Hawahami Chochote, Hawana Pesa Ni ajabu Kuona Kiongozi anayedhani Wananchi kukosa Fedha na ajira Ni Nidhamu! Hata zile za Mwenge alizoziamuru zirudishwe? Peengine zingekuwa Economic Stimulus! Nchi Zenye Viongozi Wenye Ubongo Ulio Kichwani, Mzunguko wa Fedha Ukifa, Wachapisha Fedha Kiasi, Wanaanzisha Miradi ya Ndani ambayo Itanunua Vifaa Vitengenezwavyo Nchini, Na Kuajiri watu wa Kawaida hata kama ni kwa Muda, Na Miradi itakayotapakaa Katika Kila Kona ya Nchi. Hatua ya Juu zaidi Ni Kuwapa Watu (Familia) Fedha Moja kwa Moja (Reverse Tax, au Tax Return) Kwa Imani wakienda Kuzitumia Watajump start Demand, Uzalishaji na Ajira. Lakini Porojo za hawa wetu Ni Kusema, "Watalimia Meno" Sitaki ni Mseme aliyesema Maneno haya!