Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

Na hilo haiwezekani na halipo mkuu kutenganishana TISS na rais au ikulu hata uko marekani mnapotelea mfano halipo hilo?
Director wa CIA na NSA marekani wanawajibika kwa kamati ndogo ndogo za senate zinazoundwa kuviangalia vyombo hivyo...
Na wala sio raisi wa marekani..
Kwahyo inawezekana kbsa vyombo hivi vikatenganishwa na ofisi ya raisi...

Hii wenzetu walifanya kama njia ya kumdhibiti raisi ikitokea anakwenda kinyume na maslahi ya taifa.
 
Nakubaliana na hoja yako mleta uzi ila wasiwasi wangu tu ni kwamba endapo ikivunjwa sisi wa mtaani tutakuwa kila siku tunachezea tu ' vitasa ' namaanisha kupigwa na Wao kwani nina uhakika wengi watapoteza ajira zao hapo hivyo Wananchi wa kawaida tutakuwa tumepewa Kazi ya lazima ya kuvumilia maumivu ya ' kutandikwa ' kwa hasira. Umakini mkubwa sana utahitajika katika kuivunja na kuisuka upya.

Hahahaa, lakini unajua siyo wote wanakuaga fit mkuu silaha zinawapa ule ubabe sana.
Mfano kwa JWTZ wengi mtaani huwa wakikutana na raia walojipika na kuiva wanakimbilia kambini kuita wenzao ndo wanakuja kulipa kisasi kwanini akiwa mjeshi mmoja tukikwaruzana asisimame peke yake hadi aende akasemelehe kwa wenzake!
Kuna raia wako fit sana hadi raha sijui ma black belt nk, kama anakuja asitumie silaha halafu tuone nani anajua kucheza ngoma nyingi.
 
Ivi uivunje TISS wale jamaa wakafanye kazi gani?unajua uwezo wao au unadhani ni km police wa mtaani kwenu pale?wale ni special solders with special skills n training,makomando wamejaa tele kule na siri kibao za inchi wakikosa kazi wakafanye nn..au unataka waipindue inchi,kuna vitu ht ukiwaza kwa juu juu tu unaona ni kitu hakiwezekani....only people with uelewa mdogo wanaweza waza kuivunja taasisi km hio...
Naomba kujua mkuu hivi mfano akichaguliwa rais kutoka upinzani anaeza kuvunja au bado haitowezekana?
 
Wazo Zuri sana. Tatizo la wabunge wetu wengi hawajielewi kabisa.
 
Uko sawa kabisa mkuu nadhani TISS nadhani anahisi ni kitu kidogo wakati ni zaidi ya jeshi maana hao ndo wanajua sirizote za nchi na ndo roho ya nchi kama ulivyotangulia kusema. Na pia usalama wa taifa kwenyw shughuli zao hawaingiliwi na chombo chochote na ndo maana kwanza huwezi kusikia mtu anakwambia yeye ni usalama wa taifa wala hawana sare. Na ubaya au uzuri kwenye kila idara wapo kibao hata usiomdhania kumbe naye yumo. Ogopa sana hii na kama wakiamua kukukamata wanakukamata huna ujanja na wakikukamata wakiamua kukuachia wameamua wao sio kelele za huku mitandaoni.
Hata akija rais kutoka upinzani mna maana hawezi kufanya mabadiliko na kuvunja kama ataona iliopo ina mapungufu?
 
NAJUA TISS NI USALAMA WA TAIFA SAWA..ILA KIREFU CHAKE TAFADHALI NIELEWESHENI
 
Naomba kujua mkuu hivi mfano akichaguliwa rais kutoka upinzani anaeza kuvunja au bado haitowezekana?
ipo kisheria,rais hawezi vunja,
wabunge wakiungana wanabadili sheria wanavunja kwa kuunda sheria mpya
 
