Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Hivi karibuni kumeibuka manung'uniko makubwa ya uonevu kwa wafanyabiashara kuhusu tozo kubwa za kodi.
Mishale na lawama wamekuwa wakitupiwa ndugu zetu wa TRA.
Lakini, ukichunguza kwa umakini utagundua tatizo la msingi haliko kwao.
Tatizo ni ubunifu usiotosheleza wa nchi yetu katika kubainisha vyanzo vya kodi.
Vyanzo vikubwa kama Mifugo, vimeachwa bila sababu.
Kwa hesabu ndogo tuu, mfano Wilaya kama Meatu ina takriban ya ngombe zaidi ya laki nne. Ukitoza kodi angalau 2,000/= kwa kichwa cha ngombe kwa mwaka utapata almost 800 million, bado mbuzi na wanyama wengine.
Hiki chanzo kingeweza kupunguza lengo la makusanyo ya Wilaya yaliyoelekezwa kwa wafanyabiashara tu.
Halikadhalika, Serikali hutumia gharama kubwa kutengeneza miundombinu ya mifugo. Ni kwa nini gharama hizo zisitokane na kodi ya mifugo,badala ya kutumia kodi za wafanyakazi na wafanyabiashara.
Ni maoni yangu kuwa sekta zote za kipato rasmi,zichangie kwa usawa maendeleo ya nchi yetu badala ya kuelekeza nguvu zote kwa kundi dogo.