Ni wapi naweza kupata Kiwanja cha chini ya milioni 4 kwa Dar es Salaam?

Huwezi kupata eneo ndani ya Dar es salaam kwa hela hio mzee! Maeneo yapo Mkuranga kwa hio pesa unapata eneo kubwa tu la kutosha. Hio ni Kilwa road!

Upande wa Bagamoyo road pia yapo maeneo Vikawe ni mbele kidogo ya Bunju unapata eneo freshi kubwa tu 20*20 au zaidi!

Morogoro road ni kuanzia mbele ya Kibaha hapo. Kama upo tayari tunaweka wese tunaenda kamata eneo chap!
 
Kuna maeneo ya Kisemvule nayafahamu unapata kiwanja tena kikubwa tu kizuri hakipo bondeni na kimepimwa. Pi pameendelea maji umeme na daladala zipo.

Ila ndani ya Dar es Salaam mmmmmh ni ngumu sana.

Naishi Dar ila kwa maeneo nayoishi mm bila Mil 15 na kuendelea wala usifikirie kuhusu kiwanja

Karibu
 
Back
Top Bottom