Nidhamu ya Chama: Kiini cha Kudorora Viongozi wa CCM!

Nidhamu ya Chama: Kiini cha Kudorora Viongozi wa CCM!

Date::4/15/2009
Kikwete atapimwa kwa matendo yake 2010.

Elias Msuya

Mwananchi
​

Ukiwa umebaki mwaka mmoja tu ili kufikia uchaguzi mkuu, tayari kitendawili cha nani agombee urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 kimeibuka.

Ingawa Katiba ya CCM inawapa haki wanachama wote wa chama hicho kugombea nafasi za uongozi, CCM imejiwekea utaratibu wa mgombea Rais kugombea kwa vipindi viwili mfululizo.

Utaratibu huo ndiyo unaowachanganya watu kwasababu haieleweki watu wafuate katiba au utaratibu wa kuvumiliana kwa miaka kumi.

Kwakuwa wengine wanadhani Katiba ndiyo yenye nguvu wameamua kujitokeza kugombea.


Lakini, hivi karibuni Wameibuka wazee wakimpigia kampeni Rais Kikwete aendelee kugombea kipindi cha pili. Mara ya kwanza tulimsikia aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Samuel John Malecela akisema kwamba mwaka 2010 ni Rais Kikwete tu.

Mara wakaibuka wenyeviti wastaafu wa mikoa wa CCM akina Pancras Ndejembi,Tasiri Mgoda na Hemed Mkali. Wao walinza na gea ya kukemea ufisadi, lakini wakaishia kusema kuwa mwaka 2010 ni Rais Kikwete tu.

Na wengineo wengi alimradi siku hizi kila ukiamka wanaibuka wana CCM wa kumpigia kampeni Rais Kikwete, utadhani uchaguzi ni mwezi ujao.

Wana kampeni hawa wanatoa sababu ya kumpendekeza Rais Kikwete agombee tena mwaka 2010 kuwa ni, wananchi wameridhishwa na uwezo mkubwa aliouonyesha Rais Kikwete katika kupiga vita ufisadi, na kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Wanaendelea kusema kuwa, hata katiba ya chama na Katiba ya nchi zinamruhusu kuendelea kugombea.

Mimi binafsi sipingi Rais Kikwete kuendelea kugombea mwaka 2010, kwasababau hata hivyo hakuna kitu kinachomzuia kufanya hivyo.

Kinachonishangaza ni hawa wapambe wanaoanza kumpigia kampeni sasa hivi. Kwani ni nani aliyemzuia Rais Kiwete kugombea hadi watu waanze kupiga kampeni? Hata kama Rais Kikwete amefanya mambo mengi ya maendeleo, kuna haja gani ya kuanza kumpigia debe sasa hivi? Au kuna Mtanzania asiyemjua Rais Kikwete?

Waswahili husema kwamba, "Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza".

Hakuna Mtanzania asiyejua kila anachokifanya Rais Kikwete na serikali yake. Kama ametekeleza au hakutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, watu wanajua. Ni bora Wanaompigia debe waache matendo mema ya Rais Kikwete yamuuze, badala ya maneno yao.

Mkakati huu wa kumpigia debe Rais Kikwete unadhirisha mambo mawili. Ama wametumwa na Rais Kiwete mwenyewe au wanajipendekeza tu.

Kama wametumwa na Rais Kikwete mwenyewe, basi ujue tayari joto limeshaanza kupanda na ameanza kuhofia nafasi yake mwaka 2010. Huenda ameshaona, kama wana CCM wataruhusiwa kugombea sambamba naye hataambulia kitu.


Lakini kama hawa wazee, wazazi na vijana wanaompigia kampeni wamejituma wenyewe, basi ujue hiki chama kimejaa watu waoga, wasiohoji mambo hata kama yanakwenda mrama.

Inawezekana pia kuna watutu wanatumia jina la Rais Kikwete kufichia maovu yao.

Wanapita huku na huko kumnadi Rais Kikwete huku wakiendelea na ufisadi wao. Watu hao hujifanya kuwa karibu sana na Rais lakini kumbe ni mafisadi wakubwa.

Sina ugomvi na utamaduni wa CCM wa kuachiana vipindi viwili vya urais. Utaratibu huu unaleta nidhamu ndani ya chama, ambayo itamfanya Rais aliyepo madarakani kutekeleza ahadi zake kwa amani.

Lakini utaratibu huu pia una kasoro. Ndiyo maana hata Katiba ya CCM haijakataza mwana CCM kugombea baada ya miaka mitano ya kwanza ya Rais aliyeko madarakani.

Inawezekana Rais akakaa kipindi cha kwanza na akaonyesha uwezo mdogo kiuongozi, je huyo naye aachiwe tu kugombea kipindi cha pili eti kwasababu ndiyo utamaduni wa chama?


