Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

warudi tu wakalime,maana sasa tushachoka , kwanza nashangaa polisi kuwafumbia macho,
nchi kama marekani hata secret service ukishafanya tukio hata ukaingia mikononi mwa FBI hata rais hawezi kukuchomoa utakwenda lokapu tu
Unajua tofauti ya CIA,NSA,FBI n likes na police wa kawaida huko USA au ushabiki tu?TISS yetu ni sawa kua na muunganiko wa FBI na CIA maana kule wametenganisha wao operate local (fBi) and overseas (CIA) kitu ambacho ss hatujatenganisha...atleast FBI wanaweza mtia mbaroni CIA kutokana na level ya mafunzo kua zinafanana ila sio police wa kawaida...the same na hapa Tanzania,mafunzo yao na ht treatment zao no tofauti e.g mshahara,makazi nk kifupi they are special,wanachukuliwa vijana wenye vipaji jeshini na sehem nyingine ndo wanaenda TISS...police anaanzaje kumkamata TISS,labda jamaa aamue tu kua mpole ajisalimishe ila sio by force...
 
Kama kumwondoa tu bashite mmeshindwa ndio mtavunja tiss??
 
Mkuu TISS sio kama bodi ya korosho kule lindi useme unaweza kuivunja tu anytime...utatengeneza tatizo zaidi ya hili....solution Bunge limuwajibishe sizonje na vibaraka wake tu

Sijui umesoma nilichosema au unadhani nimesema tu bila kufikiria. Haitokuwa taasisi ya kwanza ya usalama duniani kuvunjwa na taifa lake na kutoka hapo kuundwa kwa taasisi nyingine. Hakuna tatizo jingine lolote litakalotokea isipokuwa itakuwa ni woga.
 
Unajua tofauti ya CIA,NSA,FBI n likes na police wa kawaida huko USA au ushabiki tu?TISS yetu ni sawa kua na muunganiko wa FBI na CIA maana kule wametenganisha wao operate local (fBi) and overseas (CIA) kitu ambacho ss hatujatenganisha...atleast FBI wanaweza mtia mbaroni CIA kutokana na level ya mafunzo kua zinafanana ila sio police wa kawaida...the same na hapa Tanzania,mafunzo yao na ht treatment zao no tofauti e.g mshahara,makazi nk kifupi they are special,wanachukuliwa vijana wenye vipaji jeshini na sehem nyingine ndo wanaenda TISS...police anaanzaje kumkamata TISS,labda jamaa aamue tu kua mpole ajisalimishe ila sio by force...
.....
......Nidhamu ikojuu zaidi ya efubiai
 
kwa kukeep law and order usiwadharau polisi hata siku moja ,hata uwe shushushu wa gredi ipi,polisi akipewa order utakamatwa tu
wanawakamata wenye uwezo nao...sio waliowazidi mbinu na ufundi wa kiintelegensia na kimapigano...unamkamataje mtu anawaza dk 3 mbele yako?unaejua mbinu za kimapigano zaidi yako?unamkamataje mtu wa hivyo,labda umuombe ajisalimishe...
 
Naomba kuelewesha tafadhali. Idara hii ikivunjwa watumishi wake inakuaje? wanapelekwa kwenye idara nyingine? au wanakuwa kwenye idara mpya itakayotengenezwa kwa maana kuwa mfumo pekee ndo unabadilika?

Swali zuri; katika kuvunja idara hii kati ya vitu vya kwanza vitakavyofanywa ni kuhakiki "watumishi" wake. Kumbuka kwa mujibu wa sheria ya hivi sasa ni Mkurugenzi ndiye anayeajiri watumishi na kishera peke yake anayejua hata majina yao! Hili litabadilika. Nitaeleza siku si nyingi zijazo maoni ya mtazamo wangu juu ya nini kifuatie baada ya kuvunjwa kwa TISS na nini kitatokea kwa baadhi ya watumishi wake. Ikivunjwa TISS haitakuja taasisi moja nyingine; binafsi naamini zinatakiwa zije taasisi nyingine tatu hivi zenye mipaka na sheria zake.
 
