Nichukue hatua gani za kisheria dhidi ya benki ya CRDB?

SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,623
2,015
Habari zenu wadau.

Nimesikitishwa na huduma mbovu za benki ya CRDB. Ukweli siku ya juzi nikiwa safarini kuna mtu alinipigia simu alikuwa na uhitaji wa haraka wa fedha kiasi. Na wakati huo huyo mtu alikuwa ananidai kiasi fulani cha pesa.

Sasa kwa uhitaji wake wa haraka akaniomba kama niko vizuri nimurudishie hela yake na pia nimuongezee amount nyingine ili aweze kutatua changamoto aliyo nayo.

Kwa kuwa niko safarini nisingeweza kwenda kutoa fedha benk halafu niende kumwekea huyu ndugu ambaye akaunt yake iko NMB.

Nikaona isiwe tabu, nikaingia kwenye app ya crdb kwenye simu janja yangu nikahamisha pesa kutoka CRDB kwenda nmb wastan wa kama 1m hivi (siyo exact figure).

Cha ajabu, sikupokea sms ya kuonyesha kuwa nimefanya muamala, na hela kwenye account imeshaenda, na mhusika hajapokea hela. that was tarehe 3, leo ni tarehe 5 mhusika bado hajapata hiyo hela.

Jana siku nzima nimesumbuana na watu wa CRDB. Kwanza nilianza kwa kumtumia mtu anayefanya kazi CRDB. Nilipoona sipati majibu ya kuridhisha nikaamua kupiga namba yao ya customer care. Ubovu wa huduma zao ukiwapigia simu jiandae kusubiri siyo chini ya dakika 10 unasikiliza nyimbo na matangazo yao.

Haya, alipopokea ananiambia sorry system ilikuwa down jana ila wanairekebisha soon. siku ya jana ikapita bila bila. Leo tena nimepiga story kama zile za jana. Now i feel embarrassed naona uvumilivu unataka kunishinda na mhusika alikuwa na dharura kubwa sana ndio maana niliona nimuhamishie haraka, kumbe ndo hasara.

Hivi nikiwafungulia kesi ya madai nitakuwa nimekosea? How comes wanakaa na pesa ya mtu kwa zaidi ya masaa 48 bila taarifa? Na mimi nawatafuta wananipigisha story za kusema soryy, sorry for what? Do they undeerstand damage wanayosababisha kwa mteja?
 
Kwa kifupi huduma nyingi kwa taasisi za umma ziko chini , nilipewa control number toka NHIF Nilipie sasa kwa wiki 2 kila nikijaribu kulipia inakataa na mda huo namba yao haipatikani.

Jana wanapatikana wananiambia sory hio control number kuna namba mbili zilizidi.

Najaribu kukuonesha tu jinsi tunavyohainga na taasisi zetu ila kifupi tuanze kushtaki tu akili ziwakae sawa
 
Nilichokigundua mimi nikwamba haya mabank na mitandao ya simu walianzisha mambo yakurahisisha huduma kabla hawajajipanga vizuri ili watoe huduma kwa ufanisi.Ukiamini hizi huduma iko siku utakwama na hutapata msaada wowote.Pole sana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nguvu ya kuwashitaki ilikuwepo kama una tuma CRDB kwenda CRDB.

Unaweza sema tatizo la crdb, kumbe ni la benki nyingine.

Pia usisahau Kuna mikataba mingi kwenye haya mashirika/makapuni makubwa. unaweza kukuta mtoaji wa huduma za network ni kampuni nyingine na iko labda England so ukifungua kesi jiandae kwa ghaama kubwa ya pesa na muda, na ukaja daiwa fidia wewe.
 
Juzi, nmetoa fedha benki, Salio lilisoma laki moja kabla sijaanza kutoa kidogokidogo..nikatoa 10000 Kisha baadae nikatoa 20000 Kisha nikatoa 10000 Kisha nikatoa 25000 baadae ya nikaambiwa Salio langu ni elfu mbili tu baada ya kuangalia Salio

Kwa hiyo ukiwa na 100000 ukatoa 65000 gharama ya tozo na ada za benki ni 350000 (2000)

Jaman huu ni wizi, ni wizi wa adharani anayeiba sasa daaah sijui tunakimbilia wapi

Mchele 3500 @ 1kg
Unga 2200@1kg
Yaaani yaaani daaah
 
Nguvu ya kuwashitaki ilikuwepo kama una tuma CRDB kwenda CRDB.

Unaweza sema tatizo la crdb, kumbe ni la benki nyingine.

Pia usisahau Kuna mikataba mingi kwenye haya mashirika/makapuni makubwa. unaweza kukuta mtoaji wa huduma za network ni kampuni nyingine na iko labda England so ukifungua kesi jiandae kwa ghaama kubwa ya pesa na muda, na ukaja daiwa fidia wewe.
Mimi nadhani ni uelewa mdogo miongoni mwetu sisi watanzania. Kama mtoaji huduma za network ni mwingine wao wanatakiwa wamuwajibishe mtoaji huduma. Kuna mambo sisi tunachukulia poa ila kwa Nchi za wenzetu hakuna huu upuuzi, ndio maana wenzetu unaona mtu anaenda kushtaki na kudai fidia kibao kwa jambo ambalo sisi tunaona kawaida.
 