Kama mtu ameshindwa kupanga safu yake ya uongozi kikamilifu, ameshindwa kuwashitaki mafisadi, ameshindwa kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania, aachiwe tu kugombea kipindi cha pili eti kwasababu ndiyo utamaduni wa chama?

Tuupime uwezo wa Rais Kikwete kwa kuangalia ubora wa maisha ya Watazania tangu alipoingia madarakani. Maisha ya Watanzania yamebadilika kiasi gani ukilinganisha na ya awamu iliyopita? Uchumi umekuwa kuliko alivyoukuta?

Kila Mtanzania analo jibu, maana 'mvaa kiatu ndiye anayejua wapi kinabana'. Lakini kama tutaamua kusema ukweli, maisha yamezidi kuwa magumu kuliko hata awamu iliyopita.

Mfumuko wa bei umeongezeka wakati kipato cha wananchi kiko chini. Hilo limesababisha migomo mingi ya wafanyakazi na wanafunzi wa vyuo vikuu huku wakulima wakiwa hawana la kufanya. Hiyo ndiyo hali halisi

Ndiyo maana nasema hawa wanaozunguka kumpigia kampeni Rais Kikwete wakati huu, hawana jipya ila kufurahisha midomo yao na waliowatuma. Ni bora wangetumia muda huu kuhamasisha maendeleo kwa wananchi badala ya kutupigia kelele.

Kwanza hata katiba ya CCM haijakataza mwanachama yoyote kugombea, sasa kelele za nini?

Kitendo cha kutangaza hadharani kwamba fulani atagombea ni kuonyesha kwamba chama, kina mgawanyiko na kimejaa malumbano tena ya hadharani.

Kwanini matamko ya kumuunga mkono Rais Kikwete yasiishie ndani ya chama kwasababu kama kuna watakaompinga nao si watatokea ndani ya chama?


Nadhani wanaotaka kugombea sambamba na Rais Kikwete ndani ya CCM, waachwe wagombee ili Rais Kikwete awashinde kihalali.
 
unajua wameshazoea kwamba mtu wanayemchagua anakuwa yeye ndiye, halafu hawakosei caguo lao lazima lifike miaka kumi madarakani lau kama basi Kikwete anaficha mafisadi, magubeli wakubwa wasio na haya yeye akiwa kama kiongozi wao.
hata mtoto anajua hii nchi imemshinda mzee mzima.. ila safi sana kwa mada hii.
 
swala je wapinzani wanamgombea? watajipanga vipi? lengo lao ni kushinda CCM ama kila chama kushinda kivyake!
Mkuu,
mpaka sasa naona wale waliokuwa wagombea wa ngazi ya urais kwa kupitia vyama vya upinzani wameamua kwenda kugombea ubunge.Sasa sijui tafsiri sahihi nikuwa wameamua kuweka mpira kwapani&daluga shingoni au nivipi?Kwa type ya vyama vya upinzani vilivyoko nchini kwetu na aina za viongozi wake wa ngazi zajuu sidhani kama ipo siku watakuja kuungana.Unafiki,tamaa ya madaraka etc vinauathiri sana upinzani.Ona yaliyotokea Tarime na Mbeya Vijijini.
 
Unajua NIni? Kikwete akisema hatogombea 2010 ndipo tutaona jinsi CCM ilivyogawanyika. Natumaini atatangaza mapema kuwa hana mpango wa kugombea tena..

....aisee Mwanakijiji inategemea sana 'yale makubaliano' yalikuwa ni baada ya Miaka 5 au 10.......
 
Mkuu,
mpaka sasa naona wale waliokuwa wagombea wa ngazi ya urais kwa kupitia vyama vya upinzani wameamua kwenda kugombea ubunge.Sasa sijui tafsiri sahihi nikuwa wameamua kuweka mpira kwapani&daluga shingoni au nivipi?Kwa type ya vyama vya upinzani vilivyoko nchini kwetu na aina za viongozi wake wa ngazi zajuu sidhani kama ipo siku watakuja kuungana.Unafiki,tamaa ya madaraka etc vinauathiri sana upinzani.Ona yaliyotokea Tarime na Mbeya Vijijini.

Naimani kwamba demokrasia inaendelea kukua, ndani ya ccm na hata kwenye vyama vya upinzani. Naamini, Kikwete atatoka madarakani, na vyama vya upinzania vitaelewa sio waanzilishi wa harakati washike madaraka. Na hapo ndipo mabadiliko yatatokea. Nguvu ya kukuza mmea na kuungalia uchanue ndio iwe raha ya mkulima, wakati mavuno yanaliwa na wengi, cha msingi ni kuhakikisha wanakuachia cha kula na mbegu za kupanda mwakani.

Pili swala hapa sio upinzania, kwani ukweli hali upinzani sio mkumbwa hivyo, ila watu wamekaa katikati wanasubiri kuzodoe tu. Hiyo sio sahihi! wanaoyaona mapungungufu washiriki katika siasa za kweli, tuawaache woga! Hapo ndipo mgombea wa kweli wa uraisi atapatikana.

