Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,020
- 4,027
Kwanza naheshimu serikali na natambua juhudi yake katika kuhudumia wananchi, kulinda na kudhibiti taarifa zao.
Zamani sehemu ya huduma kwa jamii ambayo ilikuwa na usumbufu namba moja ilikuwa ni RITA (cheti cha kuzaliwa) lakini siku hizi namba moja kwa usumbufu ni NIDA.
Niliwahi kuandika humu kuwa NIDA ni kama vile hawajiamini au hawatuamini kwa sababu haiwezekani mfumo wa online wameutengeneza wao kisha mtu akiutumia kuomba huduma halafu akaenda ofisini kukamilisha hatua zingine anaambiwa arudi kwa mtendaji akaanze upya maana hii ya online haitambuliki. Sijui kama lilifanyiwa kazi hili lakini tuache huko kwa leo nina lingine kuhusu NIDA
NIDA bwana wana huduma yao ya kuuliza namba ya mtu online. Ajabu ni kwamba huduma hiyo ipo kama bosheni tu maana sijawahi kuona nikifanikiwa kuona namba ya NIDA humo hata siku. Utarukaruka wee humo lakini mwisho lazima uambiwe utembelee ofisi za NIDA
Wengine tupo mbali na ofisi hizo za NIDA lakini wengine kula yao inategemea kwa namna moja ama nyingine huduma fulani fulani ambapo mteja ataulizwa namba ya NIDA. Sasa kuna watu hiyo namba haipo tu akilini mwake mpaka kutokee matumizi ya dharura kama hivyo. Imagine mteja unamkosa kisa haijui namba yake ya NIDA na kikaratasi ameacha nyumbani au hajui kaweka wapi
Kuna ile njia nyingine ya kutumia kuomba kwa njia ya sms nayo sijaona ufanisi wake kwakweli
Rekebisheni na boresheni