Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

iyo taasisi ikivunjwa wanapelekwa wapi sasa? izo skills na knowledge c threats nyingine wakikaa bila kazi au embu nielewesheni
Ukiambiwa kuvunjwa haimaanishi kufutwa kwa taasisi, ni kuibadiri mfumo wa utendaji mpaka jina.
 
Mkuu TISS sio kama bodi ya korosho kule lindi useme unaweza kuivunja tu anytime...utatengeneza tatizo zaidi ya hili....solution Bunge limuwajibishe sizonje na vibaraka wake tu
Hasa Bashite aliyekabidhiwa brigade nzima ya tiss kikiwemo kikosi cha watekaji na watesi
 
tissivunjwe.png
Kuna namna nyingi za kushughulikia yanayoendelea nchini sasa hivi na hasa madai makali dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mengi tumeshazungumza juu ya Idara hii na kwa muda mrefu. Bahati mbaya inaonekana hata wabunge wetu hawajaona njia rahisi na ya haraka ya kusafisha idara hii. Tayari inaonekana wapo wabunge wengi kutoka pande zote mbili ambao wanakubaliana kuwa kuna tatizo fulani katika Idara. Sasa kwanini wabunge wasitumie umoja wao huu wa misimamo kufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao?

Wabunge ndio watunga sheria wa nchi hi (law makers). Rais hatungi sheria hata moja; yeye kwake ni kuzipitisha tu. Siyo tu wabunge wanatunga lakini pia wanaweza kufanya marekebisho sheria na Katiba!

Sasa kuna pendekezo la Zitto kuchunguza matukio mbalimbali ambayo yanadaiwa kutokea hivi karibuni na Idara kuhusishwa. Njia hii ya Kamati Teule inaweza kutangulia – kama alivyodokeza – mabadiliko yoyote ya idara. Kamati Teule inaweza kuwaita watendaji na wakuu wote wa idara za usalama na kuwahoji chini ya kiapo – mbele ya camera au nje ya camera – na kutaka kujua nini kinaendelea. Na kwa vile Kamati ina nguvu za kibunge na mahakama inaweza kumlazimisha yeyote kati yao kufika mbele ya kamati hiyo au kuagizwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya kamati hiyo.

Hiyo inaweza kuwa ni njia sahihi ya kutaka kutafuta ukweli. Pamoja na kuwaita hawa wote inaweza kuwaita hata waathirika wa vitendo hivi. Bashe kwa mfano anaweza kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kutoa ushahidi wa madai ya kuwa kuna “mawaziri” ambao wamempa taarifa kuwa yeye ni mlengwa wa kutekwa; Zitto mwenyewe vile vile n.k Lengo ni kutaka kujua ukweli zaidi ili watakapotaka kufanya mabadiliko wajue wapi pa kuanzia.

kipilimba-e1491927638963.jpg

Mkurugenzi wa TISS Dkt. Modestus Kipilimba
Hata hivyo, hilo linahitaji kuungwa mkono sana na wabunge wa CCM. Njia ya pili ambayo binafsi naipenda zaidi kama njia ya haraka ni kwa wabunge wenye kuona tatizo hasa – Bashe, Ridhiwani, Zitto, na wengine wakutane pamoja na kuandaa mswaada wa pamoja (bipartisan bill) ya kuivunja Idara ya Usalama wa Taifa na kuiunda upya ikiwa imetengenezwa kukidhi mahitaji ya kiusalama ya taifa hili na ikisimamiwa moja kwa moja na Bunge. Mswada huu uletetwe hata kwa hati ya dharura ili kabla ya Bunge hili kuisha usomwe unavyohitajika na upitishwe na Bunge na hatimaye upelekwe kwa rais kwa kuudhinisha.

Nina uhakika Rais Magufuli ataridhia kwani atakuwa amesaidiwa kazi ambayo labda ingemchukua muda yeye mwenyew ekuifanya. Na kama hatoridhia na kutishia Veto Bunge linaweza kuipiku veto hiyo kwa kura nyingi na kumlazimisha aisaini na kama haitowezekana basi Bunge litavunjwa na watu watarudishwa kwenye uchaguzi mkuu mpya ambapo wananchi watapata nafasi ya kwenda kuchagua wabunge na Rais mwingine kulingana na ajenda watakazosimama nazo.