Lakini sidhani kama Uraisi, ndio iwe target ya upinzania ila kuongeza namba ya wabunge ndio msingi! Kwahiyo wajikite huko, ila pia kusimamisha mgombea urahisi makini ni faidi katika kukuza upinzani.
 
Wanaotaka Kikwete agombee 2010, wanaogopa nini? (MwanaHalisi Aprili 15, 2009)

kikwetekampeni.jpg

1. Kuna kundi la watu waoga wanajitokeza ndani ya CCM. Kundi la watu wasiojiamini na wasioamini kuwa Rais Kikwete anaweza kuchagulika tena 2010.

2. Kundi hili lina hofu kuwa Rais Kikwete anaweza kuamua kutokugombea tena 2010 na hivyo kubadilisha kabisa mwelekeo wa kisiasa katika chama hicho na bila ya shaka nchi nzima.

3. Kundi hili limeanza kuonesha dalili ya kutetemeka na kama wapambe wanaoogopa kupoteza ujiko wao limeanza kujitokeza na kuimba wimbo wa “Kikwete mgombea tena 2010 ndani ya CCM”.

4. Ninajiuliza hawa ndugu zetu wanaogopa nini? Ni kitu gani kinawatia hofu hivi kiasi kwamba mapema mwaka huu (miezi mingi tu kabla ya uchaguzi) wameanza kutishwa na sasa wameamua kujionesha wazi kuwa chaguo lao ni Kikwete?

5. Je kwa kujitokeza kwao kusema ‘chaguo lao ni Kikwete’ kunamsaidia Kikwete au kunaonesha udhaifu wake uliopo kuelekea 2010?


Mkuu heshima zako, na hongera kwa kuandika karatasi nzuri sana isipokuwa pamoja na kwamba mimi sio mwanachama wa CCM, nina tatizo sana na baadhi ya hoja zako.

- Kwa mfano, unasema kuna waoga ndani ya CCM na kwamba uoga wao unadhihirishwa na the fact kwamba kwa kutumia haki ya kutoa maoni yao kikatiba ya jamhuri yetu ya kutaka rais wa sasa Mheshimiwa Jakaya Kikwete, agombee tena urais kwenye term ya pili. Woooow! What a political statement?

- Yaaani mkuu unasema kwamba wananchi wa Tanzania, ambao ni wanachama wa CCM, kwa kutoa maoni yao kwamba wanamtaka rais wa sasa aendelee, wanakuwa waoga? I 'm reading this right au ninakosea mkuu? Hakuna anayeogopa anything, simply watu wanatumia haki yao kikatiba, na wewe una haki ya kuamua unamtaka nani ndani ya CCM agombee urais, does that makes you unamuogopa somebody kwa sababu umesema maoni yako leo 2009, miezi nane kabla ya uchaguzi ujao wa rais?

I do not get this, labda unafafanulie kidogo mkuu!


William.
 
CCM siyo Rais!

Mojawapo ya utamaduni mbovu ambao ndugu zetu watetezi wa Kikwete wanataka uendelezwe ni ule wa “kumwachia Rais aliyeko madarakani mihula yake miwili”. Dhana hii ni potofu, ya kibabe na aina mfanano wowote na utawala wa demokrasia. Kama hili lingekuwa zuri wao CCM si ndiyo wana Bunge na wana Rais kwanini wasiamua kubadilisha Katiba na kuweka awamu ya Rais kuwa ni muhula mmoja wa miaka kumi! Maana kama tayari wanataka Kikwete awe mgombea wao 2010 na mtu mwingine yoyote CCM asigombee basi waamue tu kufanya uchaguzi wa wabunge na ule wa Urais uahirishwe hadi Kikwete atakapomaliza awamu yake 2015!

Vinginevyo, CCM hawaodhi nafasi ya Urais wa Tanzania na aliyeko madarakani hana ubia na nafasi hiyo. Nafasi hiyo Kikatiba inashindaniwa kila baada ya miaka 5 na hakuna garantii kuwa ukiwa Rais basi mhula wako wa pili utapewa kwa dezo. Kikwete ni lazima apambanishwe ndani ya CCM kama tulivyofanya 2005 na kabla yake, ni lazima arudishe fomu za kugombea pamoja na watu wengine wanaotaka kufanya hivyo, na ni lazima atetee nia yake hiyo kama alivyofanya 2005. Nje ya hapo, CCM itangaze kuwa Tanzania ni nchi ya Udikteta wa chama cha Mapinduzi!

- Ndani ya CCM kuna wananchi ambao kwa maoni yao, wanaona rais wa sasa anahitaji kuendelea ili amalizie mihula yake miwili, eti kwa kutoa maoni yao haya wanakuwa sio wana-demokrasia? Wanaleta ubabe? Ni wapotofu?

