Serikali kuwafumbia macho wanaopandikiza UDINI ni ishara gani?

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Ndugu zanguni Watanzania, tangu ulipozuka mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na DP World kumetokea maoni mengi kutoka kwa Watanzania wa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini, ambao wengi wao wanaupinga mkataba huu.

Kwa hivi karibuni kumetokea viongozi kadhaa wa Dini nyingine wakiwatuhumu wanaopinga mkataba huu kuwa wanapinga kwa sababu Rais ana Dini tofauti na wanaopinga.

Kwa kumbukumbu zangu sijawahi sikia mtu yeyote anayepinga mkataba huu anasema kwamba eti anapinga kwa sababu hiyo ya Dini. Sijamsikia hata mmoja.

Ushauri wangu:-
1. Serikali isiwafumbie macho wanaopandikiza UDINI bila hata ya kuwa na ushahidi kwamba ni nani na ni wapi mtu alisema anapinga mkataba huu kwa sababu tu ya Dini.

2. Wanaopandikiza UDINI waache mara moja.

NB:- Serikali kuendelea kuwafumbia macho watu wa namna hii inaweza kutafsiriwa kwamba Serikali ndo inayowatuma watu kupandikiza UDINI ili kupunguza kasi ya wanaopinga mkataba huu.

Nakumbuka hata wakati wa JPM, watu na makundi mbalimbali wakiwemoTEC walimpinga JPM lakini hatukushuhudia mtu hata mmoja akilalamika kwamba JPM anapingwa kutokana na Dini yake.

Kwa nini iwe leo?
Serikali isipoziba ufa leo, itajenga ukuta kesho.
 
Ni mjinga pekee ndo atakuwa na mawazo ya kuona kwamba dini ina umuhimu mkubwa kuliko maslahi ya taifa.

"Religion is the opium of the people"Karl Marx
 
Back
Top Bottom