Mkuu kuna sheria nyingine inawezekana zimetungwa vibaya au hazifai tena, mfano kwa sasa rais anateua mkurugenzi na moja kwa moja anakuwa valid sasa kama rais mpya anapoingia akiteua huyo na wakaamua kufanya overhaul kwa kurecruit upya wote kutokana na maslahi yao hii itakuwa ni sawa na kuvunja na hakika inawezekana.
Ajira hizo hazitangazwi hivyo wala hamtajua.
 
tissivunjwe.png
Kuna namna nyingi za kushughulikia yanayoendelea nchini sasa hivi na hasa madai makali dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mengi tumeshazungumza juu ya Idara hii na kwa muda mrefu. Bahati mbaya inaonekana hata wabunge wetu hawajaona njia rahisi na ya haraka ya kusafisha idara hii. Tayari inaonekana wapo wabunge wengi kutoka pande zote mbili ambao wanakubaliana kuwa kuna tatizo fulani katika Idara. Sasa kwanini wabunge wasitumie umoja wao huu wa misimamo kufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao?

Wabunge ndio watunga sheria wa nchi hi (law makers). Rais hatungi sheria hata moja; yeye kwake ni kuzipitisha tu. Siyo tu wabunge wanatunga lakini pia wanaweza kufanya marekebisho sheria na Katiba!

Sasa kuna pendekezo la Zitto kuchunguza matukio mbalimbali ambayo yanadaiwa kutokea hivi karibuni na Idara kuhusishwa. Njia hii ya Kamati Teule inaweza kutangulia – kama alivyodokeza – mabadiliko yoyote ya idara. Kamati Teule inaweza kuwaita watendaji na wakuu wote wa idara za usalama na kuwahoji chini ya kiapo – mbele ya camera au nje ya camera – na kutaka kujua nini kinaendelea. Na kwa vile Kamati ina nguvu za kibunge na mahakama inaweza kumlazimisha yeyote kati yao kufika mbele ya kamati hiyo au kuagizwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya kamati hiyo.

Hiyo inaweza kuwa ni njia sahihi ya kutaka kutafuta ukweli. Pamoja na kuwaita hawa wote inaweza kuwaita hata waathirika wa vitendo hivi. Bashe kwa mfano anaweza kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kutoa ushahidi wa madai ya kuwa kuna “mawaziri” ambao wamempa taarifa kuwa yeye ni mlengwa wa kutekwa; Zitto mwenyewe vile vile n.k Lengo ni kutaka kujua ukweli zaidi ili watakapotaka kufanya mabadiliko wajue wapi pa kuanzia.

kipilimba-e1491927638963.jpg

Mkurugenzi wa TISS Dkt. Modestus Kipilimba
Hata hivyo, hilo linahitaji kuungwa mkono sana na wabunge wa CCM. Njia ya pili ambayo binafsi naipenda zaidi kama njia ya haraka ni kwa wabunge wenye kuona tatizo hasa – Bashe, Ridhiwani, Zitto, na wengine wakutane pamoja na kuandaa mswaada wa pamoja (bipartisan bill) ya kuivunja Idara ya Usalama wa Taifa na kuiunda upya ikiwa imetengenezwa kukidhi mahitaji ya kiusalama ya taifa hili na ikisimamiwa moja kwa moja na Bunge. Mswada huu uletetwe hata kwa hati ya dharura ili kabla ya Bunge hili kuisha usomwe unavyohitajika na upitishwe na Bunge na hatimaye upelekwe kwa rais kwa kuudhinisha.

Nina uhakika Rais Magufuli ataridhia kwani atakuwa amesaidiwa kazi ambayo labda ingemchukua muda yeye mwenyew ekuifanya. Na kama hatoridhia na kutishia Veto Bunge linaweza kuipiku veto hiyo kwa kura nyingi na kumlazimisha aisaini na kama haitowezekana basi Bunge litavunjwa na watu watarudishwa kwenye uchaguzi mkuu mpya ambapo wananchi watapata nafasi ya kwenda kuchagua wabunge na Rais mwingine kulingana na ajenda watakazosimama nazo.