- Wangesema wanataka ibadilishwe katiba ya CCM ili rais wa sasa apite tu, ningeelewa, lakini wananchi wanataoa maoni yao tu bila ya kubadili anything na wala wao sio taifa zima kwamba wanalosema tu linakuwa, sasa tatizo liko wapi hapa?

- Unasema CCM itangaze kwamba Tanzania ni nchi ya kidikteta, just because kuna wanachama wachache ndani ya CCM wanaompenda rais wa sasa wanasema achaguliwe tena? Sasa mkuu wewe na wao hapa nani anakuwa kwenye fine line ya demokrasia? anayesema maoni yake, au mwenye tatizo na maoni ya wengine, badala ya hoja zao?

Mkuu ni haki ya wananchi wa Tanzania, regardless ya vyama vyao vya siasa kuamua na kusema wazi maoni yao kwamba nani wanamtaka awe rais, lakini sio haki yao kubadili katiba ili mgombea flani apite bila kuchaguliwa that is not the case so far ndani ya CCM, ni haki yako kama mwananchi kusema humtaki rais wa sasa na sababu, lakini one thing ni kwamba huna haki ya kuhoji haki za maoni ya baadhi ya wanachama wa CCM, na ningekuomba kiustaarabu uandike karatasi nyingine kuwaomba radhi wale wote wenye mawazo ya kutaka rais Jakaya Kikwete achaguliwe tena kumalizia kipindi cha pili, kwani hapa umeingilia uhuru wao kikatiba wa kutoa mawazo yao bila kuogopa, na ningekushauri in the future usiwatishe wananchi kwa sababu ya maoni yao binafsi, ambayo they have nothing to na taifa wala CCM nzima as chama cha siasa.

CCM kama chama cha siasa wana haki ya kuongea na kusema anything they want, it is nothing kwetu taifa unless wantaka kubadili katiba na kuhalalisha mambo yao ya ndani ya CCM kwenye taifa, otherwise tusikose usingizi kwa sababu ya maoni ya wachache huko ndani ya CCM juu ya chama chao, mbona tunaogopa sana maoni ya wanachama wachache waloiko ndani ya CCM?

Mkuu jaribu kuheshimu haki za wananchi wenzio kikatiba, ni haki yaoa kama yako kikatiba kuamua nani wanamtaka kuwa rais wao, na wewe pia uchague nani unamtaka awe.

Ahsante Sana.

William.
 
Nadhani hapo mwandishi alizungumzia kuhusu: asitokee mgombea ndani ya ccm.
 
- Ndani ya CCM kuna wananchi ambao kwa maoni yao, wanaona rais wa sasa anahitaji kuendelea ili amalizie mihula yake miwili, eti kwa kutoa maoni yao haya wanakuwa sio wana-demokrasia? Wanaleta ubabe? Ni wapotofu?

- Wangesema wanataka ibadilishwe katiba ya CCM ili rais wa sasa apite tu, ningeelewa, lakini wananchi wanataoa maoni yao tu bila ya kubadili anything na wala wao sio taifa zima kwamba wanalosema tu linakuwa, sasa tatizo liko wapi hapa?

- Unasema CCM itangaze kwamba Tanzania ni nchi ya kidikteta, just because kuna wanachama wachache ndani ya CCM wanaompenda rais wa sasa wanasema achaguliwe tena? Sasa mkuu wewe na wao hapa nani anakuwa kwenye fine line ya demokrasia? anayesema maoni yake, au mwenye tatizo na maoni ya wengine, badala ya hoja zao?

Mkuu ni haki ya wananchi wa Tanzania, regardless ya vyama vyao vya siasa kuamua na kusema wazi maoni yao kwamba nani wanamtaka awe rais, lakini sio haki yao kubadili katiba ili mgombea flani apite bila kuchaguliwa that is not the case so far ndani ya CCM, ni haki yako kama mwananchi kusema humtaki rais wa sasa na sababu, lakini one thing ni kwamba huna haki ya kuhoji haki za maoni ya baadhi ya wanachama wa CCM, na ningekuomba kiustaarabu uandike karatasi nyingine kuwaomba radhi wale wote wenye mawazo ya kutaka rais Jakaya Kikwete achaguliwe tena kumalizia kipindi cha pili, kwani hapa umeingilia uhuru wao kikatiba wa kutoa mawazo yao bila kuogopa, na ningekushauri in the future usiwatishe wananchi kwa sababu ya maoni yao binafsi, ambayo they have nothing to na taifa wala CCM nzima as chama cha siasa.

CCM kama chama cha siasa wana haki ya kuongea na kusema anything they want, it is nothing kwetu taifa unless wantaka kubadili katiba na kuhalalisha mambo yao ya ndani ya CCM kwenye taifa, otherwise tusikose usingizi kwa sababu ya maoni ya wachache huko ndani ya CCM juu ya chama chao, mbona tunaogopa sana maoni ya wanachama wachache waloiko ndani ya CCM?

