Ni wakati sasa Wabunge kuacha utapeli na kulipa kodi inayolingana na kipato chao

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
Wabunge wetu wa TZ wamejadili na kujinasibu niya yao ya kuinua mapato ya Taifa kupitia kodi. Hali inayojionesha kwa miaka mingi, ni tabia yao ya kutozungumzia ulipajhi wao wa kodi, usioendana na kipato halisia walichonacho. Kwa ujumla hili ni Bunge la watu wa misheni touni.

Ktk kuhakikisha wanakwepa kodi, misharaha yao iliwekwa chini kabisa. Wabunge mshahara ukawa ni milioni 2 +. Baada ya hapo wanaongezewa posho ambazo zinafikia milioni 9. Posho hazilipiwi kodi na wao wanajiona wanalipa kodi kwa kututapeli eti mshahara wao ni mililioni 2+.

Miaka ya nyuma jambo hili lilipigiwa kelele na Mh. Zitto akieleza juu ya wataalamu wa kigeni walioko migodini ambao walikuwa wakilipwa posho badala ya mishahara, na mishahara yao ikilipwa kupitia akaunti zao za nje. Pamoja na kuwalalamikia hawa, hakuwahi kueleza tatizo la wao wneyewe wabunge kutumia uhuni huo huo! Huu ni wakati wa kukamatana nguo kabla hatujakimbilia Burundi. Wabunge walipe kodi sahihi za kipato chao na siyo mishahara ya bandia. Huu ni utapeli.
 
Back
Top Bottom