Nidhamu ya Chama: Kiini cha Kudorora Viongozi wa CCM!

Mkuu you should mean it. Wayahudi waliomuua Yesu walimtambua Petro kama mfuasi wa Yesu kwa kauli zake na mwendo wake japo walipomuuliza akili kuwa ni mwanafunzi wa Yesu alikataa kuwa hamjui Yesu. Mkuu japo unasema sio mwanachama wa CCM, hoja zako zinakusuta. samahani kwa kutumia mfano huo kama utakwazika.

- Pole sana mkuu, maana sio siri unakwazika sana na michango yangu hapa JF.

William.
 
Wanaotaka Kikwete agombee 2010, wanaogopa nini? (MwanaHalisi Aprili 15, 2009)

kikwetekampeni.jpg

Kuna kundi la watu waoga wanajitokeza ndani ya CCM. Kundi la watu wasiojiamini na wasioamini kuwa Rais Kikwete anaweza kuchagulika tena 2010. Kundi hili lina hofu kuwa Rais Kikwete anaweza kuamua kutokugombea tena 2010 na hivyo kubadilisha kabisa mwelekeo wa kisiasa katika chama hicho na bila ya shaka nchi nzima. Kundi hili limeanza kuonesha dalili ya kutetemeka na kama wapambe wanaoogopa kupoteza ujiko wao limeanza kujitokeza na kuimba wimbo wa "Kikwete mgombea tena 2010 ndani ya CCM".

Ninajiuliza hawa ndugu zetu wanaogopa nini? Ni kitu gani kinawatia hofu hivi kiasi kwamba mapema mwaka huu (miezi mingi tu kabla ya uchaguzi) wameanza kutishwa na sasa wameamua kujionesha wazi kuwa chaguo lao ni Kikwete? Je kwa kujitokeza kwao kusema ‘chaguo lao ni Kikwete' kunamsaidia Kikwete au kunaonesha udhaifu wake uliopo kuelekea 2010?

Kinachonishangaza ni kuwa hawa ndugu zetu wanaonekana wanatambua kitu ambacho wengine hatukitambui; yaani, ndani ya CCM kuna mtu zaidi ya Kikwete ambaye anatamani kugombea Urais mwakani. Mtu huyo nina uhakika si Shibuda kwani Shibuda alifanya hivyo hata mwaka 2005 na sidhani kama anawatisha hivyo. Kitendo cha mtu aliyekuwa Waziri Mkuu, kitendo cha mtu aliyewahi kuwa Spika na jumuiya mbalimbali za CCM mikoani kuanza kujitokeza na kusema Kikwete ndiye atakuwa mgombea wao kunatudokeza jambo moja kuwa kuna mtu mwingine ndani ya CCM anataka kuwania nafasi hiyo ya Urais.

Mtu huyo ni nani? Sitaki hata kumdhania ni nani lakini kama yupo mtu huyo ana nguvu na ujiko wa kiasi gani hadi kuwafanya watu wazima na akili zao kutetemeka katika majumba yao, kusababisha wakongwe ambao majina yao tulishayasahau kutoka katika maficho yao? Mtu huyo ana ubavu gani wa kushindana na mtu aliyeshinda nafasi ya Urais kwa asilimia 80 ya wapiga kura?

Kama kuna mtu huyo ndani ya CCM basi ina maana ya kuwa mwaka 2005 Watanzania walifanya makosa kumchagua Kikwete. Kwa sababu kama kuna mtu ambaye anaweza kumshinda Kikwete leo hii ina maana mtu huyo tulikuwa naye 2005 na hatukumpa nafasi!

Tulifanya makosa?
Jinsi ambavyo watetezi wa uteuzi wa Kikwete wanavyozungumza ni kana kwamba wako tayari kuendelea na makosa yale yale 2010 bila kuyasahihisha hata kama wakipewa nafasi hiyo. Waoga hawa wanaamini kuwa ni bora kuendelea na kosa lao kuliko kulisahihisha na hivyo wao hawajali jingine lolote isipokuwa hawako tayari kumuona mtu mwingine yoyote akigombea nafasi ya urais zaidi ya Kikwete.

Hapa hatuna budi kujiuliza kama kweli tulifanya makosa 2010 kwa kumchagua Kikwete kama Rais wetu? Hivi tulimchagua kwa sababu tuliona nini? Alikuwa na rekodi gani ya uongozi kumlinganisha na mgombea mwingine yoyote? Alikuwa na uwezo gani wa kiuongozi tukimpima na mtu mwingine? Yawezekana wengi waliopiga walipiga kura kwa sababu ya kuangalia ile sura ya ujana na tabasamu lake? Yawezekana wengine walipiga kura kwa sababu waliamini kuwa yeye kweli ni "chaguo la Mungu"?

Sasa kama wananchi leo wamegundua kuwa walifanya makosa na wanataka kuyasahihisha hawa waoga wa CCM wanataka kuwanyima wananchi nafasi ya kubadilisha uamuzi wao kwa njia ya kura? Kwa ubavu gani walionao?

Kikwete sasa anarekodi!
Mwaka 2005 Kikwete hakuwa na rekodi ya kuonesha uongozi wake na kama ingekuwa katika nchi nyingine kuna mambo ambayo angetakiwa kutolea maelezo ndio maana walimkwepesha kufanya midahalo na wagombea wengine ili watu wampime. Kulikuwa na masuala ya IPTL na tuhuma za kupokea fedha toka Iran na Oman. Bahati mbaya waandishi na wana CCM wengi walikuwa wamepigwa ganzi ya mapenzi kiasi kwamba hakuna aliyethubutu kumhoji maswali magumu na hivyo tukampitisha kwa kufaraha kwa kuangalia vile ambavyo si vya msingi.

Sasa hata hivyo ana rekodi ambayo yeye mwenyewe anaweza kuisimamia. Watetezi hawa wa Kikwete wanatuambia kuwa anaongoza mapambano ya ufisadi wakitolea mfano wa kesi uchwara zilizofikishwa mahakamani (ndiyo nimesema uchwara). Hawa wanataka tumaini kuwa watu kufikishwa mahakamani (tusiangalie mashtaka yenyewe ni yapi) basi mapambano dhidi ya ufisadi yanaendelea chini ya Kikwete.

Lakini rekodi yake sasa ni kubwa zaidi na ambayo mwana CCM yeyote anayo haki ya kuipa changamoto, kuihoji na kumpa nafasi Rais Kikwete kuitetea. Je Rais Kikwete anahusika vipi katika kuwaleta Dowans? Je alihusika vipi katika suala la Richmond pale ambapo baadhi ya watumishi walipotaka mkataba huo usitishwe? Je Rais Kikwete alihusika vipi na kuwaacha watoto wa Kitanzania wasote ugenini na kupigwa baridi kwa kitu kimoja cha kuomba elimu na kuwalazimisha kuwarudisha kwa aibu na kwa nguvu Tanzania toka Ukraine? Kwanini hadi leo serikali yake haijaomba radhi kwa hilo?

Rekodi yake ipo na ninaamini hawa waoga walioibuka siku hizi wanajua hawezi kuitetea! Lakini uzuri ni kuwa kwa kumpambanisha na MwanaCCM mwingine basi tunampa nafasi Rais wetu kuona makosa yake, kukiri makosa ya wazi lakini pia tunampa nafasi ya kujipanga upya. Kumnyima nafasi hiyo ni kuendeleza utamaduni wa woga na sera za unafiki.

CCM siyo Rais!
Mojawapo ya utamaduni mbovu ambao ndugu zetu watetezi wa Kikwete wanataka uendelezwe ni ule wa "kumwachia Rais aliyeko madarakani mihula yake miwili". Dhana hii ni potofu, ya kibabe na aina mfanano wowote na utawala wa demokrasia. Kama hili lingekuwa zuri wao CCM si ndiyo wana Bunge na wana Rais kwanini wasiamua kubadilisha Katiba na kuweka awamu ya Rais kuwa ni muhula mmoja wa miaka kumi! Maana kama tayari wanataka Kikwete awe mgombea wao 2010 na mtu mwingine yoyote CCM asigombee basi waamue tu kufanya uchaguzi wa wabunge na ule wa Urais uahirishwe hadi Kikwete atakapomaliza awamu yake 2015!

Vinginevyo, CCM hawaodhi nafasi ya Urais wa Tanzania na aliyeko madarakani hana ubia na nafasi hiyo. Nafasi hiyo Kikatiba inashindaniwa kila baada ya miaka 5 na hakuna garantii kuwa ukiwa Rais basi mhula wako wa pili utapewa kwa dezo. Kikwete ni lazima apambanishwe ndani ya CCM kama tulivyofanya 2005 na kabla yake, ni lazima arudishe fomu za kugombea pamoja na watu wengine wanaotaka kufanya hivyo, na ni lazima atetee nia yake hiyo kama alivyofanya 2005. Nje ya hapo, CCM itangaze kuwa Tanzania ni nchi ya Udikteta wa chama cha Mapinduzi!

Wanaotaka kugombea wasitishwe
Utawala wa Demokrasia unatutaka tutoe nafasi sawa kwa mtu yeyote anayetaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi. NI kwa sababu hiyo naamini mojawapo ya mambo ambayo yafanyike mwaka huu ni pamoja na Bunge hatimaye kubadilisha sheria ili kuruhusu mgombea binafsi wa nafasi yoyote ya uongozi. Haya mambo ya kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama usichokubaliana na nacho hayana msingi! Katika taifa la watu milioni 40 ninaamini kuna watu wa kutosha wenye akili timamu wanaoweza kufikiria jinsi gani ugombea binafsi unawezakufanyika bila kuweka mzigo mkubwa kwa mgombea yeyote kulinganisha na yule wa chama.

Hata hivyo ndani ya CCM kama kuna watu wanaamini wanaweza kuliongoza Taifa letu vizuri zaidi, kwa kuthubutu zaidi na kuliamsha kuelekea mafanikio na maendeleo ya kweli (ya watu siyo vitu) basi watu hawa wako huru kujitokeza bila kuona haya kama alivyofanya Shibuda. Watetezi wake hawana uhodhi wa CCM na wasitumie jina la CCM kuwatisha watu wengine ambao wako ndani ya Chama hicho.

Kama wao wanaogopa kuwa Kikwete asipochaguliwa tena 2010 basi utakuwa ni mwisho wao na madudu yao yatajulikana basi hayo ni matatizo yao. Ni wao waliokaa kimya bila kujitokeza wakati nchi yetu inapitia wizo mkubwa kabisa wa mabilioni ya fedha, lakini linapokuja suala la hamu zao wanajitokeza huku wakitingisha vidole vyao!

Mtanzania yoyote ndani ya CCM anayetaka kugombea nafasi ya Urais ni lazima apewe nafasi sawa.

Vinginevyo, kama waoga hawa wanajua kuwa Kikwete hawezi kushinda akipambanishwa na mtu mwingine CCM basi ushauri wangu ni kuwa wawatimue wale wote ambao wanaonesha nia ya kutaka kupambana na Kikwete! Wawatimue na kuwafukuza katika Taifa la Tanzania! Na wawanyang'anye na uraia kabisa ili wasirudi.

Wakishafanya hivyo, waamue kufuta sheria inayoruhusu vyama vingine ili tuwe na chama kimoja chenye mgombea mmoja tu wa CCM ili Taifa zime limpigie kura za Ndiyo au Hapana. Na kama akipata kura nyingi za Hapana, basi wamuapishe kuwa ni Rais kwani atakuwa bado amepata kura nyingi!

Vinginevyo, wamuache Rais Kikwete afanye kazi yake na akitaka kugombea mwakani agombee akiamua kupumzika apumzike na kuwapisha wengine. Alipotaka kugombea ilikuwa ni kwa miaka 5 na kama kwa sababu zake zozote akiamua kutokugombea basi asijisikie shinikizo la kugombea ili kuwaridhidha watu fulani ambao muda wao wa kisiasa umeshapita!

Lakini akitaka kugombea basi asitumie vyombo vya dola au hawa wapambe kutuma ujumbe wa vitisho kwa watu wanaompinga au ambao wanaamini wanaweza kufanya bora zaidi ndani ya CCM bali awe tayari kusimama na rekodi yake na hoja zake kugombea tena nafasi ya Urais.

Kwa kufanya hivyo Rais Kikwete atathibitisha kuwa yeye ni mwanademokrasia na ambaye hana hofu ya kushindana na mtu yeyote kwenye sanduku la kura. Iwe ni mwana CCM mwenzake au nje ya CCM. Lakini endapo Kamati Kuu au chombo kingine rasmi cha Chama kikitoka na kusema kuwa Mgombea wa CCM atakuwa ni Kikwete tu basi lile shimo la kifo cha demokrasia tuliongezee kina chake ili ndani yake wa kwanza kutumbukizwa atakuwa ni Chama cha Mapinduzi!

Vinginevyo, mwana CCM anayetaka kugombea na kushindana na Kikwete asiwaogope waoga hawa mambo leo na asione haya kuonesha nia yake hiyo na wala asionekane adui bali asimame kama mwanademokrasia na mwanamapinduzi wa kweli kugombea nafasi hiyo na kutoa changamoto hiyo kwa Kikwete. Yeyote ambaye hapendi akimbilie baharini ajitose!

Niandikie: mwanakijiji@mwanakijiji.com
mkjj..

wanasiasa wa ccm wamechokaaa na kutawaliwa na ubinafsi mkubwa wa matumbooo yaoo tuuu...

ni kweli hofu ya kikwete kutawala tena kutokana na uwezo mdogo aliounyesha imewajaa wanasiasa wengi uchwara ndani ya ccm.

wapo wanasiasa wangependa kupanua demokrasia ndani ya ccm kwa kupambana na mtawala aliyeko madarakani ila bado kiwingu cha hofu ya kunyoshewa vidolee inawasumbuaa..

hapa namaanisha wanasiasa wa juu kama sumaye, mwandosya, ambao naamini bado wana kiu ya kupambana na kuweza kupata tiketi ya kugombea kupitia chama hicho kilichowaneemeshaa...

pia kundi la akina sitta, mwakyembe, seleli, kilango linatamani sana kumtingisha kikwete na wenzie hasa mtandao masilahi ambao sasa kashfa za ufisadi zimewachafua sanaaaaa (EL, RA, KARA,....)

Pia akina mramba, yona na vijana watiifuu wa MKAPA hawafurahii hata kidogo JK anafowafanyia kambi yao kwa ujumla kwa kuwadhalilisha kwa kila hali kwa mbinu mbali mbali kuanzia media, takukuru, dpp na mahakama.. hawa wana imani ipo siku ya kikwete kulipa ubaya wake....

ccm kwa sasa haina msingi wowote zaidi ya makanjanja wa kukwapua rasilimali zetuuu kwa kulaghai wananchi wa tanganyika kupitia umasikini waooo..

INAWEZEKANA akina mwandosya, sumaye kumtingisha JK..ANATINGISHIKAAAAA!

WAJIFUNZE KWA WANASIASA MAHIRI WALIOJIJENGA KWA KUAMINI UWEZO WAO NA SII KELELE ZA CHAMA DOLA...DKT SLAA NI DARASA ZURI SANAA..

KUPINGA NA KUSONGA MBELE INAWEZEKANA.
 
Zaidi ya kukwazika yaani!

Bro hebu nisaidie hive una undugu na jamaa anayejiita FMES naona wote mnashabiana sana kwa kuleta mavitu mazuri humu?


- Mkuu wananchi wanachangia hoja nzito ya taifa hapa, kama huna hoja kaa pembeni unataka niyataje majina yako humu si itakuwa aibu, au unafikiri una akili sana?

- Kama huna hoja kaaa pembeni mkuu!


Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Mkuu FMES,
Mimi kinachonishinda kuelewa ni hawa wanaopinga (kina Mwanakijiji) kinawaogopesha nini wao ikiwa kuna kundi la watu wamesema Kikwete ndio Chaguo lao?..
Mimi nikisema Chaguo langu ktk kugombea kiti cha rais ni Dr. Slaa na hafai kuwa na Mpinzani.....kuna tatizo?..Je, kuna kitu naogopa au ndio chaguo langu mimi na sidhani kuna ulazima wa kuonyesha ame accomplish vitu gani kuweza kupata sifa hiyo..
Kusimama kama mgombea ni sifa inayotokana na sifa za Uchaguzi, nani anafaa kuwa rais ni Chaguo la wananchi wote wala sii swala la viongozi wa CCM, Spika wa Bunge au Mkandara..

