Msaada wa kisheria: Benki ya CRDB wamenikata mshahara pasipo kunipatia mkopo

tactician

Member
Feb 16, 2020
6
10
Mimi ni mtumishi katika mkoa mmoja hapa Tanzania, Mwezi wa 5 mwaka Jana niliomba mkopo katika benki ya CRDB, lakini wakachelewa kunipatia mkopo wakisema mwajili wangu hakuidhinisha makato,mwisho nikawaomba tuahilishe zoezi la mkopo na tukakubaliana.

Ajabu ni kuwa kumbe Mwajili aliidhinisha makato na akayaweka ktk saraly slip yangu hivyo crdb walipaswa kunipatia mkopo lkn hawakufanya hivyo, Baadae nikaenda nmb kuomba mkopo nikijua crdb tulishaachana.

Ndiyo Mwajiri akagomea kunipitishia mkopo mpya akidai nimeshachukua CRDB na akanionyesha saralyslip yenye makato kwamba CRDB wamenipatia, ikabidi awasiliane na crdb kujua Kama hawajanipatia mkopo husika.

Crdb walikili kutonipatia mkopo na wakaahidi kunipatia pesa waliyoikata pamoja na barua ya kuomba radhi,lkn Hadi leo hawajafanya hivyo, Nakusudia kwenda mahakamani kudai Fidia kwa kuanza kunikata bila kunipatia mkopo wangu.

Pia kukaa na pesa yangu bila idhini yangu,,Ushauri wa kisheria Tafadhali
 
Bank ya CRDB wamenikata mshahara pasipo kunipatia mkopo, msaada kwa wanasheria hapa.

Mimi nataka kudai fidia, wao waliwahi kukili kunikata na kurudisha hayo makato lakini hawakufanya hivyo, msaada tafadhali.
 
Fuatilia huko huko benki; watakurudishia. Ingawa utapata pia usumbufu. Na kama unataka msaada wa kisheria, basi wasubiri mawakili wasomi waje kukupa mwongozo.
 
CRDB Haiwezi Kulalamikiwa Namna Hiyo Lazima Uongozi, Watumishi Kuna Shida Kubwa Sana
 
Hapo kwa haraka haraka inaonekana shida ilikua urasimi kwa upande wa mwajiri wako
 
Crdb mikopo kwa watumishi wa umma is not their priority, ndio maana urasimu mwingi sana ,
Mara
1.mshahara upite kwao
2.makato kabla ya mkopo around 6%
3.penalty for early paymenter
4.kuchelewa kupata mkopo wako
5.mkataba wa mangungo wa msovero -umeegemamia upande mmoja tu wa mkopaji huna balance btn mkopaji na mkopeshwaji I mean in terms of defaulters
6.Riba ya kijanja janja sana ,


Watumish wenzangu mikopo haisaidii Bali ni furaha ya muda tu ila kilio utalia sana,
Kwa hiyo ni Bora kukopa kwa busara hivi ukijibana miezi 3 ukalima/biashara Kisha ukapata mtaji wa 3mils alafu ukapa 3mils for 1.5 or 2yrs haina maumivu
Njaa isikupeleke Bank kopa kwa busara hasa wa take home 400k ukujichanganya mikopon utalia ww hadi ndugu zako watakukumbia
 
Kama upo Temeke nenda pale mahakama jumuishi ulizia chumba cha msaada wa kisheria utasaidiwa changamoto yako
Kama upo Kinondoni nenda pale Makamani ulizia chumba cha msaada wa kisheria
Nenda Biafra karibu na kanisa la Kinondoni Revival Church kuna kituo kinatoa msaada wa kisheria bure watakusaidia...hizo sehemu zote nilizo kutajia utapata msaada bure.

Asante.
 
Back
Top Bottom