Mkuu jaribu kuheshimu haki za wananchi wenzio kikatiba, ni haki yaoa kama yako kikatiba kuamua nani wanamtaka kuwa rais wao, na wewe pia uchague nani unamtaka awe.

Ahsante Sana.

William.

Nashindwa kuelewa nani haheshimu mawazo ya wengine kati ya MM na hao unaowatetea. Kutoa maoni ni haki ya kila mtu kikatiba, lakini kila mmoja amepewa utashi wa kupima busara za maoni yake, tunajadili uhalali wa hayo mawazo kwa jamii yetu na kutaka kulazimisha maoni yenu kuwa ndio ya watanzania wote si jambo la kuvumiliwa.Mara chache inatokea watu wachache wanaweza kuwa wapo sahihi kuliko wengi, wakiweka bayana hoja zao, bila shaka wapo watakaoukubali ukweli wa mawazo yao. Hoja za wazee wako kuhusu maoni yao ni dhaifu na ni maoni ya wengine pia ni bora wanyamaze kuliko kuendelea kujivunjia heshima zao hadharani. Utaratibu wa kutoa maoni na kuheshimiwa hauwi halali tu pale wazee fulani wanapoongea, ni bora ungeheshimiwa kwa wote, na kama utaratibu huo ungekuwepo CCM na katika utawala wa nchi hii, tusingekuwa hapa tulipo.
Tatizo lenu mnataka kuona kuwa nchi hii ni ninyi peke yenu wenye uhalali wa kuita press conference nyumbani kwenu au pale maelezo na kusema chochote mlichoota kwa maslahi yenu au ya familia zenu, na mkitaka watu wasifie kwa kuwa mmezoea hivyo. Ninaamini ipo siku watanzania watakuwa tofauti, ilichukua miaka mingi kukomesha mifumo yote ya kinyonyaji katika historia, ninaamini muda si mrefu mfumo huu wa kinyonyaji uliotawala Tanzania mpaka sasa na kutufikisha katika hali hii utakufa natural death.
 
- Ni wapi CCM wamebadili au wameomba katiba kwa kutumia hii hoja yako mkuu, na kutaka asitokee mgombea mwingine ndani ya chama chao?

William.


Nimesoma maandishi ya mwanakijiji, nadhani yupo katika hali ya kujiuliza zaidi kwanini kampeni za kikwete kuwa mgombea zimeanza mapema hivi? Ila, tunaweza kumuuliza amezilinganisha na wakati gani? Pia anajuuliza thamani za kura za wananchi katika muda wa Uraisi wa kikwete ni zipi kumrudisha temu ya pili!. Kwa maoni yake mabadiliko ni ya kuhesabu. Sasa, uchaguzi unaokuja, anajaribu kuwafanya wanachama wafungue macho kuuliza utamaduni wa ccm! Je upembuzi wake ni wa kweli! Hilo ni swali tofauti kabisa. Je anahaki ya kutoa mawazo yake! hell yes, given the present context
 
1.
mpigafilimbi;

Nashindwa kuelewa nani haheshimu mawazo ya wengine kati ya MM na hao unaowatetea. Kutoa maoni ni haki ya kila mtu kikatiba,

- Sawa sawa, hapa tuko pamoja kila M-Tanzania ana haki ya kutoa maoni yake.

2.
lakini kila mmoja amepewa utashi wa kupima busara za maoni yake,

- Sijakuelewa, nilifikiri hapo hoja inatakiwa kua kila m-Tanzania ana haki ya kuuliza validility ya hoja ya mwananchi mwignine, lakini sio kuingilia haki ya kutoa maoni yake!

3.
tunajadili uhalali wa hayo mawazo kwa jamii yetu na kutaka kulazimisha maoni yenu kuwa ndio ya watanzania wote si jambo la kuvumiliwa.

- Unaona sasa, hivi hao wanachama wachache wa CCM, wamemlazimisha nani kukubali mawazo yao kwamba lazima rais wa sasa aendelee? Ni wapi wamejaribu kubadili katiba?

- Halafu unaita maoni yenu, si unaona ubabe huu ambao mnadai hamuutaki, maana anayejaribu kuwa-question na hizi ideas basi na yeye ni maoni yenu, something is not right na hizi thinking na wala haziwezi kutusaida sisi wananchi at large.

3.
Mara chache inatokea watu wachache wanaweza kuwa wapo sahihi kuliko wengi, wakiweka bayana hoja zao, bila shaka wapo watakaoukubali ukweli wa mawazo yao.

- Sawa sawa.

4.
Hoja za wazee wako kuhusu maoni yao ni dhaifu na ni maoni ya wengine pia ni bora wanyamaze kuliko kuendelea kujivunjia heshima zao hadharani.