Mkuu Mkandara, heshima kwako. Mkuu, kinachosumbua sio chaguo la kimaoni linalotolewa na "VIONGOZI" wanaojitokeza na kupendekeza kwa kusema hadharani kuwa Kikwete atagombea kuwa Rais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2010. SIo hilo hata kidogo. Tatizo ni pale wanapokwenda mbele zaidi na kutishia kuwa asijitokeze mwingine wa kumpinga JK katika uchaguzi huo. Mkuu hilo ndilo tatizo.

Kauli ya kupendekeza ni maoni halali kabisa. Kauli za kuhitimisha hoja ambayo mtu hana mamlaka ya kuhitimisha ni kosa. VIONGOZI hao waliojitokeza kusema hadharani kuwa hakuna anaetakiwa kumpinga JK 2010 kwa kuzingatia utamaduni uliopo ndani ya chama wanakosea wanapofanya hivyo. Wanakosea kwasababu tu, wanataka wengine wasio na nguvu kama walizonazo wao waogope kupingana na maamuzi yao (si maoni yao). Maamuzi ya kuwa JK ndie atakaegombea peke yake.


I mean hizi hofu za Kikwete kuchukua awamu ya pili kunatokana na kitu gani?.. Je ni sisi wenye wasiwasi kwamba Kikwete anaweza kuchukua tena ikiwa hatapata ushindani ndani ya CCM?..Na kama kuna ushindani ni mtu gani tunayefikiria anaweza kuyatimiza mapungufu yote tuliyoorodhesha!..ukiuliza hivyo unaambiwa wapo wengi KINA NANI?.. Je, mmeweza kuongea nao wakasema watatizmiza yote aloshindwa Kikwete?.. hapana!..

Mkuu wangu hata nashindwa kuwaelewa Wabongo, waliosema wana sababu kubwa kwamba hawataki kubadilisha Nahodha hata kama anawapoteza kwa sababu hawaoni nahodha mwingine anayeweza kuongoza na jahazi lao..
Kama wewe ni msafiri na umo ktk jahazi hilo huwezi kupinga tu kuendelea kwa nahoidha huyo wakati wewe sio tu huwezi kuongoza jahazi huna mtu yeyote ambaye yuko tayari kuongoza. Mtu ambaye wasafiri wengine pamoja na mashaka yao wanaweza sema.. KWELI huyu Kikwete ameshindwa, hatutafika huko tuendako bora huyu ambaye anaonekana anafahamu tunakotaka kwenda.

Wanabodi,
Jamani eeeh, nchi yetu imekosa mwelekeo sii jana wala juzi. tanzania leo inaongozwa bila dira na Kikwete kama nahodha yeyote yule hawezi kufanya maajabu ikiwa hana dira na yeyote mtakayemleta kugombea dhidi yake hataweza kuongoza kwani CCM hawana dira tena...wote wanahaha iwe Kikwete kurudi au kuondoka!

Jibu rahisi sana Chagueni Chadema.. Chama ambacho kimejizatiti kurudisha dira ya Taifa... chama kitakacho ongoza kwa kufuata MWONGOZO wa taifa letu hatua kwa hatua hivyo mnafahamu kabisa nini nafasi ya mchango wenu kama wasafiri.

Hofu za JK kuwa Rais wa nchi hii baada ya uchaguzi ujao (kwa mtazamo wangu) zinatokana na ufanisi wake katika kipindi hiki kinachomaliza 2010 (kabla ya uchaguzi. Ufanisi ambao inavyoelekea kwa wengi haujafikia malengo. Na hayo pia ni mawazo yao ya kikatiba kabisa.

Kila mtu anatakiwa kupewa fursa ya kujitokeza (kama anataka kufanya hivyo) kugombea nafasi hiyo. Mimi naamini kabisa Mkuu kuwa katika hili hata wewe unalikubali. Si vyema kutajana majina wakati huu. Tuache demokrasia itawale, wenye nia wakiona inafaa wajitokeze (kwa uhuru na haki kabisa), wananchi wawaangalie kama wanafaa na mwisho uchaguzi uamue. Ni hilo tu. Matokeo yoyote ya uchaguzi huru na wa haki, ni matokeo mema na ya kuungwa mkono. Bila kujali nani kapewa haki hiyo. Naamini kabisa kwamba ifikapo mwaka 2010, watakaoona wanaweza kuongoza nchi watajitokeza (kutoka upinzani na ndani ya CCM). Ni vyema waachiwe kufanya hivyo.

Kama ilivyo kwa JK, si haki kumkataza JK asigombee 2010 na kulazimisha mgombea mwingine yeyote. Kila mtu anatakiwa apewe haki sawa.
 
Mkuu Mkandara, heshima kwako. Mkuu, kinachosumbua sio chaguo la kimaoni linalotolewa na "VIONGOZI" wanaojitokeza na kupendekeza kwa kusema hadharani kuwa Kikwete atagombea kuwa Rais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2010. SIo hilo hata kidogo. Tatizo ni pale wanapokwenda mbele zaidi na kutishia kuwa asijitokeze mwingine wa kumpinga JK katika uchaguzi huo. Mkuu hilo ndilo tatizo.

Kauli ya kupendekeza ni maoni halali kabisa. Kauli za kuhitimisha hoja ambayo mtu hana mamlaka ya kuhitimisha ni kosa. VIONGOZI hao waliojitokeza kusema hadharani kuwa hakuna anaetakiwa kumpinga JK 2010 kwa kuzingatia utamaduni uliopo ndani ya chama wanakosea wanapofanya hivyo. Wanakosea kwasababu tu, wanataka wengine wasio na nguvu kama walizonazo wao waogope kupingana na maamuzi yao (si maoni yao). Maamuzi ya kuwa JK ndie atakaegombea peke yake.