Uko sawa kabisa mkuu nadhani TISS nadhani anahisi ni kitu kidogo wakati ni zaidi ya jeshi maana hao ndo wanajua sirizote za nchi na ndo roho ya nchi kama ulivyotangulia kusema. Na pia usalama wa taifa kwenyw shughuli zao hawaingiliwi na chombo chochote na ndo maana kwanza huwezi kusikia mtu anakwambia yeye ni usalama wa taifa wala hawana sare. Na ubaya au uzuri kwenye kila idara wapo kibao hata usiomdhania kumbe naye yumo. Ogopa sana hii na kama wakiamua kukukamata wanakukamata huna ujanja na wakikukamata wakiamua kukuachia wameamua wao sio kelele za huku mitandaoni.
Mkuu wengi wetu humu jf tunajifanya wajuaji wa kila jambo na tunapoelekea tutasema JWTZ livunjwe kwasababu za umbumbu na kuweka kila kisiasa.
Jamaa awalali ili kuweka nchi salama.
 
Mkuu TISS sio kama bodi ya korosho kule lindi useme unaweza kuivunja tu anytime...utatengeneza tatizo zaidi ya hili....solution Bunge limuwajibishe sizonje na vibaraka wake tu

Ukivunja tiss then?

Mpe nafasi Dr. Kipilimba ashughulikie. Hajamaliza hata miaka miwili ujue pale! Vinginevyo, utatufanya tukufikirie na wewe mara tatu nne nne...!

Mmh mnafikiria kilahisi lahisi sana, Muda uliopo ni muda wa kufanya kazi. haijarishi umerudi hatua ngapi nyuma, na sio muda wa kuchagua kazi wala kuangalia mambo usiyo na uwezo nayo.

Mwisho tutaambiwa tulivunje jeshi.Rais ana vyombo vyake vya kumsaidia kutawala.Hawezi kuvunja TISS kisa tu wabunge wameona hivyo wakati RAIS hajaona tatizo lolote.
Matukio ya watu kuteswa na kuuwawa yametokea sana awamu ya nne na tatu.
Kujiteka kwa Roma hakuwezi kufanya TISS ivunjwe.
Wakati wa awamu ya nne kulikuwa na matukio yakutekwa na kujeruhiwa Ulimboka,kubenea alimwagiwa tindi kali n,k ambayo hatukumsikia Ridhiwani wala Bashe wanapiga kelele hatua zichukuliwe.

Mimi nashauri tusome between the lines na sio within!! Kwa kifupi unahitaji uwe na ubongo wenye afya kwa ajili ya kufikiri na kumwelewa Mwanakijiji, baadhi yetu tunachangia hoja hii tukiwa na uelewa mdogo sana kuhusu hoja yenyewe na suala zima!! Tusisome heading tukimbilie kuchangia! Kifupi tusiwe wavivu wa kusoma na kufikiri, kama baadhi yetu hatuelewi ni bora kubakia kimya, sio dhambi kusoma hoja za wenzio, zitakupanua na yumkini kesho ukatoa mchango maridhawa!!!!
 
Sijui umesoma nilichosema au unadhani nimesema tu bila kufikiria. Haitokuwa taasisi ya kwanza ya usalama duniani kuvunjwa na taifa lake na kutoka hapo kuundwa kwa taasisi nyingine. Hakuna tatizo jingine lolote litakalotokea isipokuwa itakuwa ni woga.
Toa mfano wa taasisi km hio iloyowahi kuvunjwa,mwaka na sababu...haya mambo yanaenda na mifano sio bla bla
 
Toa mfano wa taasisi km hio iloyowahi kuvunjwa,mwaka na sababu...haya mambo yanaenda na mifano sio bla bla

Ndio maana mtu hapo kasema usome; sasa kama hujasoma nilichoandika chote unajuaje sijatoa mifano?
 