Lakini kulalamika tu wakati nyenzo wanazo ni kupoteza muda wa watu. Ni wakati wa kufanya wanachoamini ni sahihi kufanya na wana uwezo wa kukifanya. Lakini pia utakuwa ni wakati wa watu kuhesabiwa. Kwa sisi wengine ambao tumekuwa tukilalamikia idara hii kwa muda mrefu tunaona labda hii ni nafasi ya pekee ya kuileta Idara hii kwenye karne ya 21. Inapofikia watu tena wazito wanadai kuwa Idara inajihusisha au watumishi wake wanajihusisha na vitendo ovya kighaidi hakuna namna namna nyingine ya kufanya isipokuwa kuivunja idara hiyo na kuiunda upya toka chini. Mkitaka mawazo tupo wengine tunaweza kuwasaidia.
Mzee Mwanakijiji, mapendekezo mujarabu lkn hata hivyo itakuwa ajabu kuivunja TISS kwa lawama za utekaji watu ilihali kwa kifupi na kwa maneno yaliyonyooka..failures zote hapa nchini, uwekezaji mbovu, viongozi wabovu, rushwa kubwa (BOT), biashara haramu nk wa kulaumiwa ni TISS, tumesema nyakati tofauti kwamba katiba basi iseme angalau kila tunapochagua Rais mpya 90% ya TISS au yote iwe timu mpya..haya mambo ya kukaa TISS kama sultani hayafai..na kwa kweli yule anaefanya kazi inavyopaswa akiwa TISS miaka 10 kuwa pale ni mzigo mzito ataomba yeye mwenyewe kubadilishiwa kazi..lkn kwa vile labda kuwa TISS maslahi ndio kitu cha kwanza sio ajabu mtu yupo TISS miaka 20, mambo ya namna hii hayafai,,Mungu hajaumba Superman, theres no superman in this world, wapo watz hodari wenye uwezo wa akili kupita hata hao walioko TISS sasa..angalia tu TISS imeshindwa kitu kdg kabisa cha kuscout watu wazuri wenye vipaji tofauti kwa manufaa ya nchi yetu siku zote wanachojua ni kurecycle watu hawana namna nzr ya kuidentify good people of this nation whereever they are waisaidie nchi ipige hatua..wabunge wachukue hatua stahiki wasipige kelele tu tunataka VITENDO!!!
 
Lakini chanzo cha yote haya ni Bashite...kweli Gwajima ana wakati mgumu sana kumng'oa huyu zero brain
 
Watu wanaichukia Tiss coz Anko Magu ndo kawamwaga kila sehem...babdarin/ airport hata makazini...deal zao hazifanikiw tayar washakamatwa sasa wanajua njia sahihi ya kuepukana na huu ukata n kuirudsha Tiss ya Jk ya kubebana... JPM kaza baba mpka Tz iwe mpya kifikra hizi kelele zao zisikutishe sisi wanyonge ndo wengi tupo nyuma yako.
 
Osama na Sadam waliwahi kuwa maajenti wa CIA ona kilichotokea mwisho.
USalama wa Taifa bado ipo na sidhani ni tatizo hata kidogo.
Tatizo lililopo ni ni wale maafisa wa Usalama wanaopewa kazi michepuko za Rais na watu kama Bashite hawa hawapokei order toka kwa Mkurugenzi wao ni Mazimwi ndani ya usalama wa Taifa.
Wanajulikana lakini si rahisi kuwadhibiti kwa sababu mikono yao imechafuka damu za watu kwa niaba ya rais na wateule wake. Tabia zao ni sawa na Simba liyekula nyama ya mtu.
Dawa ni kuwamaliza kwa risasi au kuwapeleka uhamishoni nje ya nchi
 
Hao wabunge wanaweza kuthibitisha juu ya hicho wanachokinena kuwa TISS ndio wanaoteka watu?
 
Ni sawa,lakini kwa sasa bado hatujafikia kiwango cha kuvunja TISS yetu.Ni juzi tu ilitusaidia kumtupa nje ya ulingo Lowassa na mafisadi wenzie,hebu fikiria,bila ya TISS kuzuia mifumo ya kuiba kura kielektroniki aliojitengenezea Lowassa na Mercenaries wake kutoka Israel,leo Lowassa angekuwa Rais

Jamani sisemi tuvunje halafu tusiwe na usalama wa taifa tena; la hasha. Hata wakati mwingine kumtibu mgonjwa inabidi umpasue au hata uondoe kiungo kabisa ili kumpa uzima!
 
Top wao huyo[emoji115]

Anaulizwa maswali anaongea definition ya anachoulizwa yaani kukariri tu!