Hofu za JK kuwa Rais wa nchi hii baada ya uchaguzi ujao (kwa mtazamo wangu) zinatokana na ufanisi wake katika kipindi hiki kinachomaliza 2010 (kabla ya uchaguzi. Ufanisi ambao inavyoelekea kwa wengi haujafikia malengo. Na hayo pia ni mawazo yao ya kikatiba kabisa.

Kila mtu anatakiwa kupewa fursa ya kujitokeza (kama anataka kufanya hivyo) kugombea nafasi hiyo. Mimi naamini kabisa Mkuu kuwa katika hili hata wewe unalikubali. Si vyema kutajana majina wakati huu. Tuache demokrasia itawale, wenye nia wakiona inafaa wajitokeze (kwa uhuru na haki kabisa), wananchi wawaangalie kama wanafaa na mwisho uchaguzi uamue. Ni hilo tu. Matokeo yoyote ya uchaguzi huru na wa haki, ni matokeo mema na ya kuungwa mkono. Bila kujali nani kapewa haki hiyo. Naamini kabisa kwamba ifikapo mwaka 2010, watakaoona wanaweza kuongoza nchi watajitokeza (kutoka upinzani na ndani ya CCM). Ni vyema waachiwe kufanya hivyo.

Kama ilivyo kwa JK, si haki kumkataza JK asigombee 2010 na kulazimisha mgombea mwingine yeyote. Kila mtu anatakiwa apewe haki sawa.

- Mkuu Recta, hakuna aliyezuiwa kugombea urais ndani ya CCM, tusianzishe maneno na hoja ambazo haziwezi kulisaidia taifa, kama tumeshindwa nguvu na akili za kujikomboa tukubali tu badala ya kuanza ku-create maneno yasiyo na faida kwa taifa.

- Hatuwezi kujikomboa na hoja za reactionary, mpaka kwanza wachache ndani ya CCM waseme maoni ndio sisi tujibu, eti ndio tutajikomboa na this kind of reactionary politics?

- Maana yake ni moja tu, kwamba miaka minne ya utawala wa Mtandao, hatukuwa na political strategy yoyote serious au valid ya kuwaondoa 2010, na hii ni kwa sisi wananchi mpaka vyama vya siasa, kazi kula ruzuku tu sasa tumekwama na kama kawaida yetu tunajaribu kutupia lawama to the wrong place, aibuuu kwetu vijana!

FMES!
 

- Mkuu wananchi wanachangia hoja nzito ya taifa hapa, kama huna hoja kaa pembeni unataka niyataje majina yako humu si itakuwa aibu, au unafikiri una akili sana?

- Kama huna hoja kaaa pembeni mkuu!


Wazee wa sauti ya umeme FMES!
FIELD MARSHALL !!, Polepole mzee cheo chako (Field Mashall) kikubwa sana katika uwanja wa mapambano. Ukikasirika haraka haraka, wapiganaji wanaweza kukosa mwelekeo, mkuu
 
- Mkuu Recta, hakuna aliyezuiwa kugombea urais ndani ya CCM, tusianzishe maneno na hoja ambazo haziwezi kulisaidia taifa, kama tumeshindwa nguvu na akili za kujikomboa tukubali tu badala ya kuanza ku-create maneno yasiyo na faida kwa taifa.

- Hatuwezi kujikomboa na hoja za reactionary, mpaka kwanza wachache ndani ya CCM waseme maoni ndio sisi tujibu, eti ndio tutajikomboa na this kind of reactionary politics?

- Maana yake ni moja tu, kwamba miaka minne ya utawala wa Mtandao, hatukuwa na political strategy yoyote serious au valid ya kuwaondoa 2010, na hii ni kwa sisi wananchi mpaka vyama vya siasa, kazi kula ruzuku tu sasa tumekwama na kama kawaida yetu tunajaribu kutupia lawama to the wrong place, aibuuu kwetu vijana!

FMES!



Mkuu unajua wengi wetu woga we unafikili kuna watu hawataki kuchukua fomu?Wanapenda sana lakini wanaogopa sana kusutwa au kutengwa....
 
Unajua NIni? Kikwete akisema hatogombea 2010 ndipo tutaona jinsi CCM ilivyogawanyika. Natumaini atatangaza mapema kuwa hana mpango wa kugombea tena..


Ninadhani atafanya hilo tamko mapema sana ili wenye uwezo wa kuchukua nafasi yake wajitokeze mapema kwa sababu anajua maswala mazito yahusuyo mustakabali wa taifa letu yanasubiri mwenye ushujaa wa kuyatekeleza. Huo mgawanyiko utajionyesha wazi na hapo ndio mpambano wa kweli ndani ya chama utatokea. Ilivyo sasa watu wanakufa na nia zao za kugombea ndani ya mioyo yao, wanaogopa kujitokeza kwa kutopewa nafasi ya kufanya hivyo, au kwa kuogopa hatima yao iwapo watafanyiwa udikteta na chama baada ya azma yao kuwa wazi. Lakini wa kukinusuru chama hivi sasa ni Kikwete pekee kwa kutoa hiyo fursa, makundi yapambane, wenye kujing'oa waondoke, chama kibaki na wasafi tu. Tofauti na hapo tutaona chama kingine kikiongoza hii nchi, tuombe uzima.
 
Kwa maoni yangu,ile 2005, CCM hawakukosea kumteua JK, si waangalia sura na tabasamu za bashasha kwa matumaini ataitetea ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi. Kampeni za ndani ya chama mnazijua zikisaidiwa na magazeti na make belive za Adobe Photoshop, matokeo JK alipita. kuna kosa kweli hapo?.

