Kiraka Kikuu
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 5,903
- 1,983
Wapinzani wao kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu.
Nakuona kipaza sauti cha mnafiki SITTA!
Wapinzani wao kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu.
Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora, alisema Mnyika na viongozi wengine wa kambi ya upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa kuelekea kupatika kwa katiba mpya, badala ya kuhangaika kutatua kero za wananchi.
Chanzo: Jambo leo
Ruge ni Al shaabab nasikia, wana jf mnijuze katika hili.....!
ELIAHKAMWELA,Hata mimi nasikia kuwa unasikia kwamba Rage ni AL Shabab
mbunge wa jimbo la tabora mjini, ismail aden rage (ccm) amemjia juu mbunge wa ubungo, john mnyika (chadema) akimtaka kuacha kuubeza uteuzi wa mwenyekiti na mkurugenzi mpya wa tume ya taifa ya uchaguzi (nec), uliofanywa na rais jakaya kikwete hivi karibuni. Badala yake, amemtaka afahamu kuwa, yote yanayofanywa na rais kikwete yamo ndani ya mamlaka yake kikatiba.
jamani, mwambieni mnyika aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kupinga kila kitu. Hivi rais amekosea wapi alichokifanya si kimo ndani ya katiba ya nchi ambayo ilimpa rais kuteua tume iliyosimamia uchaguzi mkuu uliopita na ambao mnyika alishiriki na kushinda? alihoji.
Rage, ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoani tabora, alisema mnyika na viongozi wengine wa kambi ya upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa kuelekea kupatika kwa katiba mpya, badala ya kuhangaika kutatua kero za wananchi.
Alisema kiongozi wa kweli ni yule anayeguswa na matatizo ya mwananchi, na si anayetumia muda mwingi kupinga kila jambo, hata ambalo mwananchi wa kawaida halimgusi sana.
Chanzo: Jambo leo
au wewe simba nin?Unahitaji tiba mbadala ya 'Dr.ndodi'.ili uwe timamu upatekujua alofanya Mh.mnyika,
fanya ivo kaka angu! Pamoja na mwenzio wakurogwa!
Lol!
Wapinzani wao kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu.
huyu msomali vipi..rage hujui wewe si mtanzania kwa kuzaliwa.acha wazawa waongee mambo yao,,
1.Kujenga Machinga Complex mbili moja, Manzese na ingine Ubungo
2. Kujenga soka la vyakula Tandale
3. Kuleta maji kimara pamoja na Ubungo, Sinza,
4. Kujenga barabara Kimara Bonyokwa na Temboni.
5. Kutoa ajira kwa vijana
Unaonaje uanzishe sredi nyingine uulize hayo uyasemayo? Maana hapa unataka kutuvuruga na kututoa nje ya mada,Tafakari chukua hatua.
Ritz,
Asante kwa maoni yako. Hata hivyo umetaja ahadi nyingine ambazo zijawahi kuzitoa wakati wowote kwenye kampeni zangu popote. Sijawahi kuahidi machinga complex mbili, kwa sababu naamini kwenye uzalishaji na huduma zaidi ya uchuuji. Tandale haipo katika jimbo la Ubungo, ipo Jimbo la Kinondoni; hivyo ahadi uliyoitaja sijawahi kuitoa. Kuhusu maji, barabara na ajira; ahadi zangu zilikuwa tofauti na ulivyozieleza; kwa kuwa naelewa vizuri kuwa kazi ya mbunge ni kuwakilisha, kuisimamia serikali na kutunga sheria. Ahadi zangu wakati wa kampeni niliziandika kwa ajili ya rejea kwa sababu niliamini ni mkataba baina yangu na wapiga kura. Mara baada ya kuchaguliwa nilizirudia hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/91961-ujumbe-wa-mbunge-shukrani-twende-kazi.html wakati wa kuwashukuru ili kuunganisha nguvu ya umma katika utekelezaji na pia upatikane msingi wa kupima utekelezaji wa ahadi husika katika kipindi cha miaka mitano. Kwa mwaka huu wa kwanza nimekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kutoa mrejesho wa masuala mahususi, unaweza kufanya rejea tu humu. Lakini kwa kuwa tunaelekea mwisho wa mwaka nitatoa pia taarifa nyingine ya ujumla; na pia nitaelekeza zitolewe taarifa za kata kwa kata. Nakutakia heri ya Xmas na mwaka mpya na tuendelee kushirikiana katika utumishi wa umma.
JJ
au wewe simba nin?