Ni Watanzania wanaopinga na wengine kuukubali mkataba, mjadara usiwe ni Dini zinatofautina!

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,783
3,281
Mali zote za nchi hii ni zetu sote watanzania bila kujali dini zetu

Hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine kwenye Mibaraka ya Mungu juu ya nchi yetu Tanganyika

Tunaweza kutofautiana kwenye Imani, lakini hiyo haiondoi Utanzania wetu

Hatuna nchi nyingine zaidi ya hii tuliyopo sasa, sote ni watanzania wenye dini mbalimbali

Mjadara uliopo ni kuhusu Mkataba kati ya Bandari zetu Watanganyika na kampuni ya DP word na siyo kati ya dini na dini, na wananchi ndio wanaotoa maoni!

Tunaokutana kwenye huu mjadara, ni wa Tanganyika na kinachotufanya tuzungumze ni Mkataba unaohusu nchi yetu hauna uhusiano wa dini

Nasikitishwa na baadhi ya nyuzi zinazofunguliwa zikihusisha Imani moja na Imani nyingine!

Huku ni kupotoka, kwani wanaopinga na wenye kuutetea huu mkataba ni watanzania, na wote wako sawa!

Ya nini tupambanishwe tena kijinga?

Akipinga mzee Ponda, amepinga mtanzania, akipinga Lissu, amepinga mtanzania, kwa nini maoni ya watanzania yahusishwe na dini?

Huu nao ni ujinga kama ujinga mwingine
 
Back
Top Bottom