Recta,
Mkuu Mkandara, heshima kwako. Mkuu, kinachosumbua sio chaguo la kimaoni linalotolewa na "VIONGOZI" wanaojitokeza na kupendekeza kwa kusema hadharani kuwa Kikwete atagombea kuwa Rais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2010. SIo hilo hata kidogo. Tatizo ni pale wanapokwenda mbele zaidi na kutishia kuwa asijitokeze mwingine wa kumpinga JK katika uchaguzi huo. Mkuu hilo ndilo tatizo.
Kauli ya kupendekeza ni maoni halali kabisa. Kauli za kuhitimisha hoja ambayo mtu hana mamlaka ya kuhitimisha ni kosa. VIONGOZI hao waliojitokeza kusema hadharani kuwa hakuna anaetakiwa kumpinga JK 2010 kwa kuzingatia utamaduni uliopo ndani ya chama wanakosea wanapofanya hivyo. Wanakosea kwasababu tu, wanataka wengine wasio na nguvu kama walizonazo wao waogope kupingana na maamuzi yao (si maoni yao). Maamuzi ya kuwa JK ndie atakaegombea peke yake.
Mkuu wangu hapo nilipoweka bold kwa rangi nyekundu ndipo napozungumzia mimi..Nasema hakuna kosa kabisa..sino kosa kwa sababu watu hawa - HAWANA MAMLAKA YA KUHITIMISHA..hivyo kilichosemwa bado ni Mapendekezo nitahofia tu mtu mwenye mamlaka..
Siku zote sisi wananchi tutaogopa mtu mwenye Mamlaka ya kuhitimisha anapotunga sheria ama kupitisha Utaratibu kwa wananchi wote lakini kusema tu wanasema wengi na ndizo siasa zetu..
CCM imejengwa ndani ya Ujamaa wa Kiafrika na chama hicho kina mambo mengi sana yanayoendeshwa kwa Udikteta kutokana na urithi wa nyayo za mwalimu zinazosisitiza heshima ni pamoja na kuogopa wakubwa zako..hivyo mabadiliko yoyote ndani ya chama yanatakiwa kwenda kwa hatua..Binafsi sioni kosa kabisa ktk kumpendekeza Kikwete na hata mikwara inayotolewa ikiwa kuna usiri fulani pembeni kumwangusha Kikwete ktk uchaguzi wa ndani CCM..Ni mbinu za kisiasa ktk mfumo wa Kijamaa kuwekeana mikwara..
Kwa nini wanaompinga Kikwete wasijitokeze hadharani? kwa nini wamejichimbia wakiendesha kampeni zao kichini chini wakati sisi wananchi tunataka sana kuona Upinzani kwa Kikwete ukiwa wazi nhasa ktk maswala ambayo sisi tunapenda kuona mabadiliko!.
Mkuu wangu Lisemwalo Lipo na kama halipo linakuja.. hawa wazee sio tu wameibuka toka usingizini wakaanza kusema hayo bila kuwepo dalili za vurugu ndani ya chama..
Nina hakika wazee hawa wasingefikia maneno haya kama Mwandosya, Lowassa au Asha Rose Migiro wangesimama na kusema wanatarajia kugombea kiti cha urais dhidi ya Kikwete.. hapo tungeona fair game, lakini yamepita majungu tu nyuma nyuma kiasi kwamba hata mimi hapa Mkandara naaza kuzipata data za Mapinduzi haya baridi..
Kumbukeni Mwanakijiji, FMES na wengine wengi tu wamekuwa wakitutaarifu kuhusu vikao na mikutano ya siri kumwondoa Kikwete au kuchukua majimbo fulani ya utawala kama vile utawala wa nchi hii umekuwa mnadani..Hii mikutano ilianza lini kama mnakumbuka na leo tunaanza kuona dalili zake bado tunashindwa kuamini kinachoendelea... hali ambayo sii mbaya tu kwa Kikwete isipokuwa inahatarisha Usalama wa nchi yetu..
Upinzani wa Kikwete na vyama vya Upinzani unaeleweka na ni wazi lakini Upinzani ulipo ndani ya CCM unatisha, ni kinyume cha katiba na wala na sitaomba hata siku moja mgombea wa CCM atokane na ushirika wa Mafisadi..
My biggest lesson ni uchaguzi wa Kikwete mwenyewe mwaka 2005. Nimeona jinsi Mafisadi wanavyoweza kuibomoa nchi..Mkapa alikuwa fundisho la jinsi kiongozi mmoja arrogant anavyoweza kuifilisi nchi, mafunzo yote haya mawili yananisukuma mimi kuepukana na matukio yenye harufu ya Ufisadi au Arrogant!..na sintapenda wananchi warudie makosa yale..
I still believe Kikwete kisha jikata na Mafisadi..na kweli kuna mbinu kubwa zinafanyika kumwondoa madarakani kwa sababu ambazo ni nje kabisa ya uwezo wake kutawala. Sababu ambazo hazifanani na malalamishi ya wananchi, hivyo upinzani wa aina hiyo nipo radhi kabisa ukiwekewa mikwara unless wajitokeze na kupiga kampeni wazi bila kutumia fedha na umaarufu wao kuwahadaa wananchi ambao asilimia 80 ni maskini..Firaun ni lazima atakamata wengi!