Lakini kulalamika tu wakati nyenzo wanazo ni kupoteza muda wa watu. Ni wakati wa kufanya wanachoamini ni sahihi kufanya na wana uwezo wa kukifanya. Lakini pia utakuwa ni wakati wa watu kuhesabiwa. Kwa sisi wengine ambao tumekuwa tukilalamikia idara hii kwa muda mrefu tunaona labda hii ni nafasi ya pekee ya kuileta Idara hii kwenye karne ya 21. Inapofikia watu tena wazito wanadai kuwa Idara inajihusisha au watumishi wake wanajihusisha na vitendo ovya kighaidi hakuna namna namna nyingine ya kufanya isipokuwa kuivunja idara hiyo na kuiunda upya toka chini. Mkitaka mawazo tupo wengine tunaweza kuwasaidia.
Hivi jamani TISS mfano wake inavyofanya kazi si na kama kwenye zile hadithi za Willy Gamba au?

Katiaka vitabu vya NJAMA, KIKOSI CHA KISASI, KIKOMO, KUFA NA KUPONA NA HUJUMA au sio jamani?

Sasa hii TISS ya kuvamia Studio za Luninga au Studio za kurekodia miziki ya Bongo fleva ... daaa!! Jamani!! Hata kamaaa hii ni aibu ...

Mara watu wametekwa ... mara sjui wamemtolea mguu wa kuku Mh. hadharani yani winjiwinji ... mara Oooh

Yaani mkuranga watu wanauana huko wao wamekalia kutumwa kuteka watu, mara wanatumwa kuvamia studio za watu .... acheni mambo ya aibu nendeni mkatafute wahalifu huko kama mnaweza mnajishaua tu hapa kuwaonea kina Roma ... kuna wanaume huko walitoa orodha yao na wameikamilisha hamna hata mmoja alie kamatwa ... leo mnaenda kumkomalia Roma hajui hata kushika bunduki bc mnajiona viduuume ...
 
Pia kwa kuongeza tu kuwepo na baraza la usalama la Taifa ambalo litasimamia idara hii au kushauri

Hilo baraza lipo sasa hivi na nakumbuka wakati linaanzishwa tulikuwa na mjadala mkubwa tu wa hilo na hasa mahusiano yake na vyombo vingine vya serikali.
 
Hizo ndugu yangu ni ndoto za abunuasi za kutaka kuivunja idara nyeti kama hiyo. Kwanza kumbuka kila idara ile ina kanuni zake za kuiendesha. Pili bunge halina uwezo huo. Yaani idara ya usalama wa taifa haiendeshwi kisiasa kama chama. Na kumbukeni kuwa kunamafunzo maalumu ya usalama wa taifa. Hilo msahau mkiongea sana mtaishia kufa kqa bp za vitisho. Na kutekwa.
Mkuu idara hii sasa imegeuka kuwa kikundi cha kigaidi...ni bora ivunjwe tu, hakuna namna nyingine.
 
....then inaundwa upya. Mkuu naona umesoma heading tu hujasoma 'yaliyomo'.

Yaani watu wakati mwingine wanaonesha ni kwanini Magufuli anahitajika!! Mtu anakuja na kuuliza "toa mifano" wakati kwenye mada kuna mifano karibu mitano! Sasa unajiuliza kweli hawa watu wanataka kujua kweli au ni wagumu kujua..
 
iyo taasisi ikivunjwa wanapelekwa wapi sasa? izo skills na knowledge c threats nyingine wakikaa bila kazi au embu nielewesheni
 
Kuna watu humu ni wa hovyo kabisa hata hawaelewi kitu wapo wapo tu, Ichukueni katiba ya nchi someni mjue nini maana ya TISS.Kama hujui kitu ni bora kunyamaza kuliko kuandika kiuoga uoga kutisha wale wasioelewa kitu.

Kwa sababu hawaonekani ndio kunawafanya watu kupandwa na BP humu kawafanya ndio miungu wa nchi, kwa bahati mbaya sana nimefuatilia mijadala mingi humu ni kwamba ni wachache sana humu wenye uelewa na TISS, Wengi wanaadika kwa hisia tu kwa sababu wanasimuliwa.