Sijui umesoma nilichosema au unadhani nimesema tu bila kufikiria. Haitokuwa taasisi ya kwanza ya usalama duniani kuvunjwa na taifa lake na kutoka hapo kuundwa kwa taasisi nyingine. Hakuna tatizo jingine lolote litakalotokea isipokuwa itakuwa ni woga.
.....
....MMM unawapiga Ngumi sisiemu
 
Mleta thread unadhani kuwa TISS ni kama chama cha waendesha Bodaboda!?

Hata , rais pale akiweka ugoko kuwazuia , TISS wanaweka , Nondo!!

Nchi yeyote ile inayojielewa national security , ni sawa na nchi ndani ya nchi!

Unadhani, kama ingekuwa rahisi hivyo kuvunjwa hao wabunge wangekuwa wanalialia kiasi hicho!??

Kawaze uje na mada yenye akili hii uko " the wrong side of the town!!"
 
Mimi nashauri tusome between the lines na sio within!! Kwa kifupi unahitaji uwe na ubongo wenye afya kwa ajili ya kufikiri na kumwelewa Mwanakijiji, baadhi yetu tunachangia hoja hii tukiwa na uelewa mdogo sana kuhusu hoja yenyewe na suala zima!! Tusisome heading tukimbilie kuchangia! Kifupi tusiwe wavivu wa kusoma na kufikiri, kama baadhi yetu atuelewi ni bora kubakia kimya, sio dhambi kusoma hoja za wenzio, zitakupanua na yumkini kesho ukatoa mchango maridhawa!!!!
unataka tufikiri na kuwaza kama unavyowaza wewe
 
Ndio maana mtu hapo kasema usome; sasa kama hujasoma nilichoandika chote unajuaje sijatoa mifano?
Sijaona mfano ktk post yako...na sio mbaya ukirudia km ulitoa maana nimesoma sijaona kitu,afterall u wont loose anything km ukirudi hio mifano
 
tissivunjwe.png
Kuna namna nyingi za kushughulikia yanayoendelea nchini sasa hivi na hasa madai makali dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mengi tumeshazungumza juu ya Idara hii na kwa muda mrefu. Bahati mbaya inaonekana hata wabunge wetu hawajaona njia rahisi na ya haraka ya kusafisha idara hii. Tayari inaonekana wapo wabunge wengi kutoka pande zote mbili ambao wanakubaliana kuwa kuna tatizo fulani katika Idara. Sasa kwanini wabunge wasitumie umoja wao huu wa misimamo kufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao?

Wabunge ndio watunga sheria wa nchi hi (law makers). Rais hatungi sheria hata moja; yeye kwake ni kuzipitisha tu. Siyo tu wabunge wanatunga lakini pia wanaweza kufanya marekebisho sheria na Katiba!

Sasa kuna pendekezo la Zitto kuchunguza matukio mbalimbali ambayo yanadaiwa kutokea hivi karibuni na Idara kuhusishwa. Njia hii ya Kamati Teule inaweza kutangulia – kama alivyodokeza – mabadiliko yoyote ya idara. Kamati Teule inaweza kuwaita watendaji na wakuu wote wa idara za usalama na kuwahoji chini ya kiapo – mbele ya camera au nje ya camera – na kutaka kujua nini kinaendelea. Na kwa vile Kamati ina nguvu za kibunge na mahakama inaweza kumlazimisha yeyote kati yao kufika mbele ya kamati hiyo au kuagizwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya kamati hiyo.