Baada ya kuteuliwa na CCM, alizungushwa nchi nzima akiinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Wananchi wakaikubali, wakamchagua kwa kura nyingi zilizopelekea kumpa ushindi wa kishindo. Hapo jee, kuna kosa?. Kwa maoni yangu mpaka hapa hakuna makosa.

JK ameanza kazi kwa nyimbo na mapambio ya Ari Mpya,Kasi Mpya na Nguvu Mpya zikiendana na kibwagizo cha 'Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania'. Mpaka sasa, kipi kimetekelezwa katika ilani huku nyimbo za mapambio zikipunguza mdundo mwisho zimenyamaza kabisa, ndipo watu wanaanza kujiuliza hivi kuna makosa yalitendwa?.

Jibu ni hakuna makosa tangu uteuzi mpaka uchaguzi, tatizo, watu waliangalia sura, sasa ukweli wameona. kuna waliomchagua kwa imani kubwa kuwa jamaa atafanya mambo, sasa wanapingwa na butwaa kukuta tabasamu zuri ni asili yake, hata akikasirika anaonekana kama anasmile.

Waungwana wanajiuliza uwezo wake kiuongozi, kiutawala, kibusara na uono wake baada ya kutuendesha tangu alipokamata unahodha wa jahazi alipotutoa 2005, hapa alipotufikisha 2009 na swali jee 2010 aendelee kuliongoza jahazi ili kutufikisha mahali 2015 ama hapo ndio mwisho wa uwezo wake, tutafute nahodha mwingine?.

Kwa maoni yangu, nahodha kashindwa kazi, chombo kinayumba yumba, ila hakijazama, na kama nahodha ataendesha taratibu au kuamua kusimama njiani, chombo hakitazama na mwisho wa siku tutafika safari yetu salama hata kama itachukua miaka 40 njiani kama kwenye kitabu cha 'Kutoka'.

2010, tunatafuta nahodha mwingine, kwa maoni yangu, hakuna nahodha mbadala mpaka sasa, na kitakachofuatia ni bora nahodha huyu huyu alimradi hatuzami, ndio maana nimekuwa nikisema na leo ninasema tena na tena...
"Kuna wengi wamechoshwa na CCM tangu juzi, lakini kwa vile hawajaona chama mbadala mpaka kesho, basi bora waendelee kuichagua hiyo hiyo CCM mpaka keshokutwa kitakapojitokeza chama mbadala. 2010 hiyo inakuja na haya mtayashuhudia".
 
Mkuu unajua wengi wetu woga we unafikili kuna watu hawataki kuchukua fomu?Wanapenda sana lakini wanaogopa sana kusutwa au kutengwa....[/QUOTE]

- Unapotaka kuchukua fomu unachukua fomu, hivi unajua what Obama went through mwanzoni? hizi excuse za uoga uoga mpaka lini?

- Tumeshindwa that is the bottomline, maneno mengi kumbe hakuna mkakati wowote, hawa kina Dr. Slaa, Mbowe, Mrema, Lipumba, Zitto wametuangusha period, ndio wametuangusha maana ni viongozi tuliokuwa tunawategemea watusafishie njia na tumewaunga mkono sana hapa JF, tumewapa siri chungunzima hapa za watawala hoping watazifanyia kazi na kuwamsha wananchi, kumbe ilikuwa bure.

- Sasa kilichobaki ni kuanzisha chama chetu cha siasa, cha JF na kusimama wenyewe ili 2015 tufanye kweli, unaiudhi na inasikitisha sana!

FMES!
 
Kwa maoni yangu, nahodha kashindwa kazi, chombo kinayumba yumba...., mwisho wa siku tutafika safari yetu salama hata kama itachukua miaka 40.

.... hakuna nahodha mbadala mpaka sasa, na kitakachofuatia ni bora nahodha huyu huyu alimradi hatuzami.

..... lakini kwa vile hawajaona chama mbadala mpaka kesho, basi bora waendelee kuichagua hiyo hiyo CCM mpaka keshokutwa kitakapojitokeza chama mbadala..


Watu bwana, mhhh!
Kweli hakuna Mtanzania mbandala (ndio maana yake, hata huko CCM hakuna). Kumbe inaonekana zote hizi ni ili kumsimamisha mgombea wa upinzani kupitia ccm. Hii ni kali na imekaa kiaina vile.

Watanzania wanahitaji mabadiliko yatakayobadilisha hali zao za maisha, na wakati daima ni ukuta, kama kiongozi anaonekana kupwaya, maana yake ampishe mwenzie asukume gurudumu!
 
- Sasa kilichobaki ni kuanzisha chama chetu cha siasa, cha JF na kusimama wenyewe ili 2015 tufanye kweli, unaiudhi na inasikitisha sana!

Sounds good, but also sounds like "British indirect rule" (divide them and rule them)
 
1.

- Sawa sawa, hapa tuko pamoja kila M-Tanzania ana haki ya kutoa maoni yake.

2.

- Sijakuelewa, nilifikiri hapo hoja inatakiwa kua kila m-Tanzania ana haki ya kuuliza validility ya hoja ya mwananchi mwignine, lakini sio kuingilia haki ya kutoa maoni yake!

3.

- Unaona sasa, hivi hao wanachama wachache wa CCM, wamemlazimisha nani kukubali mawazo yao kwamba lazima rais wa sasa aendelee? Ni wapi wamejaribu kubadili katiba?

- Halafu unaita maoni yenu, si unaona ubabe huu ambao mnadai hamuutaki, maana anayejaribu kuwa-question na hizi ideas basi na yeye ni maoni yenu, something is not right na hizi thinking na wala haziwezi kutusaida sisi wananchi at large.

3.

- Sawa sawa.

4.

- Unajua ni afadhali kwamba wazazi wako hawajasema kabisa, maana kama mawazo yao ni kama haya yako, ya ubabe ubabe na name calling basi wana busara sana kutosema anything, pole sana mkuu!

5.

- Hebu rudia maneno yako mwenyewe, hata sielewi unachosema, wewe ndiye uansimamkia uhalali wa maoni ya wananchi? toka lini mkuu?

6.

- Unaona kumbe ni yale yale, jina tofauti maneno yale yale naona mkuu una muda mwingi sana na chuki flani za binafsi, maana hapa unaonyesha rangi zako wazi, kwamba huna haja ya mjadala wa hoja ila ubabe na kutafuta ushujaa at the wrong place na the wrong persona, mimi sitishiki na hizi kelele zako za mlango, ambazo umekwua ukizirusha siku nyingi sana na recently naona una neno wazazi wako kama vile unawafahamu.

- Mkuu si unajua vizuri sana kwamba kati ya mimi na familia yangu na wewe nani hasa ni mwizi na mtapeli, kweli unataka nirudie tena hapa mbele ya umma? si iatkuwa aibu ndugu yangu. Ni mara nyingi sana nimekupa nafasi useme wizi wangu, ufisadi wangu, na wa familia yangu uweke hapa wazi wananchi wote wauone, mara ya mwisho ulisema wazazi wangu wanamteeta Kikwete kwa sababu sisi wote tunafanya ubalozini, nikakuomba useme ni ubalozi wa wapi hukujibu tena, sasa here you are again,

Hizi ndio zinaitwa kelele za mlango, yaani uongo uongo na uzandiki, hauwezi kulisaidia taifa letu hata siku moja!

Ahsante.

William.

*Naona umejaribu kutake personal maoni yangu, unaruhusiwa kama yanakugusa kiasi hicho mpaka umeamua kuonyesha rangi zako zote. *Nakushauri urudie tena kusoma maoni yangu halafu tanabaisha chembe ya ubabe ambao utauzidi wa kwako katika kujibu hoja hizo.
*Tatizo lako pia umefananisha characters, hasira zako kwa mtu anayefanana maoni na yangu umeamua kuhamishia kwangu? Sina muda wa kujitetea, lakini ukweli ni kwamba sina uhusiano na jina lingine tofauti hapa JF, siwezi kuwa na muda wa kutumia majina tofauti kwa lengo gani na kwa faida ipi hasa?
* Ukweli ni kitu wanasiasa wenye mlengo kama wako wasichopenda kukisikia, na ili tuwe huru lazima tuwe wakweli, kutaka kulazimisha maoni yenu yawe ndio agenda ya Taifa ni jambo lisilovumilika, not anymore.
*Kutumia "Wazee wenu na wenzako" ni kujaribu kukuweka karibu na wale ambao unawashabikia kwa sababu zinazojulikana na wewe mwenyewe binafsi, kukutofautisha nao ni kukukosea haki Mkuu.
*Hizo hasira zako zinatokana na maoni yangu au ni majumuisho ya siku nyingi? Uongo na uzandiki uko wapi hapa?
*Hayo mambo ya ubalozini na blah blah siyajui kwa sababu sina uhusiano wowote na siasa wala ambitions za kuwa mwanasiasa, ni vyema ukataja ni jina gani lingine natumia kwani naona umeamua kuparamia!!
 
...2010, tunatafuta nahodha mwingine, kwa maoni yangu, hakuna nahodha mbadala mpaka sasa, na kitakachofuatia ni bora nahodha huyu huyu alimradi hatuzami, ndio maana nimekuwa nikisema na leo ninasema tena na tena...
"Kuna wengi wamechoshwa na CCM tangu juzi, lakini kwa vile hawajaona chama mbadala mpaka kesho, basi bora waendelee kuichagua hiyo hiyo CCM mpaka keshokutwa kitakapojitokeza chama mbadala. 2010 hiyo inakuja na haya mtayashuhudia".

Kinachoudhi ni kwamba dalili zote zinaonyesha CCM bado ndio itaendelea kuongoza nchi either yenyewe fully kama leo au mseto iwapo hawa wapinzani watajimwaga kwenye ubunge ipasavyo. Si kweli kwamba CCM yooooote ni chovu na mbovu kiasi hicho. Ndani ya CCM kuna watu wachache wasafi, wenye mwelekeo, upeo na uwezo wa kuiongoza hii nchi. Hawa watu hawapewi upenyo; wamezingwa na madikteta, mazee, mafisadi na kila aina ya wabaya. Hawa ndio tunaotaka waamke, wajiamini, wapambane, wajitokeze, wagombee uraisi 2010 kumsaidia 'cheka cheka' asizamishe hili boti. Ni ukweli usiopingika kwamba mabadiliko ya nchi hii hayatakuja ndani ya siku moja. CCM haitang'oka ndani ya siku moja. Na lengo letu sio kuing'oa CCM by the way, tunataka kuwang'oa wanaoihujumu nchi hii, ili wananchi wafaidike na nchi yao, wapate maisha bora. Ndio maana nikafikiri JK ana busara za kutosha kuona anahitaji kumwachia mtu mwingine kiutu uzima, nafikiri hata washauri wake wameshaanza kumpa hiyo.

Nina imani kuwa akijitokeza mtu shupavu ndani ya CCM mwenye ujasiri wa kuwakemea na kuwafukuza uanachama akina '....mafisadi' na kutulindia raslimali zetu, malalamiko hayatakuwepo. Lengo la kuwa na upinzani ni kunyoosha pale uongozi unapokosea, not necessarily kubadilisha power. Wana CCM ni wagumu kukubali kwamba hawailetei nchi yetu maendeleo, licha ya evidence zoooooote za wizi walizonazo. Unfortunately tukisema wan CCM ni wote!

