mbadala, bila ya kuburuzwa kama treni kwa sababu amesema nani hapana hiyo ndi inaitwa utummwa wa akili, tunaukataa kutoka wka CCM sasa tusiukubali kutoka humu ndani ya JF.
2.
- Tatiio hapa sio kusikiliza, tatizo ni kufikiri for our own na kusema wazi bila kuogopa tunayofikiria, tumeburuzwa na Mwalimu weee na sasa kuna Waalimu wengine wako pembeni kama wewe wanaosubiri tuzubae waanza yale yale ya kulazimishana, siwezi kusikiliza defeated ideas, kwamba eti njia ya kujikomboa na makucha ya CCM ni kuwatukana baadhi ya wana-CCM kwa sababu ya mawazo yao wewe sikiliza hayo, mimi simo hata siku moja kwenye hayo, Malecela, na wazee wa wastaafu wanne wa CCM hawawezi kutuamulia wananchi millioni 40 nani awe rais wetu, na wakiweza then something is very wrong na sisi wananchi wote wa Tanzania na hasa sisi JF included.
3.
- Kudai umelazimishwa ni dalili za unyonge ulionao tayari kwamba mtu ndani ya CCM aksiema basi wewe unajihisi unalazimishwa, huo ni unyonge wa mawazo ndio maana hata akiandika mtu hapa huwezi ku-question kwa sababu umezoea unyonge wa kutouliza bali kukubali tu na kulaumu wazazi wa wasiokubaliana na mawazo yako, hapana mkuu CCM wape heshima kwa sababu huwawezi na huna njia kama unavyokubali mwenyewe, hakuna kiongozi wa CCM aliyelazimisha kupigiwa kura wala anything, ni mawazo yako ya kinyonge ndio yanakufanya ushindwe kuwa na alternative ya CCM, sasa unataka kutulazimisha wote tuwe kama wewe, hatuwezi mkuu hii ni bongo huru, CCM ni washindi hands down, tizama walivyobadili agenda ghafla baada ya kua kimya kwa muda mrefu sana, wakowapi Upinzani? Almost five weeks sasa tunaongelea CCM tu, hivyo ndivyo vyama vyenye kujua siasa vinavyafanya na sasa wote tunacheza mikononi mwao, siasa ni kipaji mkuu sio kuandika vizuri au kwua na elimu sana, siasa ni siasa ni an art unahitaji kipaji cha siasa kuelewa kinchoendelea bongo sasa hivi, ni kwamba CCM sasa wameweka agenda, viongozi wa upinzani wengi wako majimboni kutafuta ubunge, maana yake tumeshindwa!
4.
- Ni wewe unayeparamia sana wazazi wangu, ambao sio marais wa Tanzania, ambao wamekufikisha hapo ulipo, mimi siwezi kua na hasira na mtu nisiyemjua wala kuwajua wazazi wake, CCM wametushinda mkuu sasa unaweza kunitukana na mimi na wazazi wangu kwa sababu hiyo sina tatizo kukubali kama ulivyoanza tayari, ila ninakuhakikishia kua haitabadili anything, maana tumeshidnwa tayari.
Na sasa mpaka uchaguzi uuishe tutaongea agenda zinazowekwa na CCM tu, maana they are good at what they stand for kushinda uchaguzi na kwa mawazo haya watashinda mpaka wmisho wa dunia yetu, hatimaye nimeelewa kwa nini Mwalimu alituburuza sana wabongo, ukweli ni kwamba hatuna idea ya siasa, tunafikiri siasa ni lelemama, mkuu nitukane as much as you want na wazazi wangu pia huenda ikakusaidia kubadili mwelekeo wa taifa.
Ahsante.
William.