Kwa wenye upeo na mambo haya ngoja tuwatoe matongotongo muache kupotosha watu humu bure.

Idara ya usalama wa taifa kwanza iko chini ya ofisi ya rais, na ofisi ya Rais ndio yenye mamlaka kuamua nini kifanyike ndani ya idara hiyo.Hata mswaada wa sheria ya kufanya maboresho ndani ya idara hiyo ni lazima uandaliwe ofisi ya nchi ofisi ya Rais.

Kuna tofauti kati ya usalama wa taifa na walinzi wa Rais, usalama wa taifa kazi yao sio kumlinda Rais na ikulu yake bali kuna kikosi maalum ambacho ni special force ambacho kina mafunzo ya aina yake tofauti hata na wanajeshi wakawaida ambao kazi yao ni kulinda viongozi wa kitaifa, na ni wanajeshi hawa. Hawa walinzi sio usalama wa taifa, usalama wa taifa ni intelligence individuals ambao kupitia mafunzo ya kijeshi na kisha baadae kupelekwa mafunzo maalum ya namna ya kuendesha kazi zao na sio mafunzo ya ukomandoo kama waswahili wetu wanavyodai humu.Ila tufahamu kua hata kwenye majeshi yote usalama wa taifa wapo kuanzia JWTZ mpaka uhamiaji, wanafanya kazi za jeshi kama wanajeshi wengine lakini wanazo kazi zao za ziada ambazo ni lazima upitie chuo chao cha usalama wa taifa.

Hata wewe hapo ulipo serikali inaweza kukuona unafaa kutunza siri za nchi ukifundishwa vyema ukapelekwa jeshini na baadae chuo cha usalama wa taifa ukawa mwanausalama mzuri tu, ndio maana hata alipopotea ndugu Ben Saanane wakahisi kua usalama wa taifa wamemchukua kwenda kupewa mafunzo maalum na baadae alitumikie taifa japo wanausalama hawapatikani kwa mtindo huo.

Usalama wa taifa wanafanya kazi nyeti za siri na sio na wala hawatakiwi kukamata watu, TISS hawatakiwi kutembea na bunduki mtaani wanapoenda kufuatilia jambo flani ambalo linatia hofu juu ya usalama wa nchi, wao kazi yao ni kutumia akili ya ziada kupata ukweli wa jambo na kutoa taarifa kwa vyombo vya ukamataji kama polisi. Hawa ndio wanaotangulia mahali flani kama kuna msafara wa kiongozi flani wa kitafa kunusa kama kuna utulivu katika eneo au laah.

Njia za kuwapata hawa jamaa ziko wazi, mara nyingi huangaliwa vijana wenye tabia nzuri na nidhamu ya hali ya juu ili iwe rahisi kufundishika juu ya uzalendo wa kulitumikia taifa lao,kazi hii Mara nyingi huanzia mashuleni,hasa wale vijana wachamungu kwa na wenye imani dhabiti. Hata kwenye mafunzo ya JKT pia huangaliwa vijana wenye uwezo mzuri wa kiakili na nidhamu pindi wamalizapo mafunzo ya kijeshi hupelekwa kwenye mafunzo maalum kwa ajili ya kuitumikia idara hiyo ambapo baadae ni lazima zifuatiliwe taarifa muhimu za maisha ya mhusika kutoka familia tofauti na alivyokua JKT.

Hawa wanaoteka watu sio usalama wa taifa, ni kikundi tu cha trained personnel kwa ajili ya kazi hiyo na ni wenye mafunzo ya military force,hiyo sio kazi ya usalama wa taifa, kama ni usalama wa taifa kama wanavyohisi wengine basi nami namuunga mkono Mzee mwanakijiji.

Wasalaaam alaykum!!!
 
tissivunjwe.png
Kuna namna nyingi za kushughulikia yanayoendelea nchini sasa hivi na hasa madai makali dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mengi tumeshazungumza juu ya Idara hii na kwa muda mrefu. Bahati mbaya inaonekana hata wabunge wetu hawajaona njia rahisi na ya haraka ya kusafisha idara hii. Tayari inaonekana wapo wabunge wengi kutoka pande zote mbili ambao wanakubaliana kuwa kuna tatizo fulani katika Idara. Sasa kwanini wabunge wasitumie umoja wao huu wa misimamo kufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao?