- Unajua ni afadhali kwamba wazazi wako hawajasema kabisa, maana kama mawazo yao ni kama haya yako, ya ubabe ubabe na name calling basi wana busara sana kutosema anything, pole sana mkuu!

5.
Utaratibu wa kutoa maoni na kuheshimiwa hauwi halali tu pale wazee fulani wanapoongea, ni bora ungeheshimiwa kwa wote,

- Hebu rudia maneno yako mwenyewe, hata sielewi unachosema, wewe ndiye uansimamkia uhalali wa maoni ya wananchi? toka lini mkuu?

6.
na kama utaratibu huo ungekuwepo CCM na katika utawala wa nchi hii, tusingekuwa hapa tulipo. Tatizo lenu mnataka kuona kuwa nchi hii ni ninyi peke yenu wenye uhalali wa kuita press conference nyumbani kwenu au pale maelezo na kusema chochote mlichoota kwa maslahi yenu au ya familia zenu, na mkitaka watu wasifie kwa kuwa mmezoea hivyo. Ninaamini ipo siku watanzania watakuwa tofauti, ilichukua miaka mingi kukomesha mifumo yote ya kinyonyaji katika historia, ninaamini muda si mrefu mfumo huu wa kinyonyaji uliotawala Tanzania mpaka sasa na kutufikisha katika hali hii utakufa natural death.

- Unaona kumbe ni yale yale, jina tofauti maneno yale yale naona mkuu una muda mwingi sana na chuki flani za binafsi, maana hapa unaonyesha rangi zako wazi, kwamba huna haja ya mjadala wa hoja ila ubabe na kutafuta ushujaa at the wrong place na the wrong persona, mimi sitishiki na hizi kelele zako za mlango, ambazo umekwua ukizirusha siku nyingi sana na recently naona una neno wazazi wako kama vile unawafahamu.

- Mkuu si unajua vizuri sana kwamba kati ya mimi na familia yangu na wewe nani hasa ni mwizi na mtapeli, kweli unataka nirudie tena hapa mbele ya umma? si iatkuwa aibu ndugu yangu. Ni mara nyingi sana nimekupa nafasi useme wizi wangu, ufisadi wangu, na wa familia yangu uweke hapa wazi wananchi wote wauone, mara ya mwisho ulisema wazazi wangu wanamteeta Kikwete kwa sababu sisi wote tunafanya ubalozini, nikakuomba useme ni ubalozi wa wapi hukujibu tena, sasa here you are again,

Hizi ndio zinaitwa kelele za mlango, yaani uongo uongo na uzandiki, hauwezi kulisaidia taifa letu hata siku moja!

Ahsante.

William.
 
1. Nimesoma maandishi ya mwanakijiji, nadhani yupo katika hali ya kujiuliza zaidi kwanini kampeni za kikwete kuwa mgombea zimeanza mapema hivi?

2. Ila, tunaweza kumuuliza amezilinganisha na wakati gani?

3. Pia anajuuliza thamani za kura za wananchi katika muda wa Uraisi wa kikwete ni zipi kumrudisha temu ya pili!.

4. Kwa maoni yake mabadiliko ni ya kuhesabu.

5. Sasa, uchaguzi unaokuja, anajaribu kuwafanya wanachama wafungue macho kuuliza utamaduni wa ccm!

6. Je upembuzi wake ni wa kweli! Hilo ni swali tofauti kabisa.

7. Je anahaki ya kutoa mawazo yake! hell yes, given the present context

- Kwa nini kampeni za urais wa Kikwete zimeanza mapema? Kwani katiba yetu inasema nini on time na kampeni za uchaguzi wa rais? Miezi minane kabla ya uchaguzi ni mapema?

- Swali la thamani za kura za wananchi, linawahusu CCM? anajaribu kuwafumbua maco wananchi kwa kuwaita waoga, wapotofu, na madikteta kwa sababu maoni yao hayakubaliani na yake?

Off course ana haki kama wanachama wa CCM ambao hataki mawazo yao walivyo na haki hiyo hiyo kikatiba, asichokuwa nacho na ninachokipinga na alichokifanya, yaani kuuliza haki yao kusema wanachoamini, kwamba rais wa sasa anafaaa aachiwe nafasi kuendelea, mimi ninafikiri kwamba tunajikanyaga sana, tunajidai tunajua kuwa dawa ya CCM iko karibu au imefika kumbe tunajidanganya na tunaonyesha kwa maneno yetu wenyewe, haiwezekani tukakosa usingizi kwa sababu ya maneno ya wachache ndani ya CCM, wananchi wa Tanzania sio wajinga sana kama wengi hapa tunavyofikiri.