Hiyo inaweza kuwa ni njia sahihi ya kutaka kutafuta ukweli. Pamoja na kuwaita hawa wote inaweza kuwaita hata waathirika wa vitendo hivi. Bashe kwa mfano anaweza kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kutoa ushahidi wa madai ya kuwa kuna “mawaziri” ambao wamempa taarifa kuwa yeye ni mlengwa wa kutekwa; Zitto mwenyewe vile vile n.k Lengo ni kutaka kujua ukweli zaidi ili watakapotaka kufanya mabadiliko wajue wapi pa kuanzia.

kipilimba-e1491927638963.jpg

Mkurugenzi wa TISS Dkt. Modestus Kipilimba
Hata hivyo, hilo linahitaji kuungwa mkono sana na wabunge wa CCM. Njia ya pili ambayo binafsi naipenda zaidi kama njia ya haraka ni kwa wabunge wenye kuona tatizo hasa – Bashe, Ridhiwani, Zitto, na wengine wakutane pamoja na kuandaa mswaada wa pamoja (bipartisan bill) ya kuivunja Idara ya Usalama wa Taifa na kuiunda upya ikiwa imetengenezwa kukidhi mahitaji ya kiusalama ya taifa hili na ikisimamiwa moja kwa moja na Bunge. Mswada huu uletetwe hata kwa hati ya dharura ili kabla ya Bunge hili kuisha usomwe unavyohitajika na upitishwe na Bunge na hatimaye upelekwe kwa rais kwa kuudhinisha.

Nina uhakika Rais Magufuli ataridhia kwani atakuwa amesaidiwa kazi ambayo labda ingemchukua muda yeye mwenyew ekuifanya. Na kama hatoridhia na kutishia Veto Bunge linaweza kuipiku veto hiyo kwa kura nyingi na kumlazimisha aisaini na kama haitowezekana basi Bunge litavunjwa na watu watarudishwa kwenye uchaguzi mkuu mpya ambapo wananchi watapata nafasi ya kwenda kuchagua wabunge na Rais mwingine kulingana na ajenda watakazosimama nazo.

Lakini kulalamika tu wakati nyenzo wanazo ni kupoteza muda wa watu. Ni wakati wa kufanya wanachoamini ni sahihi kufanya na wana uwezo wa kukifanya. Lakini pia utakuwa ni wakati wa watu kuhesabiwa. Kwa sisi wengine ambao tumekuwa tukilalamikia idara hii kwa muda mrefu tunaona labda hii ni nafasi ya pekee ya kuileta Idara hii kwenye karne ya 21. Inapofikia watu tena wazito wanadai kuwa Idara inajihusisha au watumishi wake wanajihusisha na vitendo ovya kighaidi hakuna namna namna nyingine ya kufanya isipokuwa kuivunja idara hiyo na kuiunda upya toka chini. Mkitaka mawazo tupo wengine tunaweza kuwasaidia.

KWA KUSOMA KWA KIREFU BONYEZA ZAMAMPYA.COM

Ndugu yangu mambo mengine waachie walionaujuzi nayo!! Wapi duniani shirika la kijasusi lilivunjwa?? Ungesema kuliboresha hapo kidogo ningekupa marks mbili...!!
 
Hapana haitowajibika kwa Bunge kwa maana hiyo; bado itatakiwa iwe huru zaidi hadi kuchunguza wabunge! Ila inatakiwa itengenezewe mifumo ya kusimamiwa ili isije kuwa kama mbwa asiye na mnyororo.

Chief hoja yako ni nzito kuliko uwezo wa wengi tuliochangia! Wengi tumechangia kwa kusoma heading tu, itakupa shida kuwapa uelewa(baadhi yetu), kwa kuwa bado uelewa wao hauwezi kuruhusu uelewa!
 
Hapo Ndipo Pabaya Huwezi Kuivunja Tiss
Hilo Ni Jino La Juu Mdomoni Ukiling'oa Kienyeji UnaweZa Kumuuwa Mgonjwa (Serikali )

Hiyo Haina Tofauti Na PCCB Ambayo Nayo Ni Jino La Juu Mdomoni

Kwani amekuambia TISS iko kwa ajili ya kuilinda serikali?
 
Back
Top Bottom