Wabunge ndio watunga sheria wa nchi hi (law makers). Rais hatungi sheria hata moja; yeye kwake ni kuzipitisha tu. Siyo tu wabunge wanatunga lakini pia wanaweza kufanya marekebisho sheria na Katiba!

Sasa kuna pendekezo la Zitto kuchunguza matukio mbalimbali ambayo yanadaiwa kutokea hivi karibuni na Idara kuhusishwa. Njia hii ya Kamati Teule inaweza kutangulia – kama alivyodokeza – mabadiliko yoyote ya idara. Kamati Teule inaweza kuwaita watendaji na wakuu wote wa idara za usalama na kuwahoji chini ya kiapo – mbele ya camera au nje ya camera – na kutaka kujua nini kinaendelea. Na kwa vile Kamati ina nguvu za kibunge na mahakama inaweza kumlazimisha yeyote kati yao kufika mbele ya kamati hiyo au kuagizwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya kamati hiyo.

Hiyo inaweza kuwa ni njia sahihi ya kutaka kutafuta ukweli. Pamoja na kuwaita hawa wote inaweza kuwaita hata waathirika wa vitendo hivi. Bashe kwa mfano anaweza kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kutoa ushahidi wa madai ya kuwa kuna “mawaziri” ambao wamempa taarifa kuwa yeye ni mlengwa wa kutekwa; Zitto mwenyewe vile vile n.k Lengo ni kutaka kujua ukweli zaidi ili watakapotaka kufanya mabadiliko wajue wapi pa kuanzia.

kipilimba-e1491927638963.jpg

Mkurugenzi wa TISS Dkt. Modestus Kipilimba
Hata hivyo, hilo linahitaji kuungwa mkono sana na wabunge wa CCM. Njia ya pili ambayo binafsi naipenda zaidi kama njia ya haraka ni kwa wabunge wenye kuona tatizo hasa – Bashe, Ridhiwani, Zitto, na wengine wakutane pamoja na kuandaa mswaada wa pamoja (bipartisan bill) ya kuivunja Idara ya Usalama wa Taifa na kuiunda upya ikiwa imetengenezwa kukidhi mahitaji ya kiusalama ya taifa hili na ikisimamiwa moja kwa moja na Bunge. Mswada huu uletetwe hata kwa hati ya dharura ili kabla ya Bunge hili kuisha usomwe unavyohitajika na upitishwe na Bunge na hatimaye upelekwe kwa rais kwa kuudhinisha.

Nina uhakika Rais Magufuli ataridhia kwani atakuwa amesaidiwa kazi ambayo labda ingemchukua muda yeye mwenyew ekuifanya. Na kama hatoridhia na kutishia Veto Bunge linaweza kuipiku veto hiyo kwa kura nyingi na kumlazimisha aisaini na kama haitowezekana basi Bunge litavunjwa na watu watarudishwa kwenye uchaguzi mkuu mpya ambapo wananchi watapata nafasi ya kwenda kuchagua wabunge na Rais mwingine kulingana na ajenda watakazosimama nazo.

Lakini kulalamika tu wakati nyenzo wanazo ni kupoteza muda wa watu. Ni wakati wa kufanya wanachoamini ni sahihi kufanya na wana uwezo wa kukifanya. Lakini pia utakuwa ni wakati wa watu kuhesabiwa. Kwa sisi wengine ambao tumekuwa tukilalamikia idara hii kwa muda mrefu tunaona labda hii ni nafasi ya pekee ya kuileta Idara hii kwenye karne ya 21. Inapofikia watu tena wazito wanadai kuwa Idara inajihusisha au watumishi wake wanajihusisha na vitendo ovya kighaidi hakuna namna namna nyingine ya kufanya isipokuwa kuivunja idara hiyo na kuiunda upya toka chini. Mkitaka mawazo tupo wengine tunaweza kuwasaidia.
Katika siku ulizo wahi kuleta pumba ni leo
 