Juzi, nmetoa fedha benki, Salio lilisoma laki moja kabla sijaanza kutoa kidogokidogo..nikatoa 10000 Kisha baadae nikatoa 20000 Kisha nikatoa 10000 Kisha nikatoa 25000 baadae ya nikaambiwa Salio langu ni elfu mbili tu baada ya kuangalia Salio

Kwa hiyo ukiwa na 100000 ukatoa 650000 gharama ya tozo na ada za benki ni 350000 (2000)

Jaman huu ni wizi, ni wizi wa adharani anayeiba sasa daaah sijui tunakimbilia wapi

Mchele 3500 @ 1kg
Unga 2200@1kg
Yaaani yaaani daaah
Tulia uandike vizuri, una 100000 unatoaje 650000?
 
Mimi nadhani ni uelewa mdogo miongoni mwetu sisi watanzania. Kama mtoaji huduma za network ni mwingine wao wanatakiwa wamuwajibishe mtoaji huduma. Kuna mambo sisi tunachukulia poa ila kwa Nchi za wenzetu hakuna huu upuuzi, ndio maana wenzetu unaona mtu anaenda kushtaki na kudai fidia kibao kwa jambo ambalo sisi tunaona kawaida.
Nchi za wenzetu wana hii 'Customer Service Agreement'

Hii ikija kwetu huku mashirika kama Tanesco, kufirisika ni lazima. Kukata umeme bila kutoa taarifa, unalipa fidia.
Wawekezaji wengi wataingia mitini
 
Nguvu ya kuwashitaki ilikuwepo kama una tuma CRDB kwenda CRDB.

Unaweza sema tatizo la crdb, kumbe ni la benki nyingine.

Pia usisahau Kuna mikataba mingi kwenye haya mashirika/makapuni makubwa. unaweza kukuta mtoaji wa huduma za network ni kampuni nyingine na iko labda England so ukifungua kesi jiandae kwa ghaama kubwa ya pesa na muda, na ukaja daiwa fidia wewe.
Kampuni ya Airtel imepandishwa kizimbani ikidaiwa fidia ya Sh490 milioni kwa kuitumia sauti ya Nixon Bandago Haule kwenye tangazo la ‘Airtel the Smartphone Network.’

Kesi hiyo imefunguliwa na Haule Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam anayedai sauti inayosikika katika kaulimbiu hiyo na kutumika katika matangazo ya kibiashara ya Airtel ni yake lakini hakutoa ridhaa itumike.

Kwa mujibu wa hati ya madai, kiapo na nyaraka nyingine alizoziwasilisha mahakamani, Bandago anadai kuwa aliingia makubaliano ya awali na ofisa wa Airtel aitwaye Arnold Madale Oktoba mosi mwaka 2017 na baada ya kurekodi sauti aliambiwa asubiri iidhinishwe na menejimenti ili wasaini mkataba jinsi itakavyotumika, muda na haki nyinginezo anazostahili.

Katika hali ya kushangaza, anasema alianza kuisikia kaulimbiu hiyo yenye sauti yake katika vituo vya redio na runinga bila makubaliano yoyote kufanyika hivyo anaiomba mahakama iamuru kuwa mdaiwa alivunja hakimiliki zake.

Sh490 milioni za fidia anayoiomba zinajumuisha Sh390 milioni za hasara aliyoipata kwa ukiukaji huo wa haki miliki na Sh100 milioni kama riba.

Katika majibu yake, Airtel imekana kuwa na mkataba naye wa kutengeneza tangazo hilo isipokuwa ina mkataba na kampuni ya Oglivy Tanzania Limited tangu Novemba 18 mwaka 2015 kwa shughuli zote za masoko na matangazo ya kibiashara kwenye vyombo vya habari.

Airtel imesema Mandago aliingia mkataba na kampuni ya Oglivy Mei 10 mwaka 2018 na akaridhia sauti yake kutumiwa na Oglivy na au wadau wake kwenye matangazo yake na katika kampeni zake za kibiashara kwa malipo ya Sh600,000 jambo ambalo Mandago anasisitiza alikuwa ofisa wa Airtel.
 
Toka aondoke kimei crdb imekuwa ya kipumbuvu sana

Huyu mkurugenzi mpya ataiua hii benki akiendelea kuwepo pale

Acha weendelee kutangaza faida za uongo
Jamaa hua anazunguka na Rais kwny kila ziara mpk unajiuliza huyu Jamaa Ni mtumishi wa serikali au?
 
Siyo equity ya zanzibar, Kuna wafanyakazi hata kusoma kilichoandikwa wakaelewa ni mtihani. Yaani wameniudhi sana halafu wana majibu ya hovyo wakiona wewe siyo mwarabu.
Mkuu wafanyakazi watakuwa wazanzibari mkuu elimu kwao ni mbingu na ardhi.
 
Benki ya nini, mimi pesa zangu naweka nyumbani!

Shida kwa TARURA wanabambia gharama za parking, nikiwahita wahuni sijui kama nitakuwa nimekosea!
 
Back
Top Bottom