We acha tu!
 
Ndugu Mwanakijiji, tatizo sio sheria zetu, tatizo ni watu watu wa hizo taasis.

Hawamwogopi mtu, hawatii sheria. Hata ukishusha sheria na taratibu kutoka mbinguni, bila watu kiziheshimu; ni kutwanga maji kwenye kinu.
 
Naunga Mkono Hoja,TISS ya SASA ni JIPU,Ni Genge la WAUAJI na WAPIGAJI(CONMEN),WENGI WAMEJENGA MAGHOROFA YA MAANA KWA FEDHA ZA BLACKMAILING NA KUTUMIKA NA WANASIASA KINA BASHITE...IVUNJWE TU MAANA KAZI WALIYOBAKI NAYO NI KUTEKA/KUUA TU BASI,ULIMBOKA NAYE NI MJINGA SANA ILITAKIWA AFANYE KAFARA WALE WALI0MTESA WOTE WATEKETEE NDIO DAWA YAO.
 
Wewe pimbi kweli. Unadhani TISS ilitengenezwa kwa sheria za mbinguni?

Hizo ndugu yangu ni ndoto za abunuasi za kutaka kuivunja idara nyeti kama hiyo. Kwanza kumbuka kila idara ile ina kanuni zake za kuiendesha. Pili bunge halina uwezo huo. Yaani idara ya usalama wa taifa haiendeshwi kisiasa kama chama. Na kumbukeni kuwa kunamafunzo maalumu ya usalama wa taifa. Hilo msahau mkiongea sana mtaishia kufa kqa bp za vitisho. Na kutekwa.
 
tissivunjwe.png
Kuna namna nyingi za kushughulikia yanayoendelea nchini sasa hivi na hasa madai makali dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mengi tumeshazungumza juu ya Idara hii na kwa muda mrefu. Bahati mbaya inaonekana hata wabunge wetu hawajaona njia rahisi na ya haraka ya kusafisha idara hii. Tayari inaonekana wapo wabunge wengi kutoka pande zote mbili ambao wanakubaliana kuwa kuna tatizo fulani katika Idara. Sasa kwanini wabunge wasitumie umoja wao huu wa misimamo kufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao?

Wabunge ndio watunga sheria wa nchi hi (law makers). Rais hatungi sheria hata moja; yeye kwake ni kuzipitisha tu. Siyo tu wabunge wanatunga lakini pia wanaweza kufanya marekebisho sheria na Katiba!

Sasa kuna pendekezo la Zitto kuchunguza matukio mbalimbali ambayo yanadaiwa kutokea hivi karibuni na Idara kuhusishwa. Njia hii ya Kamati Teule inaweza kutangulia – kama alivyodokeza – mabadiliko yoyote ya idara. Kamati Teule inaweza kuwaita watendaji na wakuu wote wa idara za usalama na kuwahoji chini ya kiapo – mbele ya camera au nje ya camera – na kutaka kujua nini kinaendelea. Na kwa vile Kamati ina nguvu za kibunge na mahakama inaweza kumlazimisha yeyote kati yao kufika mbele ya kamati hiyo au kuagizwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya kamati hiyo.

Hiyo inaweza kuwa ni njia sahihi ya kutaka kutafuta ukweli. Pamoja na kuwaita hawa wote inaweza kuwaita hata waathirika wa vitendo hivi. Bashe kwa mfano anaweza kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kutoa ushahidi wa madai ya kuwa kuna “mawaziri” ambao wamempa taarifa kuwa yeye ni mlengwa wa kutekwa; Zitto mwenyewe vile vile n.k Lengo ni kutaka kujua ukweli zaidi ili watakapotaka kufanya mabadiliko wajue wapi pa kuanzia.

kipilimba-e1491927638963.jpg

Mkurugenzi wa TISS Dkt. Modestus Kipilimba
Hata hivyo, hilo linahitaji kuungwa mkono sana na wabunge wa CCM. Njia ya pili ambayo binafsi naipenda zaidi kama njia ya haraka ni kwa wabunge wenye kuona tatizo hasa – Bashe, Ridhiwani, Zitto, na wengine wakutane pamoja na kuandaa mswaada wa pamoja (bipartisan bill) ya kuivunja Idara ya Usalama wa Taifa na kuiunda upya ikiwa imetengenezwa kukidhi mahitaji ya kiusalama ya taifa hili na ikisimamiwa moja kwa moja na Bunge. Mswada huu uletetwe hata kwa hati ya dharura ili kabla ya Bunge hili kuisha usomwe unavyohitajika na upitishwe na Bunge na hatimaye upelekwe kwa rais kwa kuudhinisha.