Unajua tofauti ya CIA,NSA,FBI n likes na police wa kawaida huko USA au ushabiki tu?TISS yetu ni sawa kua na muunganiko wa FBI na CIA maana kule wametenganisha wao operate local (fBi) and overseas (CIA) kitu ambacho ss hatujatenganisha...atleast FBI wanaweza mtia mbaroni CIA kutokana na level ya mafunzo kua zinafanana ila sio police wa kawaida...the same na hapa Tanzania,mafunzo yao na ht treatment zao no tofauti e.g mshahara,makazi nk kifupi they are special,wanachukuliwa vijana wenye vipaji jeshini na sehem nyingine ndo wanaenda TISS...police anaanzaje kumkamata TISS,labda jamaa aamue tu kua mpole ajisalimishe ila sio by force...

Unapokuta mada kama hizi, ni vyema ukajadiri huku akili za usiku umeacha kitandani.

Kajifunze majukumu ya hivyo vyombo vyote vya nje ulivyovitaja, kisha utaelewa siku nyingine nini uandike.vinginevyo utapuyanga tena.
Ni nyie wabongo ndio wenye hulka ya kuchanya taaluma na siasa, matokeo yake ndio haya yalipofikia.eti kwamba CIA agent atafanya kosa barabarani, kisha aanze kubishana na askari kwa mateke, huu ujinga hata tiss wa bongo hawezi fanya mzee, vinginevyo kazi itaishia hapo kwa taarifa yako.

Hizi story za kahawa sio mahala pake humu.
 
Kwani serikali inaendeshwa kwa uwepo wa TISS pekee? Unajua jinsi Idara hiyo inavyotumiwa na baadhi ya watu kuviza demokrasia na kuingilia kati CCM inapozidiwa na wapinzani wao?
Mkuu Allen Kilewella,suluhisho la hilo uliloandika na mengine yanayosadikiwa kufanywa na TISS si kuivunja,bali ni kufanya marekebisho kwa kuangalia misingi ya kuundwa kwake,mfumo wake,sheria ya kuanzishwa kwake na madhumuni makuu ya uanzishwaji. Tatizo sio hii taasisi,tatizo ni mamlaka inayoisimamia hiyo taasisi. Amini kuwa hata kama ikivunjwa,kama hatutaweka misingi na madhumuni ya kueleweka pamoja na kukazia kwa sheria,kanuni na taratibu za uendeshaji,hali inayojitokeza leo itaendelea tena kujitokeza.
Tatizo lipo kwa mamlaka ambayo hii taasisi inaripoti kwake.
Tatizo lipo kwenye misingi na madhumuni ya uanzishaji wake. Je,sababu na madhumuni ya uanzishwaji wake bado ni yaleyale? Je,kama ni yaleyale,hatupo nyuma ya wakati? Kama ni mapya,yamewekwa na nani kwa sheria ipi? Maana inawezekana kila mamlaka ya juu yake mpya inapokuja inaamua taasisi ifanye hivi badala ya kusimamia misingi,na hii yote ni kutokana na kutokuwa na "independence" kwa wateuliwa wa taasisi tofauti kama ilivyo kwa CAG au CJ.
 
Kuna watu humu ni wa hovyo kabisa hata hawaelewi kitu wapo wapo tu, Ichukueni katiba ya nchi someni mjue nini maana ya TISS.Kama hujui kitu ni bora kunyamaza kuliko kuandika kiuoga uoga kutisha wale wasioelewa kitu.

Kwa sababu hawaonekani ndio kunawafanya watu kupandwa na BP humu kawafanya ndio miungu wa nchi, kwa bahati mbaya sana nimefuatilia mijadala mingi humu ni kwamba ni wachache sana humu wenye uelewa na TISS, Wengi wanaadika kwa hisia tu kwa sababu wanasimuliwa.