Anyway, back to the subject: hawa wanaopiga debe sasa hivi nahisi wana moja kati ya haya matatu.

Moja: Either, wanafaidika na current regime hivyo wanajikomba kwa 'bosi' ili waendelee kuvuta kiulaini; hawwa ni wanafiki wanaotafuta sifa na nafasi nzuri katika chama na serikali. Hawa wamekata tamaa na hawajali liwe liwalo maana uwezo na nafasi yao ya kuchukua significant position kwenye uongozi haipo.

Mbili: Au wanajifanya wako happy na mkuu wao, hivyo wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa - huku underground wana mishe zao za kumwandaa 'huyo mtu wao' atakayemwibukia JK kwa surprise. Kama hii ndio strategy, kwa kumtangazia JK kuwa 2010 ni automatic, atapumbazika na kulala tu akidanganyika yes yes, kumbe huku nyuma kambi inaandaa mambo mazito - by the time anashtukia mtu anachukua fomu, mzee mzima too late!

Tatu: Au ndio njia anayotaka kuitumia mzee mzima kuachia ngazi 2010 kisiasa. Unajua watu wakubwa hawa bwana hata wakivurunda wanapenda waondoke kwa sifa. Aongee aseme, mimi nimeamua 'kung'atuka' bwana, nchi bado ilikuwa inahitaji na chama na wazee waliniomba sana. Lakini nimeamua kuachia kipindi kimoja nikafanye shughuli za kimataifa. Kwani hamkumsikia yule aliyesema anaenda kufanya kazi za UN baada ya term zake mbili kuisha.... wapi mtu mwenyewe mwizi nani akupe kazi kama hiyo.

Kwa ufupi, si hivi hivi kuna jambo linapikwa (my thinking).
 
Mkuu unajua wengi wetu woga we unafikili kuna watu hawataki kuchukua fomu?Wanapenda sana lakini wanaogopa sana kusutwa au kutengwa....[/QUOTE]

- Unapotaka kuchukua fomu unachukua fomu, hivi unajua what Obama went through mwanzoni? hizi excuse za uoga uoga mpaka lini?

- Tumeshindwa that is the bottomline, maneno mengi kumbe hakuna mkakati wowote, hawa kina Dr. Slaa, Mbowe, Mrema, Lipumba, Zitto wametuangusha period, ndio wametuangusha maana ni viongozi tuliokuwa tunawategemea watusafishie njia na tumewaunga mkono sana hapa JF, tumewapa siri chungunzima hapa za watawala hoping watazifanyia kazi na kuwamsha wananchi, kumbe ilikuwa bure.

- Sasa kilichobaki ni kuanzisha chama chetu cha siasa, cha JF na kusimama wenyewe ili 2015 tufanye kweli, unaiudhi na inasikitisha sana!

FMES!

Mimi naomba kuwa mwenyekiti
 
- Ndani ya CCM kuna wananchi ambao kwa maoni yao, wanaona rais wa sasa anahitaji kuendelea ili amalizie mihula yake miwili...

Jinsi nionavyo, tatizo ni hitimisho. Kuna watu wamesikika kutishia wale watakaojitokeza kutaka kugombea. Let's face it, kwa Tanzania ya leo, siasa za CCM zina mchango/athari kubwa kwa mustakabali wa nchi hii. Na baadhi yetu tunajiuliza (hebu na mtu ajitokeze aelezee), hivi kampeni za waziwazi (tena ndani ya chama) huanza au zinatakiwa kuanza wakti gani kabla ya uchaguzi (ngazi ya chama/taifa)?

Kila mtu ana haki. Kikwete ana haki ya kugombea tena, kama walivyo wengine, wana haki ya kutaka kugombea. Wasichimbwe mkwara..

JMK yuko madarakani kwa sasa, bado ana kibarua mbele yake, si ajikite zaidi walau mwaka huu kuchapa kazi badala ya kukumbatia kampeni nyepesi nyepesi kama hizi? Najitahidi kujizuia kuwaza kwamba JMK hahusiki na hizi kamapeni-tangulizi, tena najitahidi sana, lakini nashindwa kujishawishi vinginevyo.
 
Mkuu MKJJ,

Hii mikwara ya akina Ndejembi na Kimaro ni ya kitoto, ya kijinga na imepitwa na wakati. Inawezekana wametumwa au wamekurupuka. Either way wanatia aibu.

MwanaCCM yeyote anayekidhi vigezo vya kugombea urais atakayeogopa kuchukua fomu kwasababu ya hii mikwara nae ni ****.

Sasa nasubiri kuona reaction ya Mheshimiwa Kikwete. Mi ningekua yeye, at the earliest opportunity ningesema something to the effect, "Ndugu wanaCCM wenzangu, nashukuru kwa support yenu, ila kwa wale wanaopiga mkwara wanachama wengine wasijitokeze kugombea urais ningewaomba wasitishe hizo kauli. Kazi niliyoifanya inaonekana na ndo itakua msingi wangu wa kuwaomba Watanzania kura zao niendelee kuwaongoza".

Hii ni fursa kwa Mheshimiwa kuonesha political maturity. Wale wanaotoa kauli za mkwara hawamsaidii bali wanamkwaza. Wamem-preempt aoneshe kwamba hahitaji kupigwa chepuo. Akikaa kimya atadhihirisha kwamba kweli yeye ni kiongozi dhaifu aliyeshindwa kazi aliyowaahidi wananchi na anahitaji kupigwa jeki.

The ball is in JK's court.
 
Back
Top Bottom