Kila siku tunajadili CCM weee, lini tutajadili our creatiion, lini tutajadili our alternative? I mean hakuna taifa duniani limewahi kupata mabadiliko na this kind of thinking, matendo hakuna mimi nilifikiri leo tutakua tunaongea mgombea tunayemuamini kwamba anaweza kumng'oa rais wa sasa, ambaye sio CCM, badala yake tunajaribu kuwazunguka watawala eti kwa mawazo kwamba huenda wakameguka au kugombana, hiyo haitakuja kutokea ndani ya CCM, never! na kama hiyo ndio our only hope basi tumekwisha kabisaa.



William.
 
Mkuu FMES,
Mimi kinachonishinda kuelewa ni hawa wanaopinga (kina Mwanakijiji) kinawaogopesha nini wao ikiwa kuna kundi la watu wamesema Kikwete ndio Chaguo lao?..
Mimi nikisema Chaguo langu ktk kugombea kiti cha rais ni Dr. Slaa na hafai kuwa na Mpinzani.....kuna tatizo?..Je, kuna kitu naogopa au ndio chaguo langu mimi na sidhani kuna ulazima wa kuonyesha ame accomplish vitu gani kuweza kupata sifa hiyo..
Kusimama kama mgombea ni sifa inayotokana na sifa za Uchaguzi, nani anafaa kuwa rais ni Chaguo la wananchi wote wala sii swala la viongozi wa CCM, Spika wa Bunge au Mkandara..

I mean hizi hofu za Kikwete kuchukua awamu ya pili kunatokana na kitu gani?.. Je ni sisi wenye wasiwasi kwamba Kikwete anaweza kuchukua tena ikiwa hatapata ushindani ndani ya CCM?..Na kama kuna ushindani ni mtu gani tunayefikiria anaweza kuyatimiza mapungufu yote tuliyoorodhesha!..ukiuliza hivyo unaambiwa wapo wengi KINA NANI?.. Je, mmeweza kuongea nao wakasema watatizmiza yote aloshindwa Kikwete?.. hapana!..

Mkuu wangu hata nashindwa kuwaelewa Wabongo, waliosema wana sababu kubwa kwamba hawataki kubadilisha Nahodha hata kama anawapoteza kwa sababu hawaoni nahodha mwingine anayeweza kuongoza na jahazi lao..
Kama wewe ni msafiri na umo ktk jahazi hilo huwezi kupinga tu kuendelea kwa nahoidha huyo wakati wewe sio tu huwezi kuongoza jahazi huna mtu yeyote ambaye yuko tayari kuongoza. Mtu ambaye wasafiri wengine pamoja na mashaka yao wanaweza sema.. KWELI huyu Kikwete ameshindwa, hatutafika huko tuendako bora huyu ambaye anaonekana anafahamu tunakotaka kwenda.

Wanabodi,
Jamani eeeh, nchi yetu imekosa mwelekeo sii jana wala juzi. tanzania leo inaongozwa bila dira na Kikwete kama nahodha yeyote yule hawezi kufanya maajabu ikiwa hana dira na yeyote mtakayemleta kugombea dhidi yake hataweza kuongoza kwani CCM hawana dira tena...wote wanahaha iwe Kikwete kurudi au kuondoka!

Jibu rahisi sana Chagueni Chadema.. Chama ambacho kimejizatiti kurudisha dira ya Taifa... chama kitakacho ongoza kwa kufuata MWONGOZO wa taifa letu hatua kwa hatua hivyo mnafahamu kabisa nini nafasi ya mchango wenu kama wasafiri.
 
Mkuu heshima zako, na hongera kwa kuandika karatasi nzuri sana isipokuwa pamoja na kwamba mimi sio mwanachama wa CCM, nina tatizo sana na baadhi ya hoja zako.


William.

Mkuu you should mean it. Wayahudi waliomuua Yesu walimtambua Petro kama mfuasi wa Yesu kwa kauli zake na mwendo wake japo walipomuuliza akili kuwa ni mwanafunzi wa Yesu alikataa kuwa hamjui Yesu. Mkuu japo unasema sio mwanachama wa CCM, hoja zako zinakusuta. samahani kwa kutumia mfano huo kama utakwazika.
 
bm21,
Mkuu Wayahudi nao kamba sana, wee utakwenda kumuuliza mtu kama ni mwanafunzi wa Yesu wakati kisha mkata askari wako sikio!!..mmmhhnnn!
Sidhani kama kuna mjadala kuhusiana na William!
 
Kila siku tunajadili CCM weee, lini tutajadili our creatiion, lini tutajadili our alternative? I mean hakuna taifa duniani limewahi kupata mabadiliko na this kind of thinking, matendo hakuna mimi nilifikiri leo tutakua tunaongea mgombea tunayemuamini kwamba anaweza kumng'oa rais wa sasa, ambaye sio CCM, badala yake tunajaribu kuwazunguka watawala eti kwa mawazo kwamba huenda wakameguka au kugombana, hiyo haitakuja kutokea ndani ya CCM, never! na kama hiyo ndio our only hope basi tumekwisha kabisaa.

Well stated! Ironically, you are walking on the same path of criticism without providing alternative. Just a reminder, in the coming election different people will have different roles, which to some starts from now. Some to shape public opinion, control perceptions, lying to people, while other fundraise and do ground work for campaigns. Parties using their electro machine will select and bring the candidates to the public. Then, I from the public i can listen to their propaganda and later vote.

Personally, since i am not in any political party, I don't have anyone in mind yet, i roughly like Mwandosya with no basis! I can still be open to kikwete if he redefine his position. So, any discussion of CCM politics enrich my position as well as any other candidate from opposition parties. However, recently i have an imaginary candidate - a woman or a candidate from opposition. Much will depend on their positions, strategies and agenda for social change, which must include peasants, education, and mining - then look into their credibility and capacity to deriver.

Different from previous years, in the coming election, i am going to campaign for the candidate of my choice to make his agenda clear to the public, and make sure i contribute to realization of presidential debates to make sure the intellectual capacity of our president is on test for once.

Currently, i am thinking of what agendas should get my votes, and i am going to have 50 voters who i am going to convince to vote to the candidate i prefer. That is the commitment i am going to live for.

So what are you going to do!
 
Kela.. na hiyo nimeirudia mara kadhaa na ukweli wake ninaanza kuona kama katika ukungu. Je yawezekana kuna mtu alikuwepo 2005 ambaye Watanzania hawakumpa nafasi na ambaye leo hii akiamua kugombea 2010 anaweza kumuangusha Kikwete?

Mkuu Mwanakijiji, mada yako inavutia sana, inatoa changamoto na kujaza hisia nyingi. Inauliza yasiyojibiwa na kusisitiza yanayohitajika.

Mkuu, kweli inaelekea tulikosea kumpa kura Kikwete 2005. Tulikosea, na kunawanaojua kuwa tulikosea kabla sisi wenyewe hatujajua hivyo. Kauli za viongozi, wabunge na wastaafu wa CCM zinaashiria kuwa wanatambua kuwa tulikosea na wanaogopa/wanahisi kuwa hatutakosea tena. Kauli zao zinaashiria kuwa wasipotishia wanaCCM wenzao wenye uwezo wa kuongoza/kutoa changamoto kwa Rais aliepo madarakani ifikapo 2010, basi JK anaweza kupoteza kiti cha uRais na wao wakapoteza mshiko walionao. Kauli zao pia zinaashiria kuwa, wanajua kuwa wao hawana nafasi ya kushika wadhifa wa uRais wa Tanzania (muda wao umekwisha) na wanataka kufaidika zaidi na utawala uliokosa mwelekeo uliopo madarakani.

JF ni moja ya sehemu ambazo ufahamu/elimu na changamoto nyingi hutolewa. Inabidi kuongeza upana wa usambazaji wa taarifa ili ziweze kufikia umma mkubwa wa waTanzania. Nafahamu kuwa wengi wanajua nchi inavyokwenda, na hawapendezwi nayo. Ila ni rahisi kwao kushawishika kukosea tena kwenye uchaguzi ujao endapo hawatapewa changamoto na ufahamu wa jinsi ya kufanya mabadiliko yanayohitajika.
 
Lakini wandungu,Tanzania si kuna mfumo wa vyama vingi vya siasa??Sasa kama JK 'kashindwa' kuwa na vision ktk uongozi wake na still akapendekezwa na chama chake kugombea tena 2010 si ndio itakuwa fursa nzuri kwa wapinzani kushinda?Sasa haya ya kusema asigombee ni kama mnakuwa mnamuogopa tu.Yan timu pinzani waingize kikosi kibovu uwanjani then kuna cha kulalamika hapo.Mi naona ndo pa kutake advantage na kuwabwaga chini.

Mkuu 911, suala si agombee Kikwete ili upinzani ushinde au ushindwe. Suala ni kuwa na wagombea wa uRais wanaoweza kuleta mafanikio yanayohitajika kwa Taifa hili masikini na lenye utajiri mkubwa (naamini ninaeleweka kusema hivi). Tufahamu tu kuwa, mgombea yeyote anaweza kuwa Rais wa nchi hii (awe wa CCM au chama kingine chochote). Tunachotaka kuwa nacho ni wagombea wenye ubora usio na mashaka (kutoka kila chama kinachokusudia kushiriki). Tunataka mtu yeyote anaetaka kuongoza nchi awe na uwezo mkubwa wa kufanya hivyo (si kwa CCM tu).

Hata wapinzani wanatakiwa wawe makini (kama inavyotakiwa kuwa CCM) katika kuteua/kuchagua mgombea atakaewawakilisha katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vyama vyote vinatakiwa kuruhusu demokrasia kutawala ili kupata mgombea wao (sio kama afanyavyo Mrema).
 
Back
Top Bottom