Ni vipi ninaweza kumfanya mke wangu awe ‘smart’?

Ni vipi ninaweza kumfanya mke wangu awe ‘smart’?

Pendaelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
13,034
Reaction score
38,505
Habari za wakati huu wakuu?

Mimi niko na mke na mtoto. Maisha yetu bado yako chini kwa kiasi. Sote kiwango cha elimu ni darasa la saba. Kimwonekano tunalingana maumbo hatupishani sana ila nimempita miaka kumi.

Kifikra namuona kama yupo chini mno, nimewahi kufuatilia stori zake na wanawake wenzake nimeona hoja zake ni nyepesi sana mpaka natamani kumwambia awe msikilizaji tu lakini nashindwa.

Mimi kwa haraka haraka watu hawadhanii kama ni std seven lakini yeye kwa kweli gepu ni kubwa. Ndani ya nyumba sijawahi kuona ushauri wake au mkakati wake wa kuinuka, yeye akipata chakula tu basi.

Kabila ni Mnyaturu mimi Mchaga. Hapo awali kabla ya kumuoa alikuwa house girl kwa kipindi chote.

Sasa natamani asiwe jinsi alivyo, natamani awe wa kimjini mjini, maana anaonekana ni shamba hivi. Nataka awe walao kama wadada waliosoma, awe mwanamke smart.

Naomba ushauri tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mchaga, msaidie kumpa exposure mpeleke vacation za maana ambapo atakutana na watu tofauti tofauti, mpeleke short courses hata za British Council zinamtosha, kama una uwezo hama uko uswazi nenda sehemu zilizostaharabika like Masaki, Msasani Mbezi Beach, hata Goba Tegeta Tabata Kinyerezi atleast utamwachanisha na marafiki zake.

Mfundishe jinsi ya kubehave anapokuwa mbele za watu wa kada tofauti n.k
 
Pole sana Mchaga, msaidie kumpa exposure
mpeleke vaccation za maana ambapo atakutana na watu tofauti tofauti, mpeleke short courses hata za British Council zinamtosha , kama una uwezo hama uko uswazi nenda sehemu zilizostaharabika like Masaki ,Msasani Mbezi Beach, hata Goba Tegeta Tabata Kinyerezi atleat utamwachanisha na marafiki zake. Mfundishe jinsi ya kubehave anapokuwa mbele za watu wa kada tofauti,n.k
I second that, na pia amtengeneze ki fikra.

Pengine mke bado anajiona yeye hana thamani kwa sababu alikuwa housegirl.
 
MTU HUWA ANAATHIRIKA KUTOKANA NA MAZINGIRA ALIYOTOKA NA MAZINGIRA ALIYOPO, KWANZA HILO TAMBUA.
IKISHA KUMFANYA MKE WAKO AWE KAMA WEWE ULIVYO, NI WEWE MWENYEWE KUMFAHAMISHA KWA NJIA ZA UTARATIBU NA URAFIKI, VIPI UNATAKA AWE.

SIO WASOMI WOTE WAPO SMART HAPANA, HILO TAMBUA.

AMA JAMBO LA KUTAKA AWE WA MJINI MJINI, HAPO JITAYARISHE NA MAMBO MENGI SANA AMBAYO HUENDA YAKAKUPELEKEA KWENGINE KABISAAA
 
Naunga mkono hoja za wadau hapo juu pia mnunulie majarida ya kielimu ujasiriamali na biashara muweke mbali na hao marafiki zake maana wanasema ndege wanaofanana huruka pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
Makundi ni mabaya sana hasa kwa wanawake wasio na elimu. Unakuta walioko kwenye kundi wana upeo mmoja. Wote wanapapasa, wako gizani. Ukishaona mke wako yuko kwenye kundi la aina hiyo ujue hata umwambie nini hakusikii.
 
Umenikumbusha nilipotoka, hata mimi nilioa mke ambae tulitofautiana sana umri na elimu, na nilipitia changamoto hizo unazozipitia wewe

Kuna watu wamekupa ushauri mzuri unaofanana na nilivyofanya mimi ongeza na haya mawili

1.onesha upendo uvumilivu na kumjali na usioneshe kukerwa na hiyo hali yake

2. kwa kumuunganisha na makundi ya wanawake (hasa wa kidini) walio eneo tofauti na mnapoishi ili apate fikra mpya za usahihi


Kumbuka uvumilivu ni muhimu na hasa kama umri wake ni mdogo, inaweza ikachukua hata miaka mitano ila ataanza kubadilika taratibu mpaka atafikia kiwango unachohitaji na zaidi ya hapo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
naona una lazimisha umkose yaani kabisa umnunulie smartphone umpeleke seh nzuri kwa miguu akati ataona v8 na watamwomba namba usije ukajichanganya ukamsomesha hapo utajua kwann CCM ni chama cha mapinduzi lakini hakitaki mapinduzi ya fikra

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani matatizo ya mke wake hayahitaji kusomeshwa ila yanahitaji kuelimishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiombe ndio awe wa design ya kununa nuna hata ukiwa JF yeye anaamini unachat na madem wengine, yaani hata ukimuonesha uzi unaoufuatilia yeye hajui ni kitu gani.

Changamoto ni kubwa na hasa anapotema pumba mbele za watu, kikubwa mtafutie mishe itakayomkutanisha mara kwa mara na watu smart. na Kama ni mzuri sana kuna uwezekano akakuzidi u smart wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom