Ni vipi ninaweza kumfanya mke wangu awe ‘smart’?

Ni vipi ninaweza kumfanya mke wangu awe ‘smart’?

Habari za wakati huu wakuu?

Mimi niko na mke na mtoto
Maisha yetu bado yako chini kwa kiasi. Sote kiwango cha elimu ni darasa la saba

Kimwonekano tunalingana maumbo hatupishani sana ila nimempita miaka kumi.

Kifikra namuona kama yupo chini mno, nimewahi kufuatilia stori zake na wanawake wenzake nimeona hoja zake ni nyepesi sana mpaka natamani kumwambia awe msikilisaji tu lakini nashindwa

Mimi kwa haraka haraka watu hawadhanii kama ni std seven lakini yeye kwa kweli gepu ni kubwa.
Ndani ya nyumba sijawahi kuona ushauri wake au mkakati wake wa kuinuka, yeye akipata chakula tu basi.
Kabila mnyaturu mimi mchaga.
Hapo awali kabla ya kumuuo alikua house girl kwa kipindi chote

Sasa natamani asiwe jinsi alivyo, natamani awe wa kimjini mjini, maana anaonekana ni shamba hivi, awe walao kama wadada walio soma hivi

Yaani natamini awe mwanamke smart hivi

Ushauri please .

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii kitu inanitesa mno, wangu shule kaenda ila ni bongo lala kwakweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia jaribu kuona anapenda nini, kama ni fashion mtaftie majarida yanayohusiana na hayo,mpeleke kwenye matamasha yao,kama ni mapishi mpeleke hata kwa Open Kitchen (simjui jina lake ila anayo page Instagram) anaweza kumsaidia kumpa orientation, usichoke kumfundisha in a soft way, pia watoto wenu nao wape exposure kama uwezo upo wapeleke shule nzuri, nawe jielimishe ili mazingira yote yanayomzuka yatamuinfluence kubehave unavotaka
 
Oa kimwanamke kinachopenda usafi,na kinachojua kuchagua pamba Kali na kiwe na mwili wa kupendezwa na hzo nguo
 
Kua nae karibu tuu mtoe matembez sehem za kisasa mtafutie kitu cha kumweka busy na aanze kusoma vtabu.
 
Mkuu wewe unajishughulisha na nini samahani lkn nimeuliza hvy sababu kama umejiajiri au una miradi yako.
Hapa ndio sehemu anaweza kubadilikia. Yaan mfanya awe partner katika biashara huko atakutana na watu wa kaliba tofauti na kila siku atajifunza kitu kipya plus changamoto za biashara mbona dishi litamkaa sawa
 
Hapa ni kweli tupu umeongea mkuu,ingawa wanawake sampuli hii wanaudhaifu wa ujuzi wa mambo (ambayo sio lazima sana ajue)lkn wako vizuri katika ustawi wa familia zao.Mm kwa kweli najivunia kuwa na mwanamke drs la saba ingawa hanijengi ki fikra.
Pia jaribu kuona anapenda nini, kama ni fashion mtaftie majarida yanayohusiana na hayo,mpeleke kwenye matamasha yao,kama ni mapishi mpeleke hata kwa Open Kitchen (simjui jina lake ila anayo page Instagram) anaweza kumsaidia kumpa orientation, usichoke kumfundisha in a soft way, pia watoto wenu nao wape exposure kama uwezo upo wapeleke shule nzuri, nawe jielimishe ili mazingira yote yanayomzuka yatamuinfluence kubehave unavotaka
Naona mnataka kumpeperushia ndege wake mangi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpeleke shule....atakuaje kama wanawake waliosoma wakati hajasoma


mpeleke hata Qt miaka miwili
 
Back
Top Bottom