Ni wakati muafaka CCM irudi kusimamia Itikadi na Misingi yake

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Asalam,

1. Ninaipenda CCM na Ni Mwanachama wa CCM
2. Ninaipenda Nchi yangu na ni mzalendo hasa.
3. Ninaulewa wa itikadi na misingi ya saisa ya CCM
4. Ninapinga Mkataba wa sasa wa DPW, nitauunga ukirekebishwa.
5. Ninawaheshimu viongozi wa Chama, ninawakosoa wanaokosea (rejea mwongozo wa CCM WA 1981, apumzike mahala pema peponi Mzee Comrade Kingunge. Ni Mwalimu wangu

MAKOSA TUNAYOPITIA KWA SASA CCM
1. Tumejenga umimi na kujikuza (personality cult)
2. Tumeshindwa kupambana na rushwa
3. Vikao vya Chama vikubwa CC NA NEC hazina tena watu wenye kujua wanachofanya. Pamejaa ngono na mapenzi binafsi. Pamejaa wapenda karamu (hedonists and extravagants).
3. Sasa tumepoteza Mwelekeo, hatujui tunachotaka, hatujui tunakoenda, hatujui kiongozi wetu, hatujui miongozo yetu.
4. Tumepoteza itikadi yetu. Aliepo kaja na yake anaita 4R. Najaribu kuitafuta ikowapi siioni kwenye misingi na itikadi ya Chama Chetu. Kwa ufupi, Aliepo kaunda Chama Chake lkn sio CCM niijuayo.

SASA TUFANYAJE
1. Nidhamu ya CHAMA irudi, kwa sasa hatujui mwenezi na msemaji ni nani? JK, CHONGOLO, KINANA, MNDEME, ETC. kila mmoja anaongea kwa wakati wake. Wa Hangover mnajua, hawa wakapate supu ya utulivu walale.
2. Mwenyekiti sasa akae kitini, ni kama hajui anachofanya. Ni kama anaigiza. Mwenyekiti lazima aongee kutoa mwelekeo. Haongei, na waoambe wanamwambia ukimya ndio UONGOZI (kicheko). Ongea Mwenyekiti.
Mwisho tukosoane (Mwongozo wetu wa 1981) tuseme wazi, na Turudie ahadi 10 za Mwana TANU.

PUMZIKA SASA MSTAAFU
 
Ni ajabu viongozi wa siasa kubishana na nyaraka za mabaraza ya kidini ambao wanaongoza waumini wengi kushinda wanachama wa vyama vyao..

CCM ina wanachama 12M plus, ina TEC ina waumini 30M plus...

Wale ni wachungaji na wanachunga kondoo wao..
 
Back
Top Bottom