Kutokana na hali ilivyo kuhusiana na mkataba tata wa DP World, ni wakati sasa viongozi wetu wa Dini kutafuta ukweli halisi wa jambo hili.
Ni wakati sasa wa viongozi wetu wa Dini kusimama katikati kati ya Serikali na Wananchi na kuishauri Serikali kuachana kabisa na mkataba huu wa DP World kwa sasa na kwa upande mwingine kuwaeleza waamini ukweli uliopo.
Yafuatayo naomba viongozi wetu wa Dini wayafanye haraka iwezekanavyo:-
1. Wakae na viongozi wa Serikali na kuwauliza ni kwa nini wanataka kubadilisha/kufuta sheria zinazolinda Rasilimali zetu za Nchi?
2. Kwa upande wa mkataba tata wa DP World, waitake Serikali kusitisha mara moja mkataba huu ili kujipa muda zaidi wa kuujadili.
Watanzania tunataka viongozi wa Dini wasio wanafiki na wasio waoga.
Kama kuna Kiongozi wa Dini anaogopa kusema ukweli juu ya mwenendo wa Serikali yetu hasa katika suala la DP World, huyo hafai hata kidogo, na atupishe.
Tunataka kuanzia sasa sisi waamini kila Ijumaa, Jumamosi na Jumapili tukiwa Misikitini na Makanisani tuanze kusikia msimamo wa viongozi wetu wa Dini kuhusu Mkataba wa DP World.
Kama viongozi wetu wa Dini watashindwa kuchukua hatua stahiki, sisi waamini tutachukua hatua.
Hapo hakutakuwa na ZAKA, SADAKA wala MICHANGO mingine yoyote ile.
Huwezi kumtaka mwumini atoe ZAKA na SADAKA wakati wewe Kiongozi umeshindwa kuisimamia Serikali kulinda utajiri wa Nchi.
Narudia tena, viongozi wetu wa Dini fuatilieni kwa kina Mambo haya mawili na kisha tuambieni ukweli wake.
1. Inasemekana kuna muswada wa kufuta sheria zinazolinda Rasilimali zetu za Nchi, je, ni kweli?
2. Kuna ukweli kiasi gani kuhusu Mkataba wa DP World?
Nawasilisha.