Kwa wenye upeo na mambo haya ngoja tuwatoe matongotongo muache kupotosha watu humu bure.

Idara ya usalama wa taifa kwanza iko chini ya ofisi ya rais, na ofisi ya Rais ndio yenye mamlaka kuamua nini kifanyike ndani ya idara hiyo.Hata mswaada wa sheria ya kufanya maboresho ndani ya idara hiyo ni lazima uandaliwe ofisi ya nchi ofisi ya Rais.

Kuna tofauti kati ya usalama wa taifa na walinzi wa Rais, usalama wa taifa kazi yao sio kumlinda Rais na ikulu yake bali kuna kikosi maalum ambacho ni special force ambacho kina mafunzo ya aina yake tofauti hata na wanajeshi wakawaida ambao kazi yao ni kulinda viongozi wa kitaifa, na ni wanajeshi hawa. Hawa walinzi sio usalama wa taifa, usalama wa taifa ni intelligence individuals ambao kupitia mafunzo ya kijeshi na kisha baadae kupelekwa mafunzo maalum ya namna ya kuendesha kazi zao na sio mafunzo ya ukomandoo kama waswahili wetu wanavyodai humu.Ila tufahamu kua hata kwenye majeshi yote usalama wa taifa wapo kuanzia JWTZ mpaka uhamiaji, wanafanya kazi za jeshi kama wanajeshi wengine lakini wanazo kazi zao za ziada ambazo ni lazima upitie chuo chao cha usalama wa taifa.

Hata wewe hapo ulipo serikali inaweza kukuona unafaa kutunza siri za nchi ukifundishwa vyema ukapelekwa jeshini na baadae chuo cha usalama wa taifa ukawa mwanausalama mzuri tu, ndio maana hata alipopotea ndugu Ben Saanane wakahisi kua usalama wa taifa wamemchukua kwenda kupewa mafunzo maalum na baadae alitumikie taifa japo wanausalama hawapatikani kwa mtindo huo.

Usalama wa taifa wanafanya kazi nyeti za siri na sio na wala hawatakiwi kukamata watu, TISS hawatakiwi kutembea na bunduki mtaani wanapoenda kufuatilia jambo flani ambalo linatia hofu juu ya usalama wa nchi, wao kazi yao ni kutumia akili ya ziada kupata ukweli wa jambo na kutoa taarifa kwa vyombo vya ukamataji kama polisi. Hawa ndio wanaotangulia mahali flani kama kuna msafara wa kiongozi flani wa kitafa kunusa kama kuna utulivu katika eneo au laah.

Njia za kuwapata hawa jamaa ziko wazi, mara nyingi huangaliwa vijana wenye tabia nzuri na nidhamu ya hali ya juu ili iwe rahisi kufundishika juu ya uzalendo wa kulitumikia taifa lao,kazi hii Mara nyingi huanzia mashuleni,hasa wale vijana wachamungu kwa na wenye imani dhabiti. Hata kwenye mafunzo ya JKT pia huangaliwa vijana wenye uwezo mzuri wa kiakili na nidhamu pindi wamalizapo mafunzo ya kijeshi hupelekwa kwenye mafunzo maalum kwa ajili ya kuitumikia idara hiyo ambapo baadae ni lazima zifuatiliwe taarifa muhimu za maisha ya mhusika kutoka familia tofauti na alivyokua JKT.

Hawa wanaoteka watu sio usalama wa taifa, ni kikundi tu cha trained personnel kwa ajili ya kazi hiyo na ni wenye mafunzo ya military force,hiyo sio kazi ya usalama wa taifa, kama ni usalama wa taifa kama wanavyohisi wengine basi nami namuunga mkono Mzee mwanakijiji.

Wasalaaam alaykum!!!
Mkuu nashukuru kwakuwa umeliona hili mapema mno.

Ni wachache wanajua haya mambo akiwamo mtoa mada, lakini kwa michango ya wachache humu, nabaki kukumbuka hadithi za kufikirika kwenye magazeti, huwenda walizibeba kama zilivyo wengi wao humu.
 
Back
Top Bottom