Nina uhakika Rais Magufuli ataridhia kwani atakuwa amesaidiwa kazi ambayo labda ingemchukua muda yeye mwenyew ekuifanya. Na kama hatoridhia na kutishia Veto Bunge linaweza kuipiku veto hiyo kwa kura nyingi na kumlazimisha aisaini na kama haitowezekana basi Bunge litavunjwa na watu watarudishwa kwenye uchaguzi mkuu mpya ambapo wananchi watapata nafasi ya kwenda kuchagua wabunge na Rais mwingine kulingana na ajenda watakazosimama nazo.

Lakini kulalamika tu wakati nyenzo wanazo ni kupoteza muda wa watu. Ni wakati wa kufanya wanachoamini ni sahihi kufanya uwezo wa kukifanya. Lakini pia utakuwa ni wakati wa watu kuhesabiwa. Kwa sisi wengine ambao tumekuwa tukilalamikia idara hii kwa muda mrefu tunaona labda hii ni nafasi ya pekee ya kuileta Idara hii kwenye karne ya 21. Inapofikia watu tena wazito wanadai kuwa Idara inajihusisha au watumishi wake wanajihusisha na vitendo ovya kighaidi hakuna namna namna nyingine ya kufanya isipokuwa kuivunja idara hiyo na kuiunda upya toka chini. Mkitaka mawazo tupo wengine tunaweza kuwasaidia.

Rais keshasema uhuru wa kusema una mipaka yake. Watu wanajifanya kuiga Marekani lakini hawaijui Marekani. Hata Marekani kazi ya usalama wa taifa ni pamoja na kufungia nyimbo na kupoteza bila ya kesi watu tishio kwa taifa.
Na yanayofanywa na usalama wa taifa mengine si maamuzi ya rais. Hivyo ni upuzi kumlaumu rais. Na ni upuzi pia bunge kuhoji mabosi wa usalama wa taifa. Bunge lenyewe limejaa upinzani mtupu.
 
Usalama wa Taifa inabidi uwe usalama wa Taifa kwelikweli, Yaani kwa mambo makubwa ya maslahi ya Nchi, Siyo maslahi madogo madogo ya kisiasa ya mtu yeyote!. Yaani kiufupi haitakiwi Usalama wa Taifa kutumika kuwanyamazisha watu wasimkosoe mtawala, wakati katiba ya nchi inaruhusu hilo, haitakiwi usalama wa Taifa kuwa ni kikosi fulani cha utesi kwa wale wanaopinga mienendo ya walioko madarakani, ikifanya hivi inajishusha sana kutoka kuwa usalama wa Taifa hadi kuwa usalama wa kisiasa wa mtu!.ni aibu kufikia huko, Intelijensia makini duniani zikisikia tumefika huko zitatushangaa!

Umewahi kusikia Mossad wakimkingia Kifua Netanyahu asisemwe kwa sababu ya corruption charges zinazomkabili?

Au Umewahi kusikia Richard Nixon akikingiwa kifua na FBI au Homeland Security kwa kashfa yake ya Watergate?

Au Bill Clinton kukingiwa kifua asisakamwe na wapinzani wake kwa ile kashfa ya Monica Lewinsky?

Haifai kutumia torture kwa raia wanyonge wasiojua hata bunduki inashikwaje, This is wrong!.
Matendo ya ajabu ya aina hii yatakuja kuradicalize watu na ni hatari sana tukifika huko!

Kuna mambo mazito ya kudeal nayo, siyo kusilence dissent kwa kutumia mbinu za kupandikizs hofu kwa umma!

TISS iwaache wanasiasa wajibebe, na wabebe consequence za maamuzi yao, Isiwakingie kifua maamuzi yao yakibackfire!
 
Wewe umekipaka kweli kweli. Trump anazogoana na kubadilisha viongozi wa CIA na FBI unafikiri ni kwanini. Usalama wa taifa juu ya yote unamlinda rais na serikali yake.
 
Tatizo haliko TISS. Liko katika katiba, sheria na mfumo mzima wa utawala wa nchi unaotoa fursa kwa mtu mmoja na maswahiba zake kuhodhi madaraka ya dola na kuyatumia atakavyo.
 
Back
Top Bottom