Tabia ya TANESCO kukata umeme imekuwa kero

Vincenzo Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2020
12,164
25,466
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tanga limemlipa Mkazi wa Mwamboni, Tanga, Mwamvua Maliki fidia ya Tsh. 778,000 baada ya kuunguliwa vitu vyake vya ndani August 31,2022 kutokana na hitilafu ya umeme iliyosababishwa na waya wa umeme kukatika na kudondokea nyumba yake.

Baada ya Zimamoto kuja na kufanikiwa kuzima moto huo TANESCO walitaka kuondoka tukawafuata na kuwaambia twendeni huku kuna shoti kubwa imetokea ndio wakaja kupiga picha na kunihoji maswali juu ya tukio hilo mara baada yahapo wakaondoka bila msaada wowote.’’

Mwamvua amesema alipata msaada kutoka kwenye kipindi cha radio kinachotolewa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma ya za Nishati na Maji (EWURA CCC ) juu ya haki za Mteja na fidia zinazotolewa kwa Mteja mwenye changamoto juu ya huduma za nishati na maji ndipo alipopata msaada wa changamoto iliyokuwa inamkabili.

Baada ya kusikiliza kipindi cha radio nilipata mawasiliano yao na hivyo nilifika ofisini kwao Febr 14,2023 nikajaza fomu ya malalamiko ya kudai fidia ya vitu vilivyoungua baada ya hapo EWURA ili kuja na kunisikiliza Mimi pamoja na TANESCO mara baada ya kikao cha usuluhishi ndipo EWURA ilikuja na muafaka wa TANESCO kunilipa fidia ambapo nililipwa Tsh. 778,000 October 13,2023’’
 
